Kuna uhusiano gani kati ya urembo na vichupi?

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Imesemwa sana, lakini sio vibaya tukaiangalia upya. Ni kuhusu haya mashindano yanayoitwa ya urembo. Hivi haiwezekani washiriki kuwa wanavaa nguo za kawaida tu badala ya hizo wavaazo ambazo kwa maoni yangu ni kama kujidhalilisha?

Kipimo kwamba haya mambo hayaendi sawa sawa, ukifuatilia mtoto ambaye malezi yake ya nyuma ni mazuri yaani alillelewa katika maadili mema na familia aliyotoka utaona kwamba hupata shida sana mwanzoni kuvaa mavazi haya. Kama jamii hatuwezi kushauri namna bora zaidi ya mavazi yetu katika mashindano haya?

Nawasilisha kwa michango ushauri na mapendekezo.
 
Lengo la kichupi ni kumwezesha binti aonekane vizuri kabisa maungo yake kama alivyoumbwa na Mungu ili majaji wapata fursa nzuri ya kumpa alama. Akivaa vazi refu (zamani ziliitwa "maksi") itakuwa vigumu majaji kumwona alivyoumbika na hivyo wanaweza kudanganyika katika kutoa alama. Yawezekana mshiriki ana nundu huko ndani au ana alama ambayo kulingana na vipimo vya uzuri ikamwongezea alama au ikampunguzia. ndo maana ili kuepuka kudanganyika wanaamua avae hicho kichupi ili aonekane kikweliii!

Ndiyo, kwa upande mwingine kuna suala la maadili kwetu sisi waafrika, japo hili nalo kwa kuangalia hali halisi linaweza kujadiliwa kwani si wote wanaona ubaya katika "mila" hiyo mpya. Kwa wengine ni sawa tu: kwani kila kitokacho ulaya na marekani ni bora kuliko chetu (kwa mawazo ya wengi). Ndiyo maana kwa sasa ni vigumu sana kuongea kiujumla juu ya Utamaduni wa mwafrika.
 
Back
Top Bottom