Kuna ukweli juu ya wizi wa nguvu za giza wa kundi la zungu Arusha?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,155
wanabodi
Kumekua na msg na audio zinazosambaa watu zikiwatahadharisha watu juu ya kundi la zungu jamani wanadai kuwa hawa jamaa wanaiba kwa nguvu za giza huku arusha
Jee kuna ukweli??
 
Hapo ndo watu wa chuga huwa nawaona maboya sana, yaani mtu au kikundi kinasifika na kitambulika kwa kuwa wazee wa ndole (wadokozi wa mifukoni) eti kuanzia miaka ya 90 mpaka leo,
Yaani mnawafuga tu hao jibwa koko eti "mzunguuuu"
Na siku wakikamtwa mitandao inajaa habari "bilionea wa Arusha akamatwa na polisi baada ya kuwasumbua kuanzia miaka ya 90 mpaka leo 2017." Kumbe wapiga ndole waliokubuhuu
Ni chuki tu kina mzunguu ni pick pockets toka miaka ya mwanzo ya 90 hadi leo hakuna uchawi bali wana uzoefu wa kutosha. .. hao wanaowalalamikia kina mzunguu ni wageni Arusha
 
Hao ni watu gani tuwekee hiyo msg tuelewe wanaume wa arusha mnashindwa kuwakamata?
 
wanabodi
Kumekua na msg na audio zinazosambaa watu zikiwatahadharisha watu juu ya kundi la zungu jamani wanadai kuwa hawa jamaa wanaiba kwa nguvu za giza huku arusha
Jee kuna ukweli??
Vizuriii tumpate aliye ibiwa coz hata mimi nasikia wanasema wanatumia nguvu za gizaa kuwaibia watu
 
Haloooo.

Kwa hiyo,

Panya road ni wababe wa watu wa Dar halafu

Zungu na team yake wababe wa Arachuga. ...?
 
Zinasaje ..mm niko Arusha Mjini Katikati kabisa hapa kwa Tojo.. lakini sijawahi sikia hayo Mambo ...mtakua mnaibiana huko Ungalimited not Twn
 
Ni chuki tu kina mzunguu ni pick pockets toka miaka ya mwanzo ya 90 hadi leo hakuna uchawi bali wana uzoefu wa kutosha. .. hao wanaowalalamikia kina mzunguu ni wageni Arusha
huyu ndiyo yule jamaa mmoja mweupe anavaa cheni za silver na bracelet?
 
hawa jamaa wapo ni wazee wa ndole mfukoni wana mbinu nyingi za makoti makubwa ,koti hili hujifanya ana kitu anatafuta au endapo ni kwenye dala dala hujifanyisha kama vile joto limemzidi na kukufunika usione kiachoendelea huku ukiwa umeweka msisitizo kuwa mwenzako anataabika na joto kumbe anakusachi mfuko mmoja kwenda mwingine .mara nyingine hutumiia mbinu ya kukuzuia wakati unashuka kwenye daladala yeye akiwa chini huingiza mkono chini ya siti pale mlangoni kama vile anatoa mzigo uliokwama wewe ukiwa uko ndani ya daladala mmeshasimama tayari kushuka chini foleni haendi kumbe unaibiwa .katika utafiti wangu jamaa hawa wanapatikana maeneo ya kwa mrombo, barabara ya shamsi karibu na dr msemo ,hupenda kutembea wanne au Zaidi ,na hupendelea gari za njiro ,usa na moshi pia gari za kwenda mjohoroni.na pia wana gari yao aina ya noa yenye rangi ya blue na silver ambayo ndio huyu mzungu hutumia ,amejenga maeneo ya bonsite .
kuhusu kesi zao polisi .mazingira ya kazi zao huwa ni magumu kumtia hatiani ,kwani anakuwa na laki mfukoni halafu anaiba . 50000 ukimkamata anatoa laki na kukuonyesha hivyo kujenga mazingira ya kuwa wanatumia dawa au nguvu za giza .kuhusu vipigo wanakutana navyo mara nyingi hivyo wana jihami wanavaa vizuri ,lugha wanayotumia ndani ya dala dala ni nyepesi utasikia anapiga simu za kuuliza biashara zake za fuso, wajijhi wao ni watu wa miaka ya 30-50 . mavazi hujigawa kuna ustadhi huvaa kiustadhi kanzu safi na wanaobaki huvaa kawaida na makoti mikononi . pia hupenda kutumia bahasha za kubwa kwa ajili ya kuzuia abiria wanaposachi upande wa kulia bahasha ataishika na mkono wa kushoto ,akikuta mfuko anaosachi hauna hela au simu atasingizia kuwa kuwa anajisikia vibaya umpishe akae upande wa pili .ushirikiano kufanikisha wizi huu huufanya kwa kumshirikisha dereva wa gari husika na konda na wakishafanisha hushuka popote na mara nyingi hawalipi nauli au watalipa nusu ..
 
Ndo huyo huyo wako wanne wanakuwa na Gari aina ya Noah na Escudo
Hao ni watu gani tuwekee hiyo msg tuelewe wanaume wa arusha mnashindwa kuwakamata?
Wakamatwe ili iweje wakati wako peace wnachokipata wanawagawia msela? ? Na siku zote wanawaibia wanataka kisoro kwa hiyo sio kosa Lao ni kosa lako kukaa kisoro ukaibiwa! ! So wajanja huwa wanapotezea huwezi wekea bero masela kisa uboya wako
 
hawa jamaa wapo ni wazee wa ndole mfukoni wana mbinu nyingi za makoti makubwa ,koti hili hujifanya ana kitu anatafuta au endapo ni kwenye dala dala hujifanyisha kama vile joto limemzidi na kukufunika usione kiachoendelea huku ukiwa umeweka msisitizo kuwa mwenzako anataabika na joto kumbe anakusachi mfuko mmoja kwenda mwingine .mara nyingine hutumiia mbinu ya kukuzuia wakati unashuka kwenye daladala yeye akiwa chini huingiza mkono chini ya siti pale mlangoni kama vile anatoa mzigo uliokwama wewe ukiwa uko ndani ya daladala mmeshasimama tayari kushuka chini foleni haendi kumbe unaibiwa .katika utafiti wangu jamaa hawa wanapatikana maeneo ya kwa mrombo, barabara ya shamsi karibu na dr msemo ,hupenda kutembea wanne au Zaidi ,na hupendelea gari za njiro ,usa na moshi pia gari za kwenda mjohoroni.na pia wana gari yao aina ya noa yenye rangi ya blue na silver ambayo ndio huyu mzungu hutumia ,amejenga maeneo ya bonsite .
kuhusu kesi zao polisi .mazingira ya kazi zao huwa ni magumu kumtia hatiani ,kwani anakuwa na laki mfukoni halafu anaiba . 50000 ukimkamata anatoa laki na kukuonyesha hivyo kujenga mazingira ya kuwa wanatumia dawa au nguvu za giza .kuhusu vipigo wanakutana navyo mara nyingi hivyo wana jihami wanavaa vizuri ,lugha wanayotumia ndani ya dala dala ni nyepesi utasikia anapiga simu za kuuliza biashara zake za fuso, wajijhi wao ni watu wa miaka ya 30-50 . mavazi hujigawa kuna ustadhi huvaa kiustadhi kanzu safi na wanaobaki huvaa kawaida na makoti mikononi . pia hupenda kutumia bahasha za kubwa kwa ajili ya kuzuia abiria wanaposachi upande wa kulia bahasha ataishika na mkono wa kushoto ,akikuta mfuko anaosachi hauna hela au simu atasingizia kuwa kuwa anajisikia vibaya umpishe akae upande wa pili .ushirikiano kufanikisha wizi huu huufanya kwa kumshirikisha dereva wa gari husika na konda na wakishafanisha hushuka popote na mara nyingi hawalipi nauli au watalipa nusu ..
Duuuuhh aiseee mbona sasa mnawafaham kwa nini msiwatie nguvuni??
 
Back
Top Bottom