t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 6,369
- 14,762
Siku moja ,Nilipanda basi la mkoani (sio TZ),bus attendant akaweka documentary film ,nakumbuka jinsi abiria walivyokua wakibadilishana mawazo kutokana na facts zilizokua zinasimuliwa kwenye documentary ile,(sijaikumbuka jina ila ilikuwa kuhusu tafiti za kisayansi) , wakati wa kurudi nikapanda basi jingine,lenyewe nalo , kama lile la mwanzo kulikuwa na documentary inayohusu mazingira . Nilistaajabu sana na jinsi abiria walivyokua na uelewa wa juu sana ,hasa katika kutoa na kupinga hoja . hali ni tofauti sana kwenye luninga za vyombo vyetu vya usafiri, utakuta unawekewa kwaya ,movie za bongo ,taarabu n.k. vitu ambavyo kimsingi havitujengi kuwa na maarifa.
My take: Inawezekana kuwa ni moja ya sababu ya watanzania, kutokuwa too demanding kwenye maarifa.
My take: Inawezekana kuwa ni moja ya sababu ya watanzania, kutokuwa too demanding kwenye maarifa.