Kuna uhusiano wowote wa kutohoa neno TANZIA kutoka kwenye TANZANIA?

... mlilikataa jina zuri la ardhi yetu - TANGANYIKA mkaleta mabalaa!
 
Wataalam!

Ukiangalia Utofauti wa neno TANZIA na TANZANIA ni mdogo sana!
Je kuna uhusiano wowote wa inchi na neno hilo?
Je, hakuna namna yoyote neno hilo likafutwa kwenye kamusi na kutaftiwa neno mbadala?
Obituary (Tanzia). Haya tupeni elimu zaidi
 
Hivi inawezekana likifutwa tukaishi milele.....!
Tanzania, tanzia, tanzu, tanzi, tanzanisha, tanzisha, nk ni maneno yanayotokana na mzizi mmoja ^tanza^ wenye maana inayokaribiana na mseto, tata, mchanganyiko, muunganiko, mshikamano, nk
 
Wataalam!

Ukiangalia Utofauti wa neno TANZIA na TANZANIA ni mdogo sana!

Je, kuna uhusiano wowote wa inchi na neno hilo?
Je, hakuna namna yoyote neno hilo likafutwa kwenye kamusi na kutaftiwa neno mbadala?


TANZANIA limetokana na

Tan=== Tanganyika
Zan====Zanzibar
I====Iqbal
A===Ahmadiyya.

Iqbal ni jina la mtu aliyebuni jina Tanzania, yeye anaitwa Iqbal Dar.
Ahmadiyya ni dhehebu la dini yake, kwani yeye ni Muisilamu wa dhehebu hilo.

Hivyo Tanzia na Tanzania havina mahusiano yoyote., Tanzia ni neno la kiswahili lililotoholewa kutoka katika neno la kiarabu; Ta'ziah likiwa na maana hiyohiyo katika Kiswahili.
 
Back
Top Bottom