Kuna uhusiano gani kati ya wauza alkasusu na itikadi kali ya kidini?

Sijawahi kuona mtu ambaye anauza alkasusu akiwa amevaa suti, au jezi, au mavazi mengine yoyote.

Wote huvaa ki Aswar Sunnah, suruali fupi na kanzu. Wanavaa sare.

Je, kuna uhusiano gani kati ya wauza alkasusu na itikadi kali za dini?

Je, hawa wauza alkasusu wanafanya biashara au kuna majukumu mengine ya kisiri wanayatekeleza?

Hebu tutafakari

Kuna mahusiano,asili ya wauzaji wa hiyo kitu ni Waislamu. Lakini kuvaa hivyo haina maana hao ni Magaidi,hapo ndiyo umeingiza chuki za kidini.

Gonga Alkasusi upate afya wewe,acha rongo rongo zako hapa.
 
We jamaa unaanzisha uzi mwingine juu ya uzi mwingine, acha udini mtu kauliza vizuri tu ww unaleta battle za uislam na ukristo
Na mimi huwa najiuliza kuna uhusiano gani kati ya wamiliki mabasi ya kwenda mikoani na udini. Maana 80% ya mabasi ya mikoani hupenda kuweka nyimbo za kwaya kwenye mabasi yao bila kujali kwamba mabasi hayo wanapanda watu wa dini tofauti. Hapo sijawataja waubiri wao wanaopandaga njiani kuhubiria watu ndan ya mabasi huku wakijua kwamba ndan ya mabasi hayo kuna abiria wa dini tofauti tofauti. Mleta mada una idea yoyote kuhusu hili swali ninalojiulizaga kila siku?
 
tatizo wengi wenu mnafikra finyu sana na hamuoni umuhimu wa kufanya hata kautafiti kidogo kabla kuandika humu

hii biashara ya al kasusu sio ngeni hii hapa tz ilikuepo miaka mingi nyuma iliopita na wauzaji wa hii kitu walikuwa washihiri toka yemen

sasa mavazi ya waarabu kwa jumla ni hayo yaani hao wanzilishi wa biashara hiyo hayo ndio yalikua mavazi yao

sasa hawa wanaoibuka sasa hivi wanawaiga wale waanzilishi tu

hakuna agenda yoyote ya siri hapo kama mleta mada alivyotilia shaka wala sio swala la dini hili

haya endeleeni kuna kimwari kinanihitaji muda huu
 
Ni kama wakamua juice ya miwa,, wengi ni kutoka zenji

Ni kama wauza nyama idodomya

Ni kama wauza kahawa, idodomya

Ni kama wakata majani ya ngombe hapa mjini wasukuma

Ni kama waendesha mkokoteni hapa mjini, sambaa


Ni kama wenye pesa hapa mjini chagga

Ni kama omba omba hapa mjini gogo

Ni kama wafuga kuku hapa mjini, kurya

Ni kama wamachinga hapa mjini, chinga

Ni kama wachoma/ wakaanga mdudu hapa mjini

Ni kama wakwea minazi hapa mjini, zaramo

Mwisho: Hakuna mzaramo ambae ni MBUNGE hapa mjini
Seleman jaffo
 
Mimi nahisi wateja wengi wa hio alkasusi pia ni waislam, hivyo sio mbaya wakipiga vivazi vitakavyo wavutia wateja wao ambao ni ndugu zao katika imani.
Ajabu ni kumuona mvaa kanzu anauza rozali na biblia.
Alkasusi mujarab kwa hisani ya watu wa Marekani.
 
Mimi nahisi wateja wengi wa hio alkasusi pia ni waislam, hivyo sio mbaya wakipiga vivazi vitakavyo wavutia wateja wao ambao ni ndugu zao katika imani.
Ajabu ni kumuona mvaa kanzu anauza rozali na biblia.
Alkasusi mujarab kwa hisani ya watu wa Marekani.
Endelea kuhisi hivyo hivyo ni jambo la heri! Halafu vikanzu na visuruali vifupi sio uislam! A town huku kuna machimbo ya Alkasus wanauza na kunywa watu wa mavazi tofauti! Kuna watu ni wa kongwe humu tunawaheshimu ila udini unawatoa ufaham, mleta uzi anasema eti wauza alkasus sio wavaa suti!!! JF inazidi kupoteza thamani
 
Ni kweli inatafakafisha. Hivi karibuni nimekuta wamachinga wanauza mazaga zaga yako branded kama Alshabaab. Nikajiuliza kwa nini mamlaka husika zinaruhusu brand kama hiyo hata kama haihusiani na kikundi cha kigaidi? Vipi mtalii anayeijua alshabaab akikutana na hiyo brand, ataamini ni brand tu au ataamini propaganda za kuwa Tanzania ndo supplier wa vijana wanajiunga huko? Nafikiri tunapaswa kuwa macho zaidi.

Mkuu kuwa serious, sasa kuna kosa gani kutumika kwa jina la Alshabaab?
 
Bujibuji mkuu hilo linatokana na mazingira ya binaadamu tulivo. Hivi umewahi jiuliza kwanini viongozi wa serekali hupenda kuvaa vi Kaunda suit? yani mtu akipata teuzi leo tu siku ya pili kashavishona kibao. au wale vimbelele wengi serekalini utawakuta ndio kivazi chao wakiamini labda vinawaweka kwenye personality ya kiuongozi. binaadamu tuna tabia ya kuiga vitu ambavyo hua havina kanuni kiasili mpaka kufikia hatua ikaeleweka kama ni jambo la lazima au ndivo uhalisia unavyotakiwa.

Wauza kahawa wengi wa vibarazani hua wanavaa kanzu kwa sababu kiasili biashara ya kahawa hapa Dar na Zanzibar ilikua ni biashara inayofanywa na waarabu, sasa waarabu kanzu na vilemba ndio mavazi yao, sasa watu weusi walivyooanza kuiga au kufanya hii biashara pia walikua wanaigiza mpaka mavazi ya waarabu na ndio yakaendelea mpaka kufikia kuselemea kuonekanwa kama ndio vazi rasmi la hiyo biashara.

Na sual la hiyo Alkasus ina muingiliano moja kwa moja na suala la kahawa kwa upande mmoja na upande wa pili umewahi kusikia maneno dawa za kisunna? hizi maana yake ni dawa asili ila wafanyaji biashara hizi wamekua wakitumia lugha hizo ili kuwavuta watu kiimani Zaidi, mana muislamu ukimzungumzia dawa ya kisunna unamfanya anajengeka kuamini Zaidi kutokana nguvu ya kiimani ilivo. So suala la Al-kasusa nalo linapita mule mule ni kujribu kuonesha kua kile kinywaji kama kina baraka za kidini ili waumini wavutike.

Kwahiyo hiyo kanzu na kilembo ni katika either ni mbinu za kutengeneza mazingira ya kuvutia biashara yake au wigo tu kwakua yeye kanza kufanya ile biashara na role models wake walikua wakifanya kazi kwenye mazingira ya mavazi hayo tu na si kengine.
 
Ni
Ni kama wakamua juice ya miwa,, wengi ni kutoka zenji

Ni kama wauza nyama idodomya

Ni kama wauza kahawa, idodomya

Ni kama wakata majani ya ngombe hapa mjini wasukuma

Ni kama waendesha mkokoteni hapa mjini, sambaa


Ni kama wenye pesa hapa mjini chagga

Ni kama omba omba hapa mjini gogo

Ni kama wafuga kuku hapa mjini, kurya

Ni kama wamachinga hapa mjini, chinga

Ni kama wachoma/ wakaanga mdudu hapa mjini

Ni kama wakwea minazi hapa mjini, zaramo

Mwisho: Hakuna mzaramo ambae ni MBUNGE hapa mjini
Ni kama wauza papunye hapa mjini ni wahaya
 
Weka facts zako Mkuu, maneno matupu hayavunji mfupa
Fact ni kwamba ,,
-- kutofautisha baina ya wauzaji kahawa wa kawaida na wale wanaouza alkasusu.

Hiyo ndy sababu ya kuvaa kimuonekano tofauti na wengine..
 
Back
Top Bottom