Kuna uhusiano gani kati ya wanawake waliofanikiwa kielimu na talaka........….? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna uhusiano gani kati ya wanawake waliofanikiwa kielimu na talaka........….?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 19, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wengine kutwa kwenye TV na wala hawawajibiki na majukumu ya nyumbani

  Inaelezwa kwamba kuna uhusiano kati ya wanawake waliofanikiwa kwenye ajira kwa kuwa na kipato kikubwa zaidi ya waume zao na talaka. Labda nisema tu kwamba, binafsi sikubaliani na jambo hilo. Sikubaliana na dhana hiyo kwa sababu kuna idadi kubwa tu tena ya kutosha ya wanawake waliofanikiwa kwenye ajira zao kwa kuwa na kipato kikubwa zaidi ya waume zao lakini ndoa zao zimeendelea kuwa na Amani, imara na furaha tele.

  Kama zipo ndoa ambazo zimetikiswa kwa sababu ya mke kumzidi mume kwa kipato, nafikiri sababu haitakuwa ni mume kuzidiwa kwa kipato, bali kuna jambo lingine ambalo wengi tunashindwa kuling’amua , inawezekana kwa makusudi au kwa kutojua. Kuna swala la kutojiamini ambalo ni tatizo linalowakabili wanandoa wengi. Kama ikitokea mume au mke ana tatizo la kutojiamini katika ndoa, basi ni vigumu kwa ndoa hiyo kuwa na amani.

  Hebu chukulia kwamba, mwanamke ndiye anayefanya kazi na mwanaume hana shughuli ya kumuingizia kipato. Mwanamke huyu anaporejea jioni kutoka kazini anakuta nyumba ni kama jalala. Vitu vimetupwa huku na kule, mwanaume pengine kalala kwenye makochi, huku TV inakoroma. Lakini, kando kuna chupa mbili tatu za pombe. Hebu niambie, hapo mwanamke afanye kitu gani? Ni lazima atazungumzia kukerwa na hali ile.

  Kwa kutojiamini kwake, mwanaume ataanza kusema, mwanamke anamnyanyasa kwa sababu ya kazi yake au cheo chake.
  Hivi hapo kuna uhusiano gani kati ya ajira au cheo na kauli au madai hayo ya mwanaume kwamba, anaonewa. Hapa kuna mtu kushindwa kukua. Mwanaume hapa anashindwa kukua na kuwajibika kwa maisha yake. Kama mwanaume hana shughuli na bado anashindwa hata kupanga vitu nyumbani na bado anaamini kwamba kunywa pombe ndiyo suluhu kwa matatizo yake ya kukosa ajira, inahusiana vipi na mke kumnyanyasa mume?

  Kama mume hana shughuli ya kumuingizia kipato au anayo lakini ina kipato kidogo ukilinganisha na kipato cha mwanamke, lakini mume huyo anajitahidi kupata shughuli itakayolipa zaidi, ni vigumu mwanamke kumzonga. Kama ikitokea mwanamke kumzonga, hapo ndipo naweza kusema, mwanamke ana matatizo. Kwa hiyo tatizo hapa ni kukua, yaani mwanamke au mwanaume anaposhindwa kukua, ndipo matatizo kama hayo ya kuoneshana ubabe na ujuaji kati yao yanapojitokeza. Kwa hiyo siyo suala la mwanamke kuwa nacho zaidi ya mwanaume.

  Lakini pia labda niseme tu kwamba, kuna suala la malezi, kwa nini kuna baadhi ya wanawake wanapopata fedha wanaamini kwamba hawana sababu ya kuwajali waume zao? Hapa kuna suala la malezi. Je mwanamke huyo aliaminishwa nini juu ya fedha? Kwa hiyo siyo kila mwanamke aliyesoma sana au ambaye ana kipato kuliko mume, anakuwa mkorofi, hapana. Kuna wakati ni kweli na kuna wakati siyo kweli. Na mara nyingi wanawake wenye tabia hizo ni wachache sana na ni wale walioathiriwa na malezi.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Nilifikiri utakuja na thread ya wanaume kum please yule dada lol

  naamini wapo wanaume wanatamani ingekuwa marufuku wasichana
  kupata elimu.....

  truth be told kuna challenges za ku deal na 'mwanamke mwenye elimu ya kutosha'...
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  The Boss mbona nishamjibu, sema tu heading inaweza kumchanganya, hebu soma between line hapa chini:

   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  nimeona aisee lol
   
 5. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  As u said Mtambuzi tatizo kubwa ni kwa wanaume wenyewe kutojiamini..mwanamke ukimzidi mwanaume asiyejiamini kipato ukichelewa kurudi kwa sababu ya msingi then mumeo akawahi utaambiwa unafanya makusudi kwa sababu ya pesa zako, ukisafiri kikazi utaambiwa unaenda kwa hawara, ukimkosoa mume kwa upole na nia njema anapokosea utaambiwa unamtawala kwa sababu umemzidi kipato..narudia kutojiamini ndio tatizo na sio elimu,kazi wala kipato cha mwanamke! Bai ze wei mwanaume mpaka unazidiwa kipato na mkeo wewe unakua umelala usingizi au?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi umenena vema uvivu wetu husababisha kutokujiamini.
   
 7. N

  Neylu JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kitu kingine kinachowatesa wanaume ni ile dhana waliojiwekea kuwa wao wanapaswa kuwa juu ya mwanamke kwa kila kitu.. Sasa mwanamke anapokuwa na Elimu na Kipato kizuri kwa kweli wanateseka sana ki mawazo hivyo kuwapelekea kutokuwa na amani na ndoa zao.! Na tuseme ukweli mwanamke aliyesoma na kufanikiwa kuwa na kipato kizuri anakuwa hayumbishwi yumbishwi na mwanaume.. Hilo linawachoma sana wanaume maana wengi wao wanapenda sana kunyanyasa wakiona hawana hiyo nafasi ya kumnyanyasa mwanamke msomi wanaanza visa mwishowe ni TALAKA..! Wanaume mjiamini bana..!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna wengine wakiona wamezidiwa kipato na wanawake, basi wanawaendea kwa waganga ili kuhakikisha wanadumisha mfumo dume....................
   
 9. N

  Neylu JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahahaaa... Kuuumbe eeeh?? Nilikuwa sijaipata hiyo..!
   
 10. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "Bora nirudi zangu kijijini, nikaendelee kukata mkaa............" Best Nasso
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Chezea wanaume weye.................
  Muulize Bishanga taelezea iko namna gani...!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  yaani kwakweli wanaume wengine.......
   
 13. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  LOL...:flypig:
   
 14. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Aaa ze Boss ye andike tu bwana uhuru wa ntu wa kufikiri hauingiliwi.by thw way it was a fair comment.
   
 15. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  title na picha haziendani. huyo kaka anaonekana ni kula kulala hata usafi nyumbani hafanyi. Hakuna mwanamke msomi atayeweza vumilia hii,thas human nature. fikiria unarudi kwako umechoka halafu unakuta nyumba chafu, chakula hakipo mezani nk, utaishi na huyo mtu ili iweje?? mwanaume kama huyo ni booty call wa kutimiza haja za mwili halafu anaondoka kulikoni kuishi kwako kwa kero. saa zingine tunawaonea tu wadada
   
 16. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi nilikuwa tafakari nini nichangie maana heading inazungumzia "Kuna uhusiano gani kati ya wanawake waliofanikiwa kielimu na talaka" na content za mada yako zinazungumzia "uhusiano kati ya wanawake waliofanikiwa kwenye ajira kwa kuwa na kipato kikubwa zaidi ya waume zao na talaka"!

  Sasa mi ngoja nichangie kwenye heading ya hii thread "uhusiano kati ya wanawake waliofanikiwa kielimu na talaka"...

  Mi nina mtazamo tofauti kidogo kuhusu hilo. Mafanikio ya elimu kwa akina dada yanawapa exposure ya kutosha juu ya maisha na mahusiano. Elimu pia huchangia mtu kujua haki zake na kugundua manyanyaso kwa urahisi zaidi kuliko dada asiye na elimu.
  Chukulia mfano huu, wengi wa mahouse gel majumbani hunyanyaswa na mabosi wao kwa kufanyishwa kazi sana, kulipwa mishahara midogo, kukosa likizo, kufanya kazi siku zote 7 za wiki bila hata off nk. Lakini kutokana na kukosa elimu, wengi wao huwa hawagundui kuwa wananyanyasika. The same applied kwa mwanadada yeyote asiye na elimu.

  Sasa elimu hiyo ambayo huungeza upeo kwa mwanamke wa kuelewa na kuchanganua mambo ndiyo baadaye huja kumfanya aweze kubaini wapi ananyanyasika. Jitihada zake za kujikwamua na manyanyaso hugongana na kupingana na mfumo dume uliojijenga siku nyingi wa kumnyanyasa mwanamke na hatma yake hujikuta akiaambulia TALAKA badala ya haki yake anayoipigania! :redface:

  Kuhusu kufanikiwa kwa kipato kwa mwanamke na talaka, hilo hutegemea kwa kiasi kikubwa na uelewa wa hao wanandoa wenyewe. Kama wote ni waelewa na walipendana kwa dhati bila ya kujali tofauti zao za kiuchumi au elimu, ndoa itadumu, lakini kama kulikuwa na shinikizo tofauti na bahati mbaya mmoja wapo au wote wakashindwa kuwa waelewa, mafanikio ya kiuchumi ya mke yanaweza kuaccelerate TALAKA yake pia!
   
 17. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  HAWA WANAWAKE NDIO WALE WANASEMA NATAKA KAMBEGU CHAKO TU TUSIJUANE TENA ANAONA KERO YA NDOA HELA ANAYO MWANAUME AMSUMBULIE NINI?WANAUME NI WADHAIFU SANA MBELE YA MWANAMKE MWENYE PESA YAKE,MIMI BABA YANGU ALISHAJARIBU KUMWACHISHA MAMA YANGU KAZI MPAK SERIKALI IKAINGILIA KATI ETI AKAE NYUMBANI AMPIKIE CHAKULA CHA ASILI SIO KILA SIKU MAROST hahahaha
  mtambuzi nafsi na roho yangu haivumilii mtu mjinga kamwe unakuta mtu anawatoto na familia analishwa na mkewe anakaa hata wiki 2 ndani anaangalia tu mieleka,movies,tv anakeshea nakushindia DSTV huyu ni nini jamani?alafu haridhiki kabisa oh hafai
   
 18. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu mimi ni kwamba, kwenye mahusiano ya ndoa hakuna kitu kinaitwa "equality" ni lazima mtu mmoja awe chini na mwingine awe juu, hata kama hali hii inatokea kwa kupokezana. Hata hivyo kwa asili (kidini pia) mwanamke ndiye anatakiwa kumtii mumewe ikiwa na maana rahisi ya kuwa chini ya mumewe huku wanaume wakitakiwa kuwaheshimu wake zao kwa maana ya kutowafanyia vitu vya hovyo.

  Sasa mahusiano ya elimu na talaka yako hivi, katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la makundi mbalimbali yanayodai haki za wanawake na usawa wao na wanaume ambapo hali hii imesababisha wale wanawake wenye elimu kwa namna moja au nyingine kukutana na movements hizi kwenye baadhi ya maeneo. Pia elimu imewafanya wanawake wawe independent na kama unavyojua when a person becomes independednt financially basi huweza kuhisi anaweza kuwa independent kwenye mambo mengine pia. Hali hii hufanya wasitake kuwa chini ya wanaume kwenye mahusiano na tafiti zinaonyesha kwamba wao ndio huanza kudai talaka.

  Elimu inafanya mtu ajitambue zaidi, aende mbali na Mungu zaidi na kuhisi ana nguvu zaidi so hii ndiyo iliwapa nguvu kubwa wanaume hapo kabla na ndio inawapa wanawake nguvu kubwa sasa. Labda kwa sisi waafrica bado tu kuna lile tatizo la mwanaume kutoa mahali na ile hofu ya wazazi hasa wa mwanamke kuhofia binti yao kuachwa ndio linafanya bado mwanaume kupewa ka nguvu zaidi kidogo lakini la sivyo na africa pia tungekuwa tunashuhudia talaka nyingi kama ilivyo kwa Ulaya na Marekani.
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu sijakielewa nadhani,au naogopa tu tafsiri yake.Lakini naomba Mungu wanawake wasiwe kama wanavyodai humu.Kama kweli watakua wanamaanisha wasemayo humu,basi watakua ni janga la kitaifa!
   
 20. BUCHANAGANDE

  BUCHANAGANDE JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,398
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mwanamke aliyesoma ni hatari tena mwenye kipato kikubwa ndo hatari sana maana atataka afanyiwe lile alitakalo yeye. Mfano ninao, hapa kwa jirani yangu kuna mwanaume ambaye ni Professor na mwanamke ambaye ni Dr by PhD. Mwanaume akienda Ujerumani mwanamke anaenda USA. Mwanamke analotaka atendewe ndo hilo hilo tena anamwambia mwanaume 'USINIBABAISHE KAMA ELIMU SOTE TUNAYO'. Sijui kwa kweli but kwa mtazamo wangu,siafiki mdada asome mpaka Masters kabla hajaolewa maana ni hatari sana kwake kuolewa. Kama unakataa, jaribu kufanya kautafiti kidogo kwa mabinti waliomaliza Degree ya kwanza, wengi wanachezewa na kuachwa tu siku zinasonga.
   
Loading...