Kuna uhalali wa kulipa hela ya sungusungu ilhali una mlinzi binafsi?

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Hii bado sijaelewa ningependa kupata au kujua ukweli, ukiwa kwenye biashara mitaani ni lazma ulipe hela ya ulinzi shirikishi hata kama kuna mlinzi kwenye fremu zenu? Hii ni nchi ya aina gani na tunapelekana wapi? Naombeni kujua ukweli.
 
Hivi wewe unaakili? Unafikiri watu wa kazi wa ukweli wakikutembelea huyo mlinzi wako mwenye gobore atawezana nao.?
 
Huo ndiyo utaratibu uliowekwa katika eneo lako. Hivyo huna namna. Lipa ili usionekane tofauti na wengine.

Kama hao sungusungu wanasaidia zoezi la usalama kwenye hilo eneo, huoni bado ni msaada kwako? Isitoshe hiyo hela yenyewe ni kiasi gani mpaka ikuume kiasi hicho?
 
Ukienda kwenye Kijiji ukakuta wanakijiji wote ni chongo na wewe una macho yote, fumba jicho Maja ili ufanane nao. Kwenye Maisha ukitaka uishi vizuri bila mgogoro na jamii epuka u ukawa ukawa. Usipende Sana kujenga hoja na kukosoa kilicho azimiwa, wanaweza kukuazimia. By the way garama hizo ni ndogo Sana
 
Unapaswa kulipa kwani hao Sungusungu wanamlinda pia mlinzi wako wakati analinda mali yako iwe salama.
 
Huu ujinga nilishaukataa mapema sana na ninapokaa wananifahamu mimi ni nani!,Huwa sitakagi mambo ya kipumbavu!.

Hawa ulinzi shirikishi sijui Sungusungu ndiyo wezi namba moja!.

Hii ishu ilinipeleka mpaka mahakamani wakati fulani na nikawashinda sasa wanabakigi "Ipo siku utaibiwa halafu usije kulalamika kwenye serikali ya mtaa" ,Niliwaambia huyo atakayejaribu kuiba kwangu atakuwa mwanaume kunizidi,mimi ninachaoamini mwanaume anayenizidi uanaume wangu ni Mkuu wa Majeshi tu!,Hilo huwa nawaambia hata nikienda kwenye mikutano yao hiyo ya kijinga kusikiliza hoja zao za kijinga jinga.
 
Ukienda kwenye Kijiji ukakuta wanakijiji wote ni chongo na wewe una macho yote, fumba jicho Maja ili ufanane nao. Kwenye Maisha ukitaka uishi vizuri bila mgogoro na jamii epuka u ukawa ukawa. Usipende Sana kujenga hoja na kukosoa kilicho azimiwa, wanaweza kukuazimia. By the way garama hizo ni ndogo Sana
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Usilipe mkuu na nnaamini watatokea wafanyabiasha wenzio watakao kuunga mkono,sungusungu ndio vibaka haohao
 
Hii bado sijaelewa ningependa kupata au kujua ukweli, ukiwa kwenye biashara mitaani ni lazma ulipe hela ya ulinzi shirikishi hata kama kuna mlinzi kwenye fremu zenu? Hii ni nchi ya aina gani na tunapelekana wapi? Naombeni kujua ukweli.

Kakae porini na mlinzi wako, ukiishi na watu kuwa mtu wa ushirikiano, mimi nina wangumwenyewe, ila nalipa na wa mtaani.... Kuna siku wezi watakuwa wanakuja kuiba kwako, walinzi wa nje watawapisha tukuone
 
Huo ndiyo utaratibu uliowekwa katika eneo lako. Hivyo huna namna. Lipa ili usionekane tofauti na wengine.

Kama hao sungusungu wanasaidia zoezi la usalama kwenye hilo eneo, huoni bado ni msaada kwako? Isitoshe hiyo hela yenyewe ni kiasi gani mpaka ikuume kiasi hicho?
Kwa hiyo nilipe tu
 
Huu ujinga nilishaukataa mapema sana na ninapokaa wananifahamu mimi ni nani!,Huwa sitakagi mambo ya kipumbavu!.

Hawa ulinzi shirikishi sijui Sungusungu ndiyo wezi namba moja!.

Hii ishu ilinipeleka mpaka mahakamani wakati fulani na nikawashinda sasa wanabakigi "Ipo siku utaibiwa halafu usije kulalamika kwenye serikali ya mtaa" ,Niliwaambia huyo atakayejaribu kuiba kwangu atakuwa mwanaume kunizidi,mimi ninachaoamini mwanaume anayenizidi uanaume wangu ni Mkuu wa Majeshi tu!,Hilo huwa nawaambia hata nikienda kwenye mikutano yao hiyo ya kijinga kusikiliza hoja zao za kijinga jinga.
Huu ni uongo unataka kumpotosha mtoa mada, makubaliano ya ulinzi hufanywa na mkutano mkuu wa mtaa/kijiji.
Wananchi huamua kuweka ulinzi na kiasi cha kulipa,hizo ndio huwa sheria ndogondogo zinazotungwa na kupata baraka kwenye baraza la madiwani kwenye halmashauri husika.
Siyo tu sungusungu hata uzoaji taka na michango mbalimbali ya kimaendeleo, unaposema uliwashinda mahakamani wakakuacha,ungetupa pia ground ya kesi iliyofunguliwa ili na sisi tujifunze, kwa ninachojua wanazengo wakipitisha jambo lao lazima ulitii, ninyi ndio mnaojifanya wababe kwenye kadamnasi ila weupe gizani
Acha upotoshaji inamaana ukipelekwa mahakamani kwa kukataa kulipa 2000 ya ulinzi? NafikIri hakimu labda alikuona hayawani wa mwituni ndio maana akakuacha usije kuwararua wafungwa wenzako,
NOTE: Kwa sasa kila kata kuna polisi kata mwenye angalau nyota moja, kazi yake ni kuratibu shughuli zote za ulinzi katika eneo lake la kimamlaka,
ACHA UJUAJI NA UPOTOSHAJI
NIMEMALIZAA
 
Back
Top Bottom