Kuna uhusiano gani kati Meeda bar na wezi wanaotumia dawa za kulevya kulewesha wateja

lodrick

Member
Dec 29, 2010
61
19
Waungwana, kama wewe ni mwenyeji wa maeneo ya sinza, mwenge au maeneo mengine yaliyokaribu na sinza utakuwa unaifaham Meeda bar.

Ni bar maarufu sana maeneo ya sinza mori barabara ya kuelekea mwenge. Kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya wateja kuibiwa mali zao kama magari, pesa, simu, vito vya thamani, laptop na vingine vingi. Ila pia wizi huu mara nyingi unafanyika baada ya mteja kuwekewa dawa za kulevya kwenye kinywaji.

Ni kweli kwamba uongozi wa meeda hauna taarifa na matukio haya? Je kama wanataarifa wamechukua hatua gani? Je ni kweli kwamba hawawajui hawa wanaofanya mchezo huo? Kuna uhusiano gani kati ya meeda na hawa wezi? Matukio ni mengi na yamewakuta wengi.
 
siku hizi watu watafuta pesa kwa mbinu nyingi haitashangaza ukawa ni mchongo wa wenye bar ama mhudumu/wahudumu wachache wamekula inshu na madealer, wao wanaminyia madawa ya kulevya jamaa wanamaliza kazi kisha wanapigiana mgao
 
kuna mshkaji wangu hivi majuzi nae aliwekewa madawa kwenye bia hapo meeda, baada ya dk chache akaanza kujiskia kuishiwa nguvu na pumzi. Lkn kwa sababu alishasikia stori za pale ikabidi atafute driver tax wa pale anaemfaham akamkabidhi funguo za gari yake na kumuomba amuwahishe nyumbani. Jamaa alikuja kuzinduka kesho yake saa kumi jioni akiwa na njaa kali
 
Meeda inataka kufa. Inawatumia majambazi na machangudoa kuiba vitu ili kukuza mtaji, hata watu wengi wanaoenda kunywa Meeda siku hizi ni ma homeless, ile night club wanaitumia kama nyumba yao
 
Thats terible.
Watu mnaenda Bar na ma laki unakunywa bia mbili unaomba bili unachomoa laki maja noti za buku tano tano unalipa bili then unaendelea kunywa. oops
 
Thats terible.
Watu mnaenda Bar na ma laki unakunywa bia mbili unaomba bili unachomoa laki maja noti za buku tano tano unalipa bili then unaendelea kunywa. oops

hiyo bar siku nyingi inajulikana,hapo nikijiwe cha majambazi wa magari hata zombe anapajua,sio hiyo tu mwika bar,nyingine ipo karibu na mgabe primary hatari sana hizo bar
 
Msiipakazie Meeda peke yake. Baa nyingi kubwa kwa sasa zina hao watu. Mchezo huo unaitwa doloree!. Cha muhimu mkinywa muwe waangalifu. Drink responsibly!. Hapo ng'ambo tu ya Meeda-bar za Mlimani City wapo kibao,kakae vibaya Ambiance,bili bar,miller bar na bar zote kubwa za jirani,hesabu maumivu!. Chamuhimu-drink responsibly na don't show off! Kwa sababu ndo tabia za wabongo wengi kwenye mabaa.
 
yule aliyekuwa jambazi maarufu wa magari MINE CHOMBA ndio kilikuwa kijiwe chake
 
Back
Top Bottom