Kuna ukweli kiasi gani kwamba muundo wa sasa wa muungano unaifaidisha ccm kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ukweli kiasi gani kwamba muundo wa sasa wa muungano unaifaidisha ccm kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 2, 2012.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu,
  Katika miaka ya hivi karibuni kumezuka malumbano ya hapa na pale ya baadhi ya wananchi wa pande mbili za muungano kulalamikia muungano. Baadhi yao wamefikia hatua ya kuona ni bora muungano uvunjwe. Wengine wanasema muungano ubaki lakini muundo wake ndiyo uboreshwe kwa kuweka serikali tatu yaani serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano.

  Hivi karibuni nilipata fursa ya kuongea na 'mnene' mmoja ambaye ana nafasi nyeti serikalini. Ni mtu wa makamo na Mungu akimjalia uzima atastaafu utumishi wa umma miaka miwili ijayo. Mzee huyo, alinieleza kwamba ccm haiwezi kuruhusu muungano wa serikali tatu kwa sababu kwa kufanya hivyo itakuwa inajikaanga kwa mafuta yake yenyewe. Tuliongea mengi kuhusu uongozi wa nchi yetu kwa ujumla jinsi ulivyopwaya katika mambo ya msingi na kusababisha hali ya maisha kwa wananchi kueendelea kuwa duni kwa kasi zaidi, ari zaidi na nguvu zaidi. Ni bahati mbaya maongezi yetu yaliingiliwa na mgeni wakati mzee alikuwa anataka kunieleza haswa ni kwa namna gani ccm inafaidika na muundo wa muungano wa sasa.

  Najua jf imesheheni wataalam waliobobea katika tasnia zote. Kwa wenye ufahamu kuhusu hujuma hii ya ccm katika muungano tafadhali karibuni jamvini.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  CCM inafaidika sana na muundo uliopo kwa sababu zote kutoka Zanzibar..
  1. CCM katika chaguzi zote wameshindwa na CUF Zanzibar tena karibu majimbo yote lakini kwa sababu mwenye dhamana ya Mapinduzi na serikali huru ya Zanzibar ni kitengo cha ASP (baraza la Mpinduzi).. CUF imekuwa ikunyimwa Ushindi wa kura hivyo CCM kuwakilishwa na wabunge walioshindwa..Hii ina maana kwamba CCM ilishashindwa siku nyingi sana Zanzibar ktk uchaguzi lakini kwa sababu ya muundo wa Muungano uliotangulia kuunganishwa kwa ASP na CCM, hivyo kuiangusha CCM ni lazima kwanza kuivunja ASP na baraza la Mapinduzi..
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  wabunge zaidi ya 50 watapungua. CCM itaporomoka zaidi
   
Loading...