Kuna uhusiano gani kati ya nyimbo na uchungu wa nafsi?

Wimbo wa Bob Marley "Chances Are" huwa unanitoa machozi.

Yani hapa nimeanza kuusikiliza tu naona machozi yanaanza kunitoka. Imebidi niukatishe kabisa yani nimeshindwa kumaliza kusikiliza wote. Ni wimbo maalum ninaosikiliza kwenye misiba ya watu ninaowapenda.Bob Marley analalamika sana kuhusu huzuni katika maisha.

Ni mambo ya hisia zaidi. Dr Robert Sapolsky ameelezea kirefu sana katika kitabu chake "Behave: The Biology of Humans at Our Best and Worst"

Kuna bidada mmoja rafiki yangu alifanya Ph.D yake ya Clinical Psychology kwenye swali hili. Nitamuuliza kupata maoni ya kisomi.


Kwa hamu na shauku kubwa, tunasubiri majibu kutoka kwa rafiki yako ili nasi tujue uhusiano wa kulia na music.
 
Mimi huwa inanitokea Sana ..sijui kwanini na mbaya zaidi mpaka kwenye nyimbo za tamthilia za wakorea na wafilipino nyimbo zao huniliza ingawa sijuagi wanaimba vitu gani😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom