Kuna uhusiano gani kati ya harufu mbaya na kutema mate?

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,730
2,388
Hili linatokea na hata mimi huwa nalifanya, ila nimejiuliza na nashindwa kuelewa kwanini huwa tunatema mate baada ya kusikia harufu mbaya.

Anayejua anijuze tafadhali...!!!
 
Hili linatokea na hata mimi huwa nalifanya, ila nimejiuliza na nashindwa kuelewa kwanini huwa tunatema mate baada ya kusikia harufu mbaya. Anayejua anijuze tafadhali...!!!
Harufu mbaya ni mixture ya chemical mfano hydroen sulfide kwenye ushuzi inadisolve kwenye saliva na kutengeneza chemical nyingine. Hi yo mate kuchefuka ni ishara kuwa mate yamechanganyika vibaya
 
Harufu mbaya ni mixture ya chemical mfano hydroen sulfide kwenye ushuzi inadisolve kwenye saliva na kutengeneza chemical nyingine. Hi yo mate kuchefuka ni ishara kuwa mate yamechanganyika vibaya
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Sasa lakn, harufu mbaya kwani huwa inasikika kwa ulimi..?? Si huwa inasikika kwa pua??
 
Fanya hivi, ukisikia harufu mbaya meza mate, uone kama hujaumwa tumbo ndipo utagundua umemeza uchafu
 
Harufu na ladha ni chemical based reception, yaani harufu ni kemikali ambayo huwa dissolved kwenye kuta za pua na hapo ndipo ubongo hung'amua aina ya harufu;

Na ndio maana mtucakiwa na mafua zile kuta za pua zikasiribwa kwa utandu wa kamasi basi zile kemikali hushindwa kuyeyushwa na hivyo mtu hushindwa kunusa harufu. Ulimi nao huonja ladha kwa kuyeyusha kemikali kwenye sakafu ya ulimi, na ndio maananmtu akiwa na mafua pia hushindwa kwa kiasi fulani kuonja ladha ya chakula ipasavyo.

Sasa harufu mbaya ikishanuswa puani moja kwa moja ile kemikali huyeyushwa kwenye mate ya ulimi pia,na ubongo hujua hili, na ndio maana imedevelop reflex za kuziba pua na kutema mate ili kuzuia kemikali (harufu) mbaya kuingia mwilini na kutokaa mdomoni kwenye mate.
 
Back
Top Bottom