Kuna ujinga, ila huu umepitiliza zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ujinga, ila huu umepitiliza zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Apr 2, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  [h=1]Kuna Sikukuu ya wajinga kweli, ila huu umepitiliza.[/h][h=1]Mji wa Singida, Jana katika Sikukuu ya wajinga, ulifurika wazo la Kijinga. Pamoja na kuwa ilikuwa ni siku ya wajinga, ujinga wa Mji huo uliokuwa chini ya msukumo wa kitaifa, uliendelea hadi mchana hadi Jioni ikawa ni sikukuu ya wajinga. Sikukuu ya wajinga iliyosherehekewa Singida, iliwahusisha zaidi viongozi wa Kitaifa, na viongozi wa Mkoa, pamoja na wabunge wa kutoka Chama cha Mapinduzi CCM na madiwani wa Chama cha Mapinduzi, na viongozi wa Chama hicho katika ngazi mbalimbali.[/h][h=1]Yawezekana mara moja kuona kuwa Viongozi wa Kitaifa, viongozi wa Mikoa wa Vyama vya Upinzani katika ngazi mbalimbali hawakushiriki sikukuu hiyo ya wajinga kwa kuwa waligundua ujinga sio kitu kizuri, ndio maana hata kimataifa japo sio sherehe rasmi, inadumu masaa manne tu. Hivyo haina tija katika maendeleo.[/h][h=1] [/h][h=1]Mji ulipambwa na mabango mengi, yakiwa yanasomeka kuwa”miti ni Uhai’. Pamoja na wao kujua kuwa miti ni uhai, lakini misafara ya viongozi wakubwa wa kitaifa waliosafiri toka Dar, kupitia Dodoma hadi Singida walikuja kuonyesha kuwa hawaoni thamani ya Uhai. Wao wanapandikiza kifo katika uhai, yaani ni wauaji wa misitu yetu.[/h][h=1]Serikali yetu kwa makusudi imeamua kufanya siku ya Upandaji miti kitaifa. Siku hiyo bahati mbaya imeangukia siku ya wajinga duniani, na ikaangukia katika Mkoa masikini kuliko mingi nchini, yaani Singida. Suala la upandaji miti ni la kupongezwa kabisa, ni zuri linafaa na linapaswa kuungwa mkono hata na watu wasio na akili maana hata wao wanahitaji vivuli, kuni, matunda, mbao n.k. Hivyo lilikuwa wazo ambalo sio la kupuuzwa kabisa.[/h][h=1]Bahati mbaya serikali yetu inahitaji mwekezaji hata katika kufikiri. walishindwa wote tangu Rais ambaye amewahi kuwa mkaazi wa Singida, Waziri Mkuu, Mawaziri wengine na wakuu wa Idara, wakiwemo usalama wa Taifa, wakiwemo Wabunge wote wa Mkoa wa Singida wa Chama cha Mapinduzi, na viongozi wote wameshindwa kushauriana na kuona kuwa Mkoa wa Singida Mvua hunyesha Novemba hadi Aprili Mwanzoni. Maana yake tunapoandika hapa na nyie mnaosoma, kwa sasa Mkoa wa Singida hakuna mvua, huenda ikanyesha mara moja isinyeshe tena hadi mwezi Novemba. Hivi Miti inayokuja kupandwa kitaifa itamwagiliwa kwa njia zipi? Bahati mbaya zaidi naibu Waziri wa viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu ambaye miti imepandwa katika Jimbo lake ameshindwa kuwaaambia viongozi kuwa tukio hili linafanyika katika muda ambao sio muafaka. Ameshindwa kumwambia Waziri Mkuu miti unayoenda kuendesha zoezi hili kitaifa itakauka kwa kuwa Ilongero (Jimbo la Singida kaskazini) unapoenda kupanda miti sio musimu wa mvua, na ni sehemu kame kati ya sehemu kame zaidi nchini. Hili nalo tunahitaji mwekezaji kujua? [/h][h=1] [/h][h=1]Mkuu wa mkoa huo, Bwana Vincent Perseko Kone, amekiri kabisa katika mazungumzo yake aliyotoa mwezi wa kwanza, mwaka huu akiwa Shelui. Ilikuwa ni musimu wa mvua kati kati, japo mvua za Singida sio za kutosha sana, alisema Zaidi ya asilimia 50 ya miti inayopandwa mkoani Singida hufa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ukame; imefahamika.

  Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alibainisha wakati wa maadhimisho ya siku ya kupanda miti kimkoa yaliyofanyika kijiji cha Nselembwe, Kata ya Shelui wilayani Iramba.

  Kone alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, mkoa umekuwa ukipata mvua kidogo kiasi cha mm500 hadi 800 tu na kwamba hunyesha kwa wa siku 30 tu kati ya mwezi Novemba na Aprili.

  Alisema kuwa uhaba huo wa mvua husababisha ukame mkubwa ambao huchangia miti mingi inayopandwa mwaka hadi mwaka kufa.

  Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Grace Mesaki,Siku hiyo Kone aliorodhesha sababu nyingine zinazochangia miti iliyopandwa kufa kuwa ni kuliwa na mchwa na ulishaji mifugo unaofanywa na wafugaji.

  Kone alisema kuwa kutokana na uhaba mkubwa wa mvua, juhudi za mkoa za upandaji wa miti mara zote zimekuwa hazifikii malengo yaliyowekwa. Alitoa mwito kwa wakazi wa mkoa wa Singida kupanda miti ya asili kwa kuwa inavumilia ukame.

  Jamani ushauri huu alitoa wakati tupo katikati ya msimu wa mvua, haikuwa busara kwa Mkuu huyu wa Mkoa kumshauri Rais na Waziri kuwa huu sio muda mzuri kutekeleza wazo hilo zuri kitaifa? Sasa watapata faida gani. Waziri Mkuu amekuja na msafara mkubwa kuja kupanda miti, ametumia mafuta mengi ya walipa kodi watanzani, kuja kuzindua zoezi la kupanda miti itakayokauka, aibu gani hii? Mimi nitakuwa wa mwisho kukubali mawazo kama hayo yasiyo na tija kwa taifa. Ukiangalia kwa jicho la kizalendo, hata wazee wa kijijini walishangaa, maana hata wao japo hawajaonja vidato basi wanajua kuwa msimu wa kupanda miti kwa Mkoa wa Singida kwa sababu tu ya Ukame huwa wanapanda desemba, januari, na Februari ili mvua ya mwezi wa Machi angalau istawishe miche iliyopandwa na kama itaweza kuhimili hadi Novemba, japo ni vigumu.
  [/h][h=1]Huwezi kukana uwepo wa mchwa katika maeneo kame kama ya Singida, hivyo miche michanga itashambuliwa na mchwa haraka zaidi. Nini sasa hatima ya zoezi hili? Ni kweli viongozi wetu hamkuona hili au hamkuona hasara ya zoezi hili ndo maana mkasafiri kwa foleni ndefu Dar hadi Singida, kupigiwa ving’ora sisi tuwapishe ili muwahi kuzindua zoezi la kitaifa lisilo na tija? Kwa akili hizi tutabaki masikini milele. jicho langu limeona aibu kubwa sana.[/h][h=1]Niwakumbushe tu kwamba pamoja na kuwa huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hivyo, tungeadhimisha siku hii kwa kutathmini tulikotoka, tulipo na tunapokwenda kuhusiana na hali ya misitu kwa akili nyingi sio kufanya mambo ya kitoto kama ilivyofanyika Singida jana.. Kama rafiki wa mazingira namshauri Kila mmoja wetu mwenye akili timamu na asiye na akili timaku kuwa anatakiwa atathmini athari anazopata kutokana na ufyekaji na uharibifu wa misitu na kuamua kwa dhati kuhifadhi misitu, miti iliyopo nje ya misitu na kuongeza jitihada za kupanda kwa wingi miti ya asili na ya kigeni. Nitafuatilia mwaka mzima kuwajulisha hali ya Mradi bubu huu wa kizalendo wa kupanda miti kwenye ukame uliofanywa katika muda usio mufaka na serikali yetu.[/h]
   
 2. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Posho zao walishaweka mfukoni kwahiyo miti kuota au kutoota wao haiwahusu.
   
 3. NAPITA

  NAPITA JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 5,076
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Tatizo magamba yanawasumbua
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  yaani we isango unashauri magama wasuiri posho kwa miezi 8?

  unawajua au huwajui?hata hiyo desemer watakuja tena,si posho ipo?
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kweli siku ya wajinga
   
 6. MANI

  MANI Platinum Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280

  Hii kubwa !
   
 7. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Umaskini wa watanzania una uhusiano wa moja kwa moja na akili za watumishi wa serikali ukijumuisha viongozi wa kisiasa.
  Wakati mwingine ukifuatilia sana maamuzi na vitendo vyao, waweza kudhani kuwa akili zao ni za kuazima!
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hahahaaa...
  Uchambuzi makini kwelikweli halafu umekaa kivichekesho chekesho hv!
  Nadhani mwandish alitaka walengwa{wajingawajinga} wavutiwe na uchesh ndani yake alafu humohumo wakutane na intended message!
  Big up great thinker!
   
 9. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wao hufikiria posho kwanza na mambo ya maendeleo baadaye, kama kuna posho waalike hata kwenda kuchimba kisima katikati ya ziwa watakuja! Kama hakuna posho hata waalike kwenda kuvuna mazao-hawaji!
   
 10. MAPUMA MIYOGA

  MAPUMA MIYOGA JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2016
  Joined: Jan 30, 2013
  Messages: 2,820
  Likes Received: 1,058
  Trophy Points: 280
  Wewe nawe unaandika andika tu huna lolote ujualo kuhusu SGD. Hata huo ukame unaokomalia sio wa kiivyo. Hivi Same pana mvua au uoto mzuri kuliko Singida kwa mfano, au shinyanga ambapo maeneo mengi hata kulima mahindi huwa yanakauka mapema tu hata kabla ya kuanza kuweka maua?? Acheni Umbea na chuki dhidi ya SGD!
  Kwenye miti mimi mwenyewe nina shamba la miti cyprus na Gilveria pale Kinampanda, namwagilia mwaka mmoja tu wakati ikiwa bado michanga na baada ya hapo inakuwa vema tu. Achana na Jiografia ya kisiasa uliosoma miaka ileNjoo Kinampanda uone shamba la miti.
   
 11. MAPUMA MIYOGA

  MAPUMA MIYOGA JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2016
  Joined: Jan 30, 2013
  Messages: 2,820
  Likes Received: 1,058
  Trophy Points: 280
  Kone alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, mkoa umekuwa ukipata mvua kidogo kiasi cha mm500 hadi 800 tu na kwamba hunyesha kwa wa siku 30 tu kati ya mwezi Novemba na Aprili.

  Umbea mwingine, Mimi naishio kinampanda_Iramba. kwa haya unayosema hapa tusingekuwa tunavuna mahindi hadi kufikia hatua ya kusafirisha mikoa ya kanda ya ziwa na Arusha.
   
Loading...