Kuna ugumu gani kubadilisha mfumo wa timu zetu za soka na kuwa kampuni?

Fikra Angavu

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
301
105
Mpira wa miguu Tanzania unatakiwa kubadilisha mifumo wa kiutendaji na uendeshaji.. Ili kuleta maendeleo ya soka na wanaojihusisha na soka kwa ujumla... na kuleta maendeleo kwa taifa...

Kuna haja ya TFF kuweka sheria au kufikia maamuzi ya kuvitaka vilabu vyote Tanzania kubadilisha mfumo wa kiutendaji na kua wa kampuni... Ili kila idara iendeshwe kisomi na kwa malengo ya kampuni ili kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kampuni kwa ujumla...

Hivi vilabu vikiwa kampuni.. kuna faida nyingi zitapatikana;

1. Mipango endelevu kuhakikisha kampuni inakua na kuleta faida.

2. Uwekezaji katika vilabu hivi utaongezeka.

3. Itaongeza ajira kwa vijana na wote wenye uwezo stahiki.. kuanzia wachezaji mpaka professions nyingine.

4. Hapa ndipo kila timu itaweza kuendesha miradi ya kukuza watoto, timu B. Kuuza bidhaa... kuwezesha wachezaji wao kua bidhaa na kuongeza kipato.

5. Ukuaji wa hawa wachezaji utaongeza ajira kama mawakala.. wanasheria na watu wengine.

6. Itapunguza pia hujuma baina ya wanao husika na mpira.

Hawa wanaoitwa wanachama... wabaki kua mashabiki au wawe wanahisa katika hizi kampuni..

Najua kuna watu watasema kuna watu watakufa njaa.. wanategemea kula hapo hapo kwenye izo timu...

Hapa mnazungumzia wale wanaoendesha timu kiholela bila elimu au wenye uweledi na mambo ya soka...?

Tatizo liko wapi...? ni kukosekana kwa viongozi wenye malengo chanya na mpira wetu au ni nini…!?
 
Tatizo ni maslahi binafsi, kuna watu wanazitegemea klabu za mpira kujikimu maisha yao on a daily basis, mfumo wa kampuni utawakwaza watu wa aina hiyo, rejea yaliyomkuta Reggie Mengi alipojaribu kuiingiza Yanga kwenye mfumo wa kampuni! Kwa kifupi tatizo ni narrow selfish interests basi!
 
Wale wenye njaa wanaonufaika na mfumo wa sasa ndiyo tatizo. Ni wanachama wa vilabu lakini ada zao hulipwa na wagombea wakati wa uchaguzi.

Bila kuondoa mfumo wa kijima na kujiendesha kama kampuni, vilabu vyetu vya mpira vitabaki kuwa vilabu vya wacheza bao mtaani kama ilivyo sasa.
 
Kuna haja ya wadau kuishinikiza serikali kuingilia kati hili swala na kuufanya mpira kama ajira zingine... ili kuwafanya hawa viongozi wa mpira wawajibike kama vile inavyofanyika China....
 
Mkuu bjereko, naonaumekuja na swali zuri sana.
Mimi naona tatizo ni akili ndogo kutawala akili kubwa, na ukienda mbali zaidi ni kama vile 'akili kubwa' haiko kabisa maana ingelikuwepo basi ingelikuwa imeshaishinda 'akili ndogo' na kugeuza hivi vilabu.
Matumaini yapo na hasa tukiangalia kinachoendelea Chamazi pale taasisi kama NMB inapooona ni rahisi kuingia mkataba na timu isiyo kubwa lakini iliyo na mfumo mzuri wa uendeshwaji badala ya timu 'ndogo' huku zikikuzwa na mashabiki uchwala!
 
Ndio ninachosema... hizi timu zikiwa kampuni lazima makampuni yatawekeza kwao...

Ni wakati sasa hizi akili kubwa hata kama ni wachache... ni wakati wa kujitoa na kuleta mapinduzi yatakayo ongozwa na serikali...!
 
Mkuu bjereko, naonaumekuja na swali zuri sana.
Mimi naona tatizo ni akili ndogo kutawala akili kubwa, na ukienda mbali zaidi ni kama vile 'akili kubwa' haiko kabisa maana ingelikuwepo basi ingelikuwa imeshaishinda 'akili ndogo' na kugeuza hivi vilabu.
Matumaini yapo na hasa tukiangalia kinachoendelea Chamazi pale taasisi kama NMB inapooona ni rahisi kuingia mkataba na timu isiyo kubwa lakini iliyo na mfumo mzuri wa uendeshwaji badala ya timu 'ndogo' huku zikikuzwa na mashabiki uchwala!
Azam sio timu ya kuitolea mfano, uendeshaji wao ni tofauti kabisa na huo unaoupendekeza
 
Mpira wa miguu tanzania unatakiwa kubadilisha mifumo wa kiutendaji na uendeshaji..
Ili kuleta maendeleo ya soka na wanaojihusisha na soka kwa ujumla... na kuleta maendeleo kwa taifa...

Kuna haja ya TFF kuweka sheria au kufikia maamuzi ya kuvitaka vilabu vyote Tanzania kubadilisha mfumo wa kiutendaji na kua wa kampuni...

Ili kila idara iendeshwe kisomi na kwa malengo ya kampuni ili kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kampuni kwa ujumla...

Hivi vilabu vikiwa kampuni.. kuna faida nyingi zitapatikana.
1. Mipango endelevu kuhakikisha kampuni inakua na kuleta faida.

2. Uwekezaji katika vilabu hivi utaongezeka.

3. Itaongeza ajira kwa vijana na wote wenye uwezo stahiki.. kuanzia wachezaji mpaka professions nyingine.

4. Hapa ndipo kila timu itaweza kuendesha miradi ya kukuza watoto, timu B. Kuuza bidhaa... kuwezesha wachezaji wao kua bidhaa na kuongeza kipato.

5. Ukuaji wa hawa wachezaji utaongeza ajira kama mawakala.. wanasheria na watu wengine.

6. Itapunguza pia hujuma baina ya wanao husika na mpira.

Hawa wanaoitwa wanachama... wabaki kua mashabiki au wawe wanahisa katika hizi kampuni..

Najua kuna watu watasema kuna watu watakufa njaa.. wanategemea kula hapo hapo kwenye izo timu...

Hapa mnazungumzia wale wanaoendesha timu kiholela bila elimu au wenye uweledi na mambo ya soka...?

Tatizo liko wapi...? ni kukosekana kwa viongozi wenye malengo chanya na mpira wetu au ni nini…!?
Tatizo malengo la ulaji yataosekana hapa watu wanabadilishana ulaji sio uongozi wa maendelea ya tim ambazo
 
Tatizo ni maslahi binafsi, kuna watu wanazitegemea klabu za mpira kujikimu maisha yao on a daily basis, mfumo wa kampuni utawakwaza watu wa aina hiyo, rejea yaliyomkuta Reggie Mengi alipojaribu kuiingiza Yanga kwenye mfumo wa kampuni! Kwa kifupi tatizo ni narrow selfish interests basi!
Uko sahihi ndugu, uliyoyataja hapo juu ndiyo yaliyomkuta Mohamed Dewji hivi majuzi, alipotaka Simba wauze hisa DSE na kuwa kampuni ili wafaidike na hisa. Uongozi wa Simba wamekalia mafaili mpaka kesho.
 
Kifanyike nini sasa.... ili tutoke kwenye haya matatizo... mi ndio kitu nataka tuzungumze...
nini kifanyike...!?
Serikali iandae mikakati na sheria...
au wadau wenyewe tufanye mapinduzi..!?
 
Tumekosa viongozi ambao wana nia ya kuleta mabadiliko kwenye mpira wa kitanzania wengi wanatafuta majina kwenye vilabu ili baadae waingie kwenye siasa au kuzitangaza biashara zao,bila kubadilisha mfumo viongozi wanaweza kufanya yafuatayo

1.Kuongeza idadi ya wanachama hai
Tanzania tunakaribia milion 50 lakini klabu zetu(Simba/Yanga) wanachama hai hawafiki hata laki moja,nina amini Simba/Yanga kila klabu inaweza kuwa na wanachama hai angalau milioni 2 na mfano ada ya uanachama kwa mwaka ikiwa Tshs 5000 (elfu tano) .Klabu inaweza kuingiza kiasi cha bilioni 10 kwa mwaka kama hao wanachama hai watalipa ada ya mwaka

Klabu kupitia maafisa habari/afisa masoko/katibu wanaweza kuanzisha kampeni kuanzisha mfumo wa kuandikisha wanachama wapya.Wanapewa target idadi ya wanachama kila baada ya miezi 3

2.Kuzitangaza Klabu kwa wanachama hai
Mfumo uliopo sasa wanachama hawana sauti,klabu zinaendeshwa na viongozi na wanafanya maamuzi karibia yote pasipo kuwashirikisha wanachama.Kwa nini wanachama karibia wote wako hapa Dar,Je mwanachama aliyepo Sumbawanga,Kasulu,Moshi,Dodoma,Mbinga etc ana mchango wote kwenye timu.Kuna mikoa hata kuiona hiyo timu inaweza kupita hata miaka 5 hajaiona live ukiacha kuiona kwenye TV na sio wote wana access ya TV.

Klabu inaweza kuandaa ziara kila mwaka kuhakikisha timu inafika kila mkoa (au kuanzia kwa kanda) na wanacheza mechi za kirafiki kufungua matawi na kushiriki baadhi ya shughuli za kijamii na kutoa misaada kama hospital,shuleni na vituo vya yatima.Kingine ni kuandaa vipindi vya TV kutangaza klabu (nafikiri Azam wanacho )

3.Kutengeneza na kuuza bidhaa za klabu
Ukitaka kuona hizi klabu zinavyopoteza mapato nenda uwanjani jinsi wanavyocheza utaona jinsi baadhi ya wafanyabiashara wanavyotengeneza jezi na kuziuza klabu zikiwa hazipati hata shilingi tano .Bidhaa kama jezi,sweta,jacket,sandals,kofia,skafu,keyholders,taulo,kalenda,bendera na vinginevyo ni mojawapo ya vitu ambavyo vinaweza kuongeza mapato ya klabu na kupunguza utegemezi kutoka kwa viongozi/watu binafsi.Viongozi wakishirikiana vizuri na huu uongozi wa awamu ya tano naamini wanaweza kupunguza au unyonyaji unaofanywa na wafanyabiashara kuingiza mapato kupitia mgongo wa klabu

4.Kutengeza kumbukumbu,taarifa na historia ya klabu
Ni aibu sana hizi klabu zimeanzishwa muda mrefu na zina historia,na matukio mbalimbali ambayo yalitokea huko nyuma
Kwa teknolojia ya sasa yanaweza kutengenezewa documentary kwa kuwahoji baadhi ya viongozi,wachezaji,mashabiki na wanachama waliokuwepo enzi hizo.Matukio kama Simba kufika fainali ya CAF, Mechi ya Simba vs Yanga iliyocheza Mwanza 1974,Coastal Union walivyochukua ubingwa 1988,Yanga ile ya Lunyamila walivyochukua kombe kule Uganda yanapaswa kuandikwa au kutengenezewa documentary ili kuendelea kutunza historia ya klabu.Klabu zina website lakini hakuna habari za kutosha

Siamini kama kufanya hayo klabu zinahitaji kubadilisha mfumo wa uendeshaji ni ubunifu tu wa viongozi wao ndio wanaweza ku-propose kwa wanachama wakaamua na sidhani kama kuna wanachama wanaweza kupinga mawazo ambayo hayata ondoa umiliki wao kwa klabu bali yatapunguza utegemezi kwa watu binafsi.Pia inaweza kusaidia hata TFF ikaja kupata viongozi wa kuleta mabadiliko kwenye mpira wetu
 
Kuna tatizo gani kama mfumo ukabadilika na zikawa kampuni.
Alafu hawa wanachama wakapewa elimu ya kununua hisa za kampuni hizo na kua sehemu ya wamiliki wa kampuni hizo...?

Swala la maamuzi ni kuwe na vikao vya wanahisa kila mwaka... bodi na pia vikao vya watendaji (ma meneja wa kila idara "masoko, rasilimali watu, mahusiano nk.") kama sehemu ya kampuni ili kuwawakilisha wao na kufanya kazi kwa niaba ya wanahisa na bodi na mashabiki.

suala la wanachama ndio hii kila siku tunasikia wao ndio wana sajili na kuingilia maamuzi ya kocha...

Na hili swala la kampuni ni kila timu kuanzia daraja la kwanza mpaka la mwisho (sio simba na yanga).. ziwe ni kampuni.
ziendeshwe kiuweledi.

Tunazungumzia swala la kuongeza idadi kubwa ya ajira. Hasa vijana ambao ndio soka lina waangalia sana...

Mi suala la wanachama siungani na wewe kabisa... tupo katika dunia nyingine na kila kitu ni ushindani...
imefika muda soka liongozwe na wenye iweledi wa soka na hao wanaojua kuleta faida kupitia soka
 
1.Yani ufungue kampuni then ndio uje uwaelimishe wanachama ?

2.What is so special with kampuni ? Tupe mifano

3.Timu zinapangwa na viongozi au wanachama (Kaburu,Hans Pope,) ? Tupe mifano ya hao wanachama unaosema

Real Madrid,Bayern Munich,Barcelona ni timu zinaendeshwa na wanachama na zina mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja
 
Back
Top Bottom