Kuna uhusiano gani kati ya wenye nyumba ndogo kuwa na msongamano wa watu?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,270
40,080
Wakuu kuna uhusiano gani, kati ya wenye nyumba ndogo kuwa na msongamano wa watu, na wenye nyumba kubwa kuwa na msongamano mdogo wa watu?

Unakuta nyumba kubwa ipo kwenye ekari moja, lakini wanaoishi humo ndani unaweza kukuta ni baba, mama, na mtoto mmoja; kwa upande mwingine, unakuta nyumba ya vyumba viwili ina watu wengi mpaka wengine wanalala kwenye makochi.

Sasa nataka kujua huu uhusiano unasababishwa na nini?

bbb.PNG

 
Wenye nyumba kubwa wanakuwaga matajiri na wana roho mbaya na wenye nyumba ndogo ni maskini wanakuwa na roho nzuri wanapenda wageni. Matajiri wanakuwaga bize na wengi ni wakaksi sana ukimtembelea anakuuliza unaondoka lini? Ukitoka hapo hurudi tena
Ina maana na hao wenye nyumba ndogo wakifanikiwa kuwa na nyumba kubwa na tabia zao zinaweza kubadilika?
 
Wenye nyumba kubwa wanakuwaga matajiri na wana roho mbaya na wenye nyumba ndogo ni maskini wanakuwa na roho nzuri wanapenda wageni. Matajiri wanakuwaga bize na wengi ni wakaksi sana ukimtembelea anakuuliza unaondoka lini? Ukitoka hapo hurudi tena
Sio kweli bro. Wenye Hela na matajiri KILA MTU NA KILA NDUGU ANATAKA KUWA KARIBU NA WW NA AISHI NA WW. Sasa utaishi na wangapi? Kwa hio tunaangalia tu wachache sana ambao wana Faida kwetu.. mfano ni kama ndugu Wachapa kazi sana nk ndio tunawaruhusu maishani mwetu. Na kama ndugu wa namna hio hayupo sababu ndugu wote wanataka kukunyonya tu damu, basi unafyekelea ndugu wote kisha unabakia na mke wako na watoto wako, kijana wa kazi, na Dada wa kazi tu.
 
Unamaanisha umasikini unasogeza watu karibu?
Umaskini wa mali, umaskini wa fikra, na umaskini wa elimu UNAWEZA ukasababisha mtu anakuwa na kajumba kadogo ka room 2, halafu ANAJAZANA NA WATU WAVIVU humo ambao wanataka kula tu cha bure na wala hawafikirii kufanya maendeleo MAKUBWA. Ni lazima kila mtu ajifunze kupambana na sio kutegemea tu nduguye.
 
Huo ndo UHALISIA,

Hata watoto walokulia mazingira hayo, Ni wabinafsi mno.
Unajua tunaishi katika dunia ambayo ukijifanya ww unajali sana ndugu, watakuvuruga Haswaaa. Kwa hio ni muhimu kuwa na ubinafsi kwa asilimia fulani, sio asilimia zote. Hio ni muhimu ili kuzuia watu kukunyonya damu. Ukijifanya una roho siku izi ukatoa moyo wako kidogo, kuna watu watataka WAUCHUKUE MOYO WAKO WOTE, AKILI ZAKO ZOTE, NA DAMU YAKO YOTE. Hivyo pia ni uhalisia tu wa dunia ya leo na watu wengi walivyo leo. Ni Wabinafsi....
 
watu wenye hela kidogo hawapendi kabisa zile kadhia na kero za ndugu na jamaa, hupenda kuishi hivyo, nenda mjini ukakae hata kwa ndugu toka nitoke, mke wake anavyokuangalia tuu utajua huyu hapendi niwe hapa..
.
.
na hii tabia ni ya kurithishana, we chunguza hata vitoto vya familia za kawaida akipewa hata Biskut wataombana hapo wee mpaka itaishia kuvunjiana, lakini we mtoto wa familia za juu kidogo walivyo kwanza hawajazoea kuombwa ombwa vitu, ukisogea hapo utashangaa dogo anavitupa vyote chini.. halafu anakuangalia vibaya sana!!
.
.
lakini kukaa nyumba ndogo na watu wengi si vizuri pia, hasa kwa watoto wa kileo, punguza shobo kwa ndugu, penda panapowezekana, kama ni shule sawa changia asome hukohuko kijijini, kwa kusaidia ada, watembelee mara kwa mara, heshima itakuwepo na utajiepusha na vingi!!
.
.
Juzi tuu hapa tumezika dogo ameletwa kukaa kwa ndugu yake, zile himiza himiza za dogo kusoma, ameona isiwe kesi ugali wa nini, akajitundika na kujinyonga mpaka kufa, jitahidi sana kubalance shobo!!
 
Lakn pia wenye kipato kidogo hujikuta wanautegemezi wa maisha yote na muendeleo wa kiazn fulan

Pia wanaofanikiw huw hawaendekez kusaidia sana ndugu hiyo hutokn na historia zao za kimaisha.
 
Kwakifupi kabisa, sisi wenye tunamiliki vibada ndio tunishi maisha yetu ya ukweli na tuna upendo wa dhati kwa ndugu jamaa na marafiki.
Na wale wenye mijengo/mahekalu wao huishi maisha ya kuiga na uzungu mwingi unaowafanya kuishi kama watumwa. Pia ubinafsi umewatawala hadi kwneye hesabu ya chumvi itakayo ongezeka kwenye mlo wako nyumbani kwao...🤓
 
Back
Top Bottom