Alexism
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 3,423
- 2,045
Katika mambo ambayo mpaka leo sijapata jibu ni kuhusu Lugha inavyoweza changia ukabila na mpasuko katika nchi hii ya Tanzania.
Nchi hii ina makabila takribani 120 na yote yana Lugha zao lakini mara nyingi hazitumiki katika sehemu rasmi kama redioni,magazetini,shuleni na maofisini na kutotambuli kama ni lugha halali huku wengi wakiwa na hisia na imani waliyo mezeshwa kuwa zinaleta matatizo mpaka kuligawa taifa.Nakumbuka mbunge mmoja kama sikosei kutoka CDM alichangia bungeni mwaka huu 2011 kuhusu kuruhusu watu watumie lugha zao katika matangazo ya maredioni na magazeti ili lugha hizi zisife na ilikuwa ni wizara ya utamaduni na michezo kama sikosei.Wengi wa wachangiaji walimponda na kumbeza kuwa mwl.nyerere alikataza,siyo uzalendo eti taifa litagawinga mfano Mama Rwakatare aliponda sana.
Tunaweza kujikumbusha wakati magazeti yanatumia lugha hizo kama kule BK lilikuwepo Rumuli,Bukya na Agandi,je ulikuwepo mpasuko? Kuna ata Biblia imeandikwa kwa kihaya ukienda kwenye magazeti na redio zipo zinatangaza kwa lugha zao katika nchi kama uganda ndo usiseme,S.Afrika mpaka ata mashuleni zinafundishwa hadi chuo.
Mtazamo wangu ni kwamba lugha hizi kwa miaka ijayo zitapotea na kubaki as a dead history kabisa na siyo kweli kuwa kuwepo na kutumika lugha hizo kunaleta mpasuko wa nchi.Mada ndefu nashukuru kwa uvumilivu na ninawasilisha.