Kuna uhitaji wa exhibition hall kubwa Tanzania na pia indoor stadium na performance theatre

Tz_one

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,613
2,000
1.Uhitaji wa Exhibition hall na Theatre
Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri kwenye swala la muziki yan bongo fleva na movie yan bongo movies ..sekta hii imeajiri vijana wengi na pia ni moja ya sehemu nzuri kwa ajili ya kutengeneza ajira kwa watu ..nchi kama south Africa kwa africa..inazo exhibition hall na theatre,kama vile soweto theatre na nyingenezo ..

Je zitasaidia nini?
Theatre na Exhibition hall ..ni sehemu ambapo matukio mbalimbali ya muziki kama vile show mbali mbali ,tuzo za muziki na movies na pia mikutano na maonesho mbali mbali huweza kufanyika

Kwa Tanzania hasa DAR hatuna theatre, ila kuna exhibition hall kama mlimani city hall na diamond jubilee ..shida yake hizo sehemu ..humilikiwa na watu binafsi na hutoza pesa kubwa ,,na hii huwasumbua wasanii wadogo na pia hata wakubwa

Tunayo theatre pale national museum ila ni ndogo sana ina iwezo wa watu 500 ..na kwa udogo huo pesa haitatosha kurudisha faida kwa watu watayoitumia

Kuna kila sababu ya Baraza la michezo kujenga ukumbi mkubwa wa maonesho na theatre ili kusadia events mbali mbali kufanyika..na pia kupunguza gharama za kukodi mlimani city hall au diamond jubilee...

Kwa kuanza exhibition hall yaweza kuwa na ukubwa wa kuchukua watu 10000 na theatre hata watu 7000

Wizara ya michezo inaweza kukopa na pia hata ikaomba ufadhili iweze kujenga vitu hivi kwan vitasaidia sana kwenye sekta ya sanaa

2..Indoor stadium
Hii ni stadium ambayo michezo mbali mbali ya ndani huweza kufanyika ..kama vile basket ball ,volley ball na net ball ..Tanzania tunayo indoor stadium ila hairidhishi kabisa ..kuna haja ya Tanzania kuanza kuipa vipaumbele michezo mingine kama hyo ..na sio mpira wa miguu tu ..

Kwa mapendekezo yangu Tanzania inahitaji indoor stadium ya capacity ya seats 10000

Uzuri ukiwa na multi purpose indoor stadium .inaweza pia ikatumika kama performace theatre..na exhibition hall..kutegemea na inavyopangwa ..hii hutumika sana marekani USA ..ndo maana viwanja kama The Forum Inglewood CA hutumika kwa ajili ya Basket ball na Pia hata shoo za muziki
 

Tz_one

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,613
2,000
Kunazo propasal nyingi ambazo ..nying zmeundwa na wanafuzi wa architecture tanzania ..na pia kuna nyingine ya serikali inayohusisha ..sports complex ila cjui kama itakamilika ..ilikua inahusisha ujenzi wa Uwanja wa Taifa 60,000seats ,upanuzi wa uwanja wa uhuru 30,000 ..na kujenga indoor stadium 10,000 seats ..na perfomance theatre 5000seats
 

Salamanders

JF-Expert Member
Oct 31, 2016
365
250
4% ya dhahabu + Makinikia hazitoshi kufanya yote hayo, tuna budget deficit ya 37%. Subirini mungu ashushe Rehema zake
 

Raja Casablanca

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
507
250
Kwa Tanzania hasa DAR hatuna theatre, ila kuna exhibition hall kama mlimani city hall na diamond jubilee ..shida yake hizo sehemu ..humilikiwa na watu binafsi na hutoza pesa kubwa ,,na hii huwasumbua wasanii wadogo na pia hata wakubwa
ni kweli mkuu, hebu jiulize ni watu wangapi wanaweza kuona movie kwa sh elfu 10?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom