Kuna ukweli gani? (LUGHA NA UKABILA)

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Katika mambo ambayo mpaka leo sijapata jibu ni kuhusu Lugha inavyoweza changia ukabila na mpasuko katika nchi hii ya Tanzania.
Nchi hii ina makabila takribani 120 na yote yana Lugha zao lakini mara nyingi hazitumiki katika sehemu rasmi kama redioni,magazetini,shuleni na maofisini na kutotambuli kama ni lugha halali huku wengi wakiwa na hisia na imani waliyo mezeshwa kuwa zinaleta matatizo mpaka kuligawa taifa.Nakumbuka mbunge mmoja kama sikosei kutoka CDM alichangia bungeni mwaka huu 2011 kuhusu kuruhusu watu watumie lugha zao katika matangazo ya maredioni na magazeti ili lugha hizi zisife na ilikuwa ni wizara ya utamaduni na michezo kama sikosei.Wengi wa wachangiaji walimponda na kumbeza kuwa mwl.nyerere alikataza,siyo uzalendo eti taifa litagawinga mfano Mama Rwakatare aliponda sana.
Tunaweza kujikumbusha wakati magazeti yanatumia lugha hizo kama kule BK lilikuwepo Rumuli,Bukya na Agandi,je ulikuwepo mpasuko? Kuna ata Biblia imeandikwa kwa kihaya ukienda kwenye magazeti na redio zipo zinatangaza kwa lugha zao katika nchi kama uganda ndo usiseme,S.Afrika mpaka ata mashuleni zinafundishwa hadi chuo.
Mtazamo wangu ni kwamba lugha hizi kwa miaka ijayo zitapotea na kubaki as a dead history kabisa na siyo kweli kuwa kuwepo na kutumika lugha hizo kunaleta mpasuko wa nchi.Mada ndefu nashukuru kwa uvumilivu na ninawasilisha.
 
japo hujaweka mchanganuo mzuri lakini hoja yako ni ya msingi.
Niliwahi kusikia mtu mwingine akisema kuwa maadili na virtues viko kwenye mila na desturi na mila na desturi maana yake ni makabila. Hii inawezekana ndio maana taifa linapoteza mwelekeo kwa maana halina utamaduni wa kufuata ukichukulia kuwa kiswahili (uswahili) ni utamaduni wa jumla na hauna miko au mafundisho ya moja kwa moja ukilinganisha na 'unyanyusa', 'usukuma, 'ugogo', uzaramo nk.
Hii hoja inaweza ikaonekana ni 'mbaya' kwa sababu mletaji anaonekana kutoa mfano unaoonekana anatokea katika eneo linalodhaniwa kuwa na ukabila lakini tukumbuke kuwa wakati tunazitupilia mbali lugha zetu na tamaduni za asili, UNESCO wako kwenye mpango mkubwa wa kuokoa lugha zinazotoweka - engendered languages and culture
 
Kufa kwa lugha inachangiwa pia na utoro ktk miji na vijiji vyetu, mtu anajiita mngoni kazaliwa kakulia na anazeekea Dsm utakijua kingoni? Angalia ndugu zetu wachagga kwa mwaka wanamsimu wa kurudi kwao na kuendeleza tamaduni zao na ndio maana wengi wanajua lugha yao/zao ikumbukwe si kila kabila ni kubwa kuweza kuwa na redio au gazeti na likapata wateja wa kutosha so makabila madogo yatafutika kwa mpango huo kwa mfano kabila la wasukuma ni wengi kuanzia mwnz, shinyanga mpaka tabora
Angalia wachagga ingawa ni kabila moja lakini limegawanyika na hata lugha hawasikizani sasa utaanzisha redio kwa kichagga cha wapi? Watanzania tupende kurudi ktk miji yetu walao mara moja kwa mwaka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom