Oxpower
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 2,133
- 2,987
imekuaje hadi nikajiuliza hilo swali?
story yenyewe iko hivi.
nina rafiki yangu wa kike,siku za hivi karibuni yapata kama mwezi sasa,mara kwa mara na humtokea baada ya kutoka kusali tu,anajikuta anandika vitu ambavyo hata yeye havijui.anakuja kushtuka tu ameandika.hiyo hali haikutushtua na tuliona kawaida tu
kilichotushtua ni hiki
alianza kuandika kwa kukoroga koroga kama ambavyo watoto wa awali huwa wanafanya wakipewa daftari na peni bila kufundishwa chochote.kisha akaanza kuimprove kidogo kidogo na ikafikia hatua anaandika kitu furan kinachoeleweka ambacho hatujui ni nini na ni lugha gani.
kwa kifupi kapitia hatua zote za mtu ambaye anajifunza kuandika lakini hata yeye binafsi hajui.ila anaandika mtindo kama kikolea au kichina kwa kwenda chini,tumejaribu kugoogle lugha mbali mbali hatukupata hata lugha moja ya mtindo huo
mashaka yakaanza
baada ya hiyo hali tukaanza kupata mashaka kua inawezekana kuna namna kiroho,pengine ni lugha ya kiMungu au ni mapepo.
tukaona tuwashirikishe watu wa Mungu(nazungumzia waokovu).siku ya ijumaa ikabid aende kwenye jumuiya na akawasimulia kila kitu.
baada ya kuonesha hilo daftar analoandika mama wa kwanza tu ambaye ndio mkuu wa jumuiya akashtuka ,akasema hiki si kiarabu lugha ya mashetani au majini.kisha akamwambia chukua namba ya simu badae utanipigia.lakini mpaka saizi hatujampigia maana bado tunamaswali mengi juu ya kauli yake.
swali liko hivi.
Ni kwanini ?hasa wakristo huwa wanahusisha lugha ya kiarabu na mambo ya kishirikina,majini,mapepo nk.
ikitokea sehemu yoyote ambayo inautata frani hivi kukawa na lugha ya kiarabu basi wazo la kwanza ni mapepo.
hiki kitu nmekisikia mara nyingi na nlijua ni kwa watu ambao hawajui.mambo ya Mungu sasa kilichonishangaza hadi myu wa Mungu nae yumo kwenye huo mkumbo.
mwenye ufahamu tafadhali tubadirishane uzoefu.
Angalizo,mimi ni mkristo na naamini katika Mungu,pia naheshimi dini zote duniani.kama.ninavyoheshimu dini yangu.mada kama hizi huwa hazichelewi kuhama lakini mimi sipo hapa kukashifu dini ya mtu yeyote.nipo hapa kupata ufafanuzi.na pia kama kutakua na mtu ambaye anaweza kunisaidia kuhusu tatizo la huyo dada nitamshukuru sana.
kama kuna sehem patahitaji kueleweshana nipo hapa,
natanguliza shukran