Kuna Ufisadi wa kutisha Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA)

Moshi town

Senior Member
Dec 7, 2021
171
120
Kuna ufisadi Mkubwa unafanyika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha (AUWSA). Ufisadu huu unafanywa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi AUWSA, Eng. Justine Rujomba kwa kushirikiana na Waziri wa Maji Ndg. Juma Aweso na Katibu Mkuu Engineer Sanga.

Kuna Mradi wa Ujenzi wa Mtandao wa Uondoaji huduma ya Majitaka Eneo la Kisongo A to Z wenye thamani ya Tzs 3.5 bilion amepewa Mkandarasi 'Tumaini Engineering' bila tenda kutangazwa huu ni ukiukwaji wa taratibu za Ununuzi pamoja na Waziri wa Maji Ndg. Aweso, Katibu Mkuu Eng. Sanga na Bodi ya AUWSA chini ya Dr. Masika kuwa na taarifa juu ya Ufisadi huu wameshindwa kuchukua hatua yoyote.

Watumishi wa AUWSA waliandika barua kwa Waziri Aweso kumtaarifu juu ya Ufisadi wa Mradi wa Majitaka wa A to Z cha kusikitisha Waziri alimpatia barua MD wa AUWSA na kumtaadharisha kukaa mbali na Technical Manager Eng. Humphrey Mwombelwa badala ya Waziri kuifanyia kazi barua yeye akamchonganisha MD na TM hivyo kumlazimisha TM kuacha kazi. Ni aibu na Kinyume cha Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Waziri kutoa taarifa za siri kwa mhusika.

Serikali ilitoa TZS 3 billion zitumike kujenga mtandao wa majisafi Longido hadi Namanga kwa kutumia Force Account, cha Kusikitisha MD wa AUWSA ameipatia kazi ya Ujenzi kampuni ya Tumaini Engineering bila kufuata taratibu za Ununuzi zabuni haikutangazwa kama taratibu zinavyotaka.

Pamoja na Serikali kuzuia Posho, Management ya AUWSA na wasimamizi wa mradi kila mwisho wa Mwaka wanajilipa posho kila Mmoja TZS 1 Million hadi 5 Million za Sikukuu ya Noeli (Christmas) huku upotevu wa Maji NRW ukiwa ni asilimia 54. Serikali ilishapiga marufuku Posho za Sikukuu.

Ofisi ya Rais, Waziri Mkuu, PCCB Makao Makuu (PCCB wa Arusha wamewekwa Mfukoni) tuna imani sana na ofisi zenu; tumeni wakaguzi huru wachunguze Ufisadi unaondelea AUWSA.
 
Mkuu kaa kimya watu wapige pesa huu ni mwisho wa mwaka na January kuna mambo mengi sn hii itasaidia mzunguko wa pesa mtaani, bilioni 3 ni pesa kidogo sn maana hawa wakubwa wanapiga mabilioni ya pesa
 
Mkuu kaa kimya watu wapige pesa huu ni mwisho wa mwaka na January kuna mambo mengi sn hii itasaidia mzunguko wa pesa mtaani, bilioni 3 ni pesa kidogo sn maana hawa wakubwa wanapiga mabilioni ya
MD auwsa na Aweso wanakula kama Mchwa, kuna Ufisadi mwingine Mkubwa wa Uniform za Watumishi badala ya kununua uniform ( Sharti) Mmoja kwa Tzs 20,000/= Auwsa imenunua Uniform Mmoja kwa Tzs 54,000/= Procurement Officer Madam Mija aligoma kufanya ufisadi huu kumwadhibu wamemuamishia pondi ya Majitaka ili kumkomoa.

Makoti ya Overal wananunua Kwa Tzs 40,000/= Gharma ni tofauti na kitambaa ukiweka na kitambaa Jumla inakuwa 80,000/=

Management kila Mwaka wanapewa 14 Milion za kununua Sofa

Management na Watumishi wa Project kila Disemba wanavuta Tzs 2 Milion hadi 5 Milion then wafanyakazi ambao wana toil Mwaka Mzima (Juha lao Mvua yao) wanapewa Tzs 50,000/= ya Sikukuu tena wanaambiwa waje Jumamosi

Kama siyo kuwanyanyasa ni nini? Wengine wanapokea Tzs 2 Milion hadi 5 Milion then wafanyakazi wa Chini wamapokea 50,000/= siyo sawa

Waziri Aweso ana Taarifa zote huyu Mswahili Mwenzetu wa Tanga akishavuta pesa kutoka Auwsa anarudisha taarifa kwa MD .. Aweso ni hatari sana amefanya TM mahiri Eng Humphrey kaacha kazi

Kila akivuta pesa anamwambia MD wa Auwsa akae makini na TM wake Mwisho wa Siku wakamfrustrate TM akaondoka..
 
Huyu Waziri namjua vzr mamlaka nyingi za maji ameweka watu wake wa karibu sn, kimsingi mkuu hii nchi ni shamba la bibi kila mtu ale kwa urefu wa kamba ake hakuna namna maana pamejaa uozo tupu kila kona.
 
😁😁😁
1638006971_1638006971-picsay.jpg
 
Rais alisema anataka kuongeza mzunguko wa pesa mtaani mlidhani anaenda kuzitupa barabarani? Mzunguko wenyewe ndiyo huu watu wapiga pesa haswa kwenye miradi wanakuja kununua bia, kuhonga, kula mbuzi katoliki na mengine
Na huku wewe unakandamizwa na TOZO na mpaka vizazi kumi vijavyo vitakuwa vinalipa Madeni ya Mikopo iliyotokana na huu ubadhirifu, mbaya zaidi badala ya mabomba kutoa maji yanatoa hewa.
 
Na huku wewe unakandamizwa na TOZO na mpaka vizazi kumi vijavyo vitakuwa vinalipa Madeni ya Mikopo iliyotokana na huu ubadhirifu, mbaya zaidi badala ya mabomba kutoa maji yanatoa hewa.
Utafanyaje sasa watu wamejitungia sheria za kutoshitakiwa? acha waibe mpk tupate akili hakuna namna mwananchi huna la kusema mpk Rais apende
 
Hizi kauli huwa najiuliza kama wananchi hawa either wanahusika katika huu wizi au hawajui kwamba pesa hizo ni za kwao / kwa manufaa yao...

No wonder tunazidi kurudi nyuma kila kukicha...
changamoto ni mfumo mbovu, angalia Sabaya alikuwa anavunja maduka ya watu na hakuna mtu wa kumgusa isipokuwa Rais pekee, hakuna kitu wewe ukipata nafasi piga pesa kaa pembeni.
 
Back
Top Bottom