Kuna ukweli hapa

hahaha, mie nishaenda hospitali moja ya binafsi tena ni kubwa tu (ina jina), nilikuwa najisikia maumivu kwenye tumbo mkono wa kushoto karibia na nyonga, nikafanyiwa ultrasound. Kwenye kupewa dawa nikapewa dawa za UTI (kumbuka sikupima hata mkojo wala nini zaidi ya ultrasound), nikapewa na dawa zingine ambazo sikujua ni nini. Nilivyofika nyumbani nikameza dawa halafu nikawasha pasi kuanza kunyoosha nguo zangu. Salaaale, ilikuwa kila nikinyoosha ndio usingizi unazidi. NIkaamua kuzima pasi na kuchomoa. Nililala fofofo. Nilipoamka, nikaona isiwe shida, nikakumbuka kuna kaka tulisoma naye, japo yeye alikuwa ni mfamasia wa hospitali ya mkoa fulani huku kanda ya ziwa, aliamua kusomea na fani nyingine zaidi ya huo ufamasia.
Nikamwelezea zile dawa zilivyo nitenda, pia nikamweleza na ugonjwa wangu. Akaniambia hebu nitumie sms ya jina la hiyo dawa, nikamtumia.
Uwiiiiiii, sikuamini alichoniambia!!! alisema hivi "weee...... (akitaja jina langu) mbona hizi ni dawa za vichaa? kwani wewe uliwaambia unaumwa nini? au mwonekano wako ukoje siku hizi....)

mxeweeeu, nilichofanya nilitupa yale madawa na yale ya UTI, sina hamu na hospitali za binafsi hata kama inapokea BIMA YA AFYA.
Dawa moja inaweza kuwa na matumizi mengi nishawahi tumia oral chlorumbucil kwa ajiri ya figo ila ni ant cancer na inakubalika eorld wide kuwa inaweza saidia kwa certain condition.
 
Habari za sahizi wadau? Me mwenyewe Naona Kama kuna tatzo hvi nimeeenda kupima hospital binafsi nkaambiwa nna UTI sasa dawa nliopewa ni vidonge kwa maelezo ya doctor ni antibiotics sasa nimejarbu kuifuatilia hii dawa (DIOMYCIN/ ERYTHYROKANT) mtandaoni nimeona Kama ni dawa ya macho sasa sielew wadau naombeni Masada wa mawazo kwa wenye utaalam
 
Picha ndo hii wadau
IMG_20190511_113152.jpeg
 
Back
Top Bottom