Kuna ujumbe wa madaktari bingwa wako njiani kwenda kumuona rais Kikwete

Haina haja, nadhani hii sense ya utu mbele alhali wanaotakiwa kujali utu hawajaliwi utu wao haina mantiki. Hawa madaktari bingwa wajue kuwa ni movement ya haki za wafanyakazi makazini, na haitaisha na hawa more to come. Madaktari walio kwenye mgomo tuwaache waamue wanachojua wao kwa maslahi yao, hawa mabingwa kama hawaungani na wenzao ni wasaliti pia maana hata hawa wagomao leo ndo mabingwa wa kesho.
 
serikali imechelewa sana kutatua jambo hili.na siku zinavyoenda ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya.mfano bugando madaktari wameazimi kufanya mgomo wa nguvu zaidi.hata ratiba ya kutoa huduma haijapangwa,KCMC maresident doctors wameingia kwenye mgomo leo hii.maeneo ya arusha huduma zimeanza kusuasua.muhimbili balaa ni lile.wakati wa maamuzi magumu lazima watu wawajibishwe.
Wakuanza nae lazima awe anayejiita mtoto wa mkulima wa ufipani.
 
Wangemalizia tamko lao kuwa kama mgomi hautaisha basi na sie tunagoma....hapo Pinda angelia bungeni.
 
Hasira nilio nayokubwa ni kuzingatia kuwa hospitali ya mkoa wa kilimanjaro, ambayo ni rufaa kutoka hospitali zote za mkoa HAINA THEATER!!! hivi mtu hapo unatoa sababu gani??
ni kweli tatizo ni pesa? sidhani, matatizo ni mengi likiwapo la kufunika udhaifu wa kiutendaji wa viongozi wenye madaraka ya maamuzi.
Mambo yanaharibika, hatuwezi kukemeana wala kujirekebisha wala kurekebishwa, hii ni moja tu ninayoijua, hata huu mgomo, wasema ukweli, wanaotafuta solutions genuinely wanaweza kuhesabika katika mkono mmoja.
 
Wasiache kumweleza mtawala mkuu kuwa dawa tunazoletewa toka India zimechakachuliwa sana na mafisadi wenzake kiasi kuwa badala ya kutibu yanasababisha vifo

Sample zichukuliwe kuangalia ubora.
 
Wakuu huu ni mgomo ambao sijasikia matamko ya Polisi na FFU ina maana wako likizo ? Kwa nini hawajawafuata majumbani mwao na kuwasimamia kuwalazimisha wafanye kazi au wawafungulie mashitaka mahakamani kwamba wamefanya mgomo bila kibali cha polisi ?Shame on Faiza Foxy na CCM yenu .
 
maazimio ya kikao cha mabingwa MNH leo:

1. Madaktari warudishwe kazini bila masharti wala adhabu yoyote ile mara moja
2. Madai ya madaktari yalikuwa sahihi, yapatiwe majibu mara moja
3. PM Pinda alipotoshwa na hakuwa sahihi
4. Ufumbuzi utolewe ndani ya masaa 24

Duh, haya maazimio mazito sana!
Kama ya ukweli basi nmewakubali madaktari
 
haitasaidia kitu..jk hawezi kuamua kitu chochote maana ccm wenzie hawatamuelewa..
 
Back
Top Bottom