Kuna uhusiano mkubwa kati ya starehe za bei rahisi na kuongezeka kwa umasikini, the reverse is also true

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,052
Hello bosses

Hapa duniani nadhani moja ya kitu kibaya na chenye madhara makubwa ni umasikini, hasa hasa umasikini wa kiuchumi tukiweka pembeni ule wa kiakili. Umasikini ndio uongeza chuki kwenye jamii, husababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na maswaibu kibao.

Kuna vyanzo vingi vya umasikini na watu wanajitahidi kupambana navyo ili wajitoe kwenye hali hio lakini tukiachana na vyanzo vya umasikini kuna vitu vinavyofanya umasikini uwe endelevu na hivyo kuweka raia kwenye hali ile ile miaka mingi kama sio yote. Moja ya vitu hivyo ni hizi STAREHE ZA BEI RAHISI.

Tunakumbuka kabla ya kupigwa marufuku viroba ulikua unakuta mtu ana 1500 lakini kalewa balaa tena asbh, kutokana na quality ya hzo pombe zinafanya watumiaji wawe legevu na kuendeleza uvivu kunapopelekea umasikini kukithiri.

Pia ukienda uswahilini hasa mikoa ya pwani hizi ngoma za kucheza uchi au nusu uchi zimekithiri sana. Sehemu kama marekani na nchi zilizoendelea kuna strip clubs ambazo kama unataka burudan ya namna hio lazima ulipie ama utoe tips kwa wadada wanaotoa hio burudan, hii inafanya watu wawajibike na inaongeza mzunguko wa fedha then matokeo yake ni kupunguza umasikini.

Kiukweli kwenye nchi zilizoendelea kuna kina aina ya burudani lkn zote ni ghali kiasi fln na matokeo yake wananchi wanathamini kazi na ukifika mda wa kuenjoy wanaenjoy kweli. Na hawawezi kuburudika kila siku coz bei za burudan ziko juu hivyo mda wa kazi wanakua nao mwingi.

Nenda kanda ya ziwa unakuta familia masikini ila ina watoto 7 na kuendelea, hio ni kwa sababu kwa wazazi sex ndio burudan rahisi kupata, na matokeo yake ni kupata watoto wengi wasiotarajiwa.

Mimi sio mwana uchumi lkn ningependa kushauri wanaocontrol uchumi wa nchi hii wapandishe gharama za burudan, pia waruhusu hata stripping clubs na ma-casino coz watakuza uchumi na kupata kodi zaidi badala ya kuongeza tozo na kodi kwenye mahitaji muhimu ya maisha kama vle mawasiliano, vyakula na usafiri (diesel & petrol). Hio itasaidia sana kubalance maisha.

Peace

~Kali
 
Uchumi ni mbovu tu hakuna mtu asiyetaka kuburudika na Dom Perignon kwenye yachts!

Mazingira ya kupata hela bongo ni magumu sana yani bila kuwa ntu ya dili za wizi ukiwa ofisini au kutengenza mazingira ya rushwa huwezi kupata hela hata ya kunywa heineken mwisho wa week. Hilo ni moja tu pili kazi yenyewe kuipata ni kipengele zinaishia kwa watoto wa wakubwa tu.

Mifumo tu ya malipo iboreshwe kuzingatia standards za maisha na watu walipwe kwa usawa. Ukiangalia gharama za maisha kwa sasa zinamtaka kila mtu sasa alipwe sio chini ya elfu 80 kwa siku ila mtu wa chini asie na wadhifa mwenye wategemezi lundo analipwa 15,000 kwa siku halafu ofisa anaelipiwa kila kitu na serikali ndio analipwa laki na nusu kwa siku kwanini huyo wa chini asiwaze rushwa na kutengeneza dili ofisini?

Utaona kuwa hakuna equity kabisa. Mfumo wa kulipana kwa masaa huenda ukasaidia pengine.
 
Hii kimitazamo tunasema European reasoning points! Kwa jinsi mifumo ya kihoja ilivyo. Inawezekan pia starehe ikiongezwa thamani baadhi ya matatizo ya kijamii pia yataongezeka mfano, WIZI wa Aina zote
Wizi ku-control ni rahisi ukilinganisha na umasikini. Ukiweka polisi wawajibikaji na adhabu kali zikitolewa hutosikia kesi za wizi mara kwa mara
 
Kuifananisha Bongo na Marekani ni maji na mafuta
Hatuifananishi bali tunajifunza kwa kuchukua mifano kutoka kwa walio mbele yetu. Kwa wanaotafuta maendeleo ya aina yyt ile reference ni muhimu kama sio lazima
 
Bei ya pombe na sigara inaongezeka kila mwaka wa fedha, ulisikia mauzo ya pombe na sigara yakipungua? Nafikiri kikubwa ni kuwawezesha wananchi kujitambua.

Huko ulikotoa mifano wananchi wanajitanbua sana, hata ambae hajaingia darasani ana upeo wa kutosha.
Nini kinafanya mtu ajitambue?
 
Elimu,malezi etc
Elimu ipi? Kwa sababu kwa uelewa wangu sio elimu ya darasani ndo itafanya mtu ajitambue coz kuna mazuzu wengi tu huko mashulenj. Kwenye malezi nakubaliana napo lkn malezi yanategemea mazingira. Mtu aliekulia sehemu za urban(mjini) anakua na percent kubwa za kujitambua zaidi ya alokulia kijijini. Urbanization inachangiwa na nlichokisema hapo juu kwenye mada, ie (uwepo wa starehe za bei ghali, Macasino, stripping clubs, etc...)

Kwenye comment yako ya kwanza umesema "huko nlikotoa mifano watu wanajitambua hata kama hawajaenda shule" hio ni kwa sababu maeneo mengi ni urban.
 
Elimu ipi? Kwa sababu kwa uelewa wangu sio elimu ya darasani ndo itafanya mtu ajitambue coz kuna mazuzu wengi tu huko mashulenj. Kwenye malezi nakubaliana napo lkn malezi yanategemea mazingira. Mtu aliekulia sehemu za urban(mjini) anakua na percent kubwa za kujitambua zaidi ya alokulia kijijini. Urbanization inachangiwa na nlichokisema hapo juu kwenye mada, ie (uwepo wa starehe za bei ghali, Macasino, stripping clubs, etc...)

Kwenye comment yako ya kwanza umesema "huko nlikotoa mifano watu wanajitambua hata kama hawajaenda shule" hio ni kwa sababu maeneo mengi ni urban.
Majibu yote unayo.
 
Back
Top Bottom