Kuna uhusiano gani kati ya Chato na Mwalimu Nyerere?

Aug 18, 2019
80
177
Na Mwananzengo wa Chato.

Tarehe 09 Januari, 1967 Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya ziara Chato katika Mkoa wa West Lake. Wakati huo Chato ilikuwa katika Wilaya ya Biharamulo.

Mwl. Nyerere alikwenda Chato kuzindua kinu cha kuchambua pamba (Chato Ginery) kilichojengwa kwa ubia wa chama cha ushirika cha Igokelo na mwekezaji kutoka Mwanza Bw. CK Patel kwa gharama ya shilingi milioni 2.

Katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Chato, Hayati Mwl. Nyerere alipongeza juhudi za wananchi wa Chato kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuwahimiza kuzalisha pamba zaidi kwa kuwa kiwanda hicho kilikuwa na uwezo wa kusindika marobota 20,000 ya pamba kwa mwaka wakati uzalishaji wa wananchi wa eneo hilo ulikuwa mdogo wa marobota 7,500 tu

Akiwa katika mkutano huo Mwl. Nyerere alianzisha mchango ambapo yeye mwenyewe alitoa paundi 1,000 sawa na shilingi 20,000 (kwa thamani ya shilingi ya wakati huo) kwa ajili ya kujenga upya bandari ya Nyamilembe ili kuanza kusafirisha marobota ya pamba kutoka Chato kwenda Mwanza na kwingineko.

Bandari ya Nyamilembe mpaka leo ipo, ikiwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Mwl. Nyerere alitoa fedha hizo akichangia asilimia 10 ya fedha zote paundi 10,000 zilizotakiwa kujenga bandari hiyo na kuwahimiza wananchi kuendelea kuchangia ujenzi huo kwa kuwa maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe.

La kujifunza hapa ni kuwa juhudi za kuijenga Chato ambayo ilikuwa kijiji kidogo wakati wa Uhuru zilianza tangu enzi za Mwalimu. Pamoja na kwamba kiwanda hicho kwa sasa kimedorola lakini bado kipo na ni moja ya chanzo cha ajira na kuongeza thamani ya pamba ya wakulima.

Hii ni kusema kwamba Mwl. Nyerere aliona umuhimu mkubwa wa kuijenga Chato na hivyo akawahimiza wananchi kuijenga Wilaya yao kwa kujitegemea.

Pamoja na kuhimiza dhana ya kujitegemea alipochangia paundi 1,000 na kisha kuwahamsisha watu kuchangia ujenzi wa bandari, alitamani kuiona Chato iliyokua kimaendeleo.

Aidha, baada ya kutoka Chato ilipofika tarehe 05 Februari, 1967 Mwl. Nyerere alikwenda Arusha na akatangaza Azimio la Arusha linalohimiza kujitegemea.

Katika mkutano huu wa tarehe 09 Januari, 1967 pia wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato (ambayo ilikuwa shule ya msingi pekee ya Chato) walikuwepo kumpokea Mwl. Nyerere akiwemo John Pombe Joseph Magufuli wakati huo akiwa mwanafunzi wa darasa la kwanza.

Siku hiyo wananchi walitoa zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya muhogo mkubwa uliokuwa mrefu kuliko urefu wa Mwl. Nyerere, muhogo huu uliotolewa na Mzee Maliganya (ambaye kwa sasa ni Marehemu).

Historia hii inawakumbusha Wananchi wa Chato kwamba Chato ilianza kujengwa na Mwl. Nyerere kwa kujenga Kiwanda cha Pamba na Bandari ya Nyamilembe, kwa hiyo wasishangae kuona juhudi hizo zikiendelezwa hata sasa.

Juhudi hizi za Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere ziliendelezwa na viongozi wengine waliofuata akiwemo Mzee Mwinyi aliyefanya ziara katika Mji wa Chato, baadaye Hayati Benjamin William Mkapa nae aliitangaza Chato kuwa Wilaya na alipokuja Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akaizindua Wilaya ya Chato.

Na sasa aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza mwaka 1967 amekuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2015.

Ndio kusema Kijiji cha Chato kilichotembelewa na Mwl. Nyerere.

Tarehe 09 Januari, 1967 ndio Wilaya hii ya Chato ya leo ambayo ina umeme, ina maji, ina barabara za lami, ina taa za barabarani, ina uwanja wa ndege, ina hospitali, ina bandari ya Nyamilembe, ina Ginery na ina maendeleo makubwa ya makazi ya watu na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa wananchi.

Mafunzo mengine tunayoyapata hapa ni kuwa Mwl. Nyerere alidhamiria hasa kujitegemea kwa kujenga viwanda sio tu mijini bali pia hadi vijijini.

Lakini pia lipo swali la kujiuliza, kama kiwanda cha pamba cha Chato bado kipo mpaka leo, Je viwanda vyetu vingine vimekwenda wapi? Kiko wapi kiwanda cha Zana Za Kilimo (ZZK), kiko wapi kiwanda cha MWATEX, MUTEX, General Tyre na vingine.

Lakini kama tangu enzi za Nyerere kulikuwa na joto kubwa la kuijenga Chato, ni vizuri kuelewa yanayotokea leo Chato hayakuanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tano. Yalianza tangu Awamu ya kwanza.

Historia ni mwalimu mzuri.
 
Tofauti ya sasa na enzi za mwalimu wakati ule alihimiza wananchi wa chato kuchangia maendeleo wenyewe lakini sasa hivi ni nguvu kubwa ya kuchota rasilimali ya taifa kuendeleza sehemu moja wakati deni linabebwa na taifa zima.

Nyerere alijitahidi kufuta ukabila nq kujenga umoja wa taifa lakini kinachotokea sasa kinaonyesha kuwa hakufaulu ukitaka kuona tofauti nenda Musoma halafu uangalie mji wenyewe ulivyo.
 
Hapo kuna mmoja alizindua kiijiji, mwingine akifanya wilaya, matarajio ni kufanywa mkoa, nadhani ingefanywa nchi kabisa,Ili sio KILA awamu tza iwe huko pekee.
Point yako kuu ni kutaka kuhalalisha yatendekayo sasa juu ya matumizi ya Kodi zetu kwamba ni sahihi kuelekezwa sehemu moja.
But kumbuka yanakuja kuwa magofu Kama hicho kiwanda cha pamba.
 
Elimu ya shule ya msingi ulimaliza kweli?
Maana umeandika utopolo tu,ili mradi usifie na kuabudu miungu.
 
Duh.... yote hii ni juhudi ya kuhalalisha Chatonization ya serikali nzima.

Urais siku zote huwa haunaga mipaka ya kisheria mingi.... udhibiti mkubwa wa tabia za Rais unafanywa na Rais mwenyewe, kupima historia za viongozi wenzake waliopita; kupima mrejesho wa wananchi kuhusu mambo anayoyafanya au yanyofanyika na athari za hayo mambo kwenye taasisi ya Urais.

Huyu wa sasa hana kabisa Self Awareness.
 
Mkuu umeelezea vizuri Sana, ila aliyofanya nyerere usiyafananishe na haya Matakwa binafsi yanayovikwa sura ya Maendeleo.
 
Dah nyie watu ni wapumbavu Sana mnatumia nguvu nyingi sana kualalisha uchafu unaofanyika Chato,uzuri ni kwamba wenye akili wote wameshakataa kinachofanyika huko, endeleeni kudanganya wajinga wenzenu.
 
Na Mwananzengo wa Chato.

Tarehe 09 Januari, 1967 Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya ziara Chato katika Mkoa wa West Lake. Wakati huo Chato ilikuwa katika Wilaya ya Biharamulo.

Mwl. Nyerere alikwenda Chato kuzindua kinu cha kuchambua pamba (Chato Ginery) kilichojengwa kwa ubia wa chama cha ushirika cha Igokelo na mwekezaji kutoka Mwanza Bw. CK Patel kwa gharama ya shilingi milioni 2.

Katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Chato, Hayati Mwl. Nyerere alipongeza juhudi za wananchi wa Chato kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuwahimiza kuzalisha pamba zaidi kwa kuwa kiwanda hicho kilikuwa na uwezo wa kusindika marobota 20,000 ya pamba kwa mwaka wakati uzalishaji wa wananchi wa eneo hilo ulikuwa mdogo wa marobota 7,500 tu

Akiwa katika mkutano huo Mwl. Nyerere alianzisha mchango ambapo yeye mwenyewe alitoa paundi 1,000 sawa na shilingi 20,000 (kwa thamani ya shilingi ya wakati huo) kwa ajili ya kujenga upya bandari ya Nyamilembe ili kuanza kusafirisha marobota ya pamba kutoka Chato kwenda Mwanza na kwingineko.

Bandari ya Nyamilembe mpaka leo ipo, ikiwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Mwl. Nyerere alitoa fedha hizo akichangia asilimia 10 ya fedha zote paundi 10,000 zilizotakiwa kujenga bandari hiyo na kuwahimiza wananchi kuendelea kuchangia ujenzi huo kwa kuwa maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe.

La kujifunza hapa ni kuwa juhudi za kuijenga Chato ambayo ilikuwa kijiji kidogo wakati wa Uhuru zilianza tangu enzi za Mwalimu. Pamoja na kwamba kiwanda hicho kwa sasa kimedorola lakini bado kipo na ni moja ya chanzo cha ajira na kuongeza thamani ya pamba ya wakulima.

Hii ni kusema kwamba Mwl. Nyerere aliona umuhimu mkubwa wa kuijenga Chato na hivyo akawahimiza wananchi kuijenga Wilaya yao kwa kujitegemea.

Pamoja na kuhimiza dhana ya kujitegemea alipochangia paundi 1,000 na kisha kuwahamsisha watu kuchangia ujenzi wa bandari, alitamani kuiona Chato iliyokua kimaendeleo.

Aidha, baada ya kutoka Chato ilipofika tarehe 05 Februari, 1967 Mwl. Nyerere alikwenda Arusha na akatangaza Azimio la Arusha linalohimiza kujitegemea.

Katika mkutano huu wa tarehe 09 Januari, 1967 pia wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato (ambayo ilikuwa shule ya msingi pekee ya Chato) walikuwepo kumpokea Mwl. Nyerere akiwemo John Pombe Joseph Magufuli wakati huo akiwa mwanafunzi wa darasa la kwanza.

Siku hiyo wananchi walitoa zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya muhogo mkubwa uliokuwa mrefu kuliko urefu wa Mwl. Nyerere, muhogo huu uliotolewa na Mzee Maliganya (ambaye kwa sasa ni Marehemu).

Historia hii inawakumbusha Wananchi wa Chato kwamba Chato ilianza kujengwa na Mwl. Nyerere kwa kujenga Kiwanda cha Pamba na Bandari ya Nyamilembe, kwa hiyo wasishangae kuona juhudi hizo zikiendelezwa hata sasa.

Juhudi hizi za Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere ziliendelezwa na viongozi wengine waliofuata akiwemo Mzee Mwinyi aliyefanya ziara katika Mji wa Chato, baadaye Hayati Benjamin William Mkapa nae aliitangaza Chato kuwa Wilaya na alipokuja Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akaizindua Wilaya ya Chato.

Na sasa aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza mwaka 1967 amekuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2015.

Ndio kusema Kijiji cha Chato kilichotembelewa na Mwl. Nyerere.

Tarehe 09 Januari, 1967 ndio Wilaya hii ya Chato ya leo ambayo ina umeme, ina maji, ina barabara za lami, ina taa za barabarani, ina uwanja wa ndege, ina hospitali, ina bandari ya Nyamilembe, ina Ginery na ina maendeleo makubwa ya makazi ya watu na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa wananchi.

Mafunzo mengine tunayoyapata hapa ni kuwa Mwl. Nyerere alidhamiria hasa kujitegemea kwa kujenga viwanda sio tu mijini bali pia hadi vijijini.

Lakini pia lipo swali la kujiuliza, kama kiwanda cha pamba cha Chato bado kipo mpaka leo, Je viwanda vyetu vingine vimekwenda wapi? Kiko wapi kiwanda cha Zana Za Kilimo (ZZK), kiko wapi kiwanda cha MWATEX, MUTEX, General Tyre na vingine.

Lakini kama tangu enzi za Nyerere kulikuwa na joto kubwa la kuijenga Chato, ni vizuri kuelewa yanayotokea leo Chato hayakuanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tano. Yalianza tangu Awamu ya kwanza.

Historia ni mwalimu mzuri.
Serikali ya Nyerere ilipeleka miradi mingapi Butiama katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake?
 
Walaaaah nikiwa raisi kulekwetu vudee(upareni)Kijiji Cha msanga njia kuu ya kupanda chomee kutakuwaaa Kama ulayaaa
 
Mtoa hoja unataka kujustify tu kwamba kwa nini kwa sasa ni Chato badala ya Geita!!

Bado hujatushawishi.
 
Nyerere alitembea vijiji vingi sana.

Tarehe 8 mwezi wa tisa mwaka 1971 alitembelea kijiji changu kufungua madaraja mawili.

Kuanzia hapo vijiji vyangu viwili Mpinji na Ivuga havijawahi kutembelewa na rais yoyote.

Kwa hio mwalimu alikuwa very special Na exceptional
 
Hapo kuna mmoja alizindua kiijiji, mwingine akifanya wilaya, matarajio ni kufanywa mkoa, nadhani ingefanywa nchi kabisa,Ili sio KILA awamu tza iwe huko pekee.
Point yako kuu ni kutaka kuhalalisha yatendekayo sasa juu ya matumizi ya Kodi zetu kwamba ni sahihi kuelekezwa sehemu moja.
But kumbuka yanakuja kuwa magofu Kama hicho kiwanda cha pamba.
Hiyo ni wilaya hata akitoka madarakani itaendelea tu
 
Back
Top Bottom