Rais2020
JF-Expert Member
- Jul 14, 2016
- 3,248
- 5,537
Kwa ufupi
Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inabainisha uwiano sahihi wa mwalimu kwa wanafunzi (PTR) katika shule za msingi kuwa ni mwalimu mmoja kwa watoto 40 (1:40).
By Saumu Mwalimu na Nuzulack Dausen, Mwananchi
Wakati shule za msingi zikimaliza mwezi wa kwanza katika muhula mpya wa masomo wa 2017, walimu kutoka nusu ya shule za umma nchini watalazimika kufundisha idadi ya wanafunzi juu ya wastani unaotakiwa kutokana na uhaba wa watumishi hao.

Serikali imekuwa ikijitahidi kuajiri walimu lakini hadi Desemba mwaka jana, takwimu za Tamisemi zinaonyesha bado kulikuwa na uhaba wa walimu 47,151 wa shule za msingi, idadi inayozidi kidogo jumla ya walioajiriwa katika shule za msingi za umma na binafsi kwa miaka 10 iliyopita ambao ni 45,528.
Uchambuzi wa takwimu za uwiano wa mwalimu na wanafunzi kwa shule za msingi za umma mwaka 2016 uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa pamoja na jitihada za Serikali kuongeza watumishi wa umma, bado asilimia 58 ya shule za msingi zina uwiano wa juu ya kiwango kinachotakiwa.
Me: kuna uwezekano mkubwa sana wa kudhalisha watoto wasiojua kusoma na kuandika mpaka anafika darasa la Saba.
Ushauri: Elimu bure iendane na elimu bora. Ajiri walimu wafundishe watoto kwa matokeo mazuri zaidi. Elimu bure bila walimu wa kutosha ni sawa na kuruka sarakasi kwenye transformer.
Source: Mwananchi
Monday,30,2017