Kuna Uchawi au Uganga unaweza kufanya ukaongezwa mshahara au kupandishwa cheo kazini?

Mawazo ya kichawi na ulozi yanapunguza uwezo wa akili kuchanganua mambo ya kimsingi.....akili inajengeka kutazamia vitu vya kufikirika kuliko uhalisia.....na hiyo inahamia kwenye viungo vya mwili na kuathiri utendaji wako wa kazi........

Wote waliojenga maisha Yao kwenye misingi ya kichawi na ulozi wamesha ANGAMIA.....
 
Hao wachawi wangekuwepo Mimi ningehakikisha nakuwa Rais. Fanya kazi kwa bidii na maarifa tu. Hiyo ndiyo ndumba yenyewe na si mganga wala uchawi. Ila kuna ngekewa pia yaani bahati. Wanasema Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
 
Hayo mambo yapo sana na bila hivyo hutoki lazima uwe na upande umesimamia sehemu yoyote Kama ni Mungu Basi kwa kiwango Cha kujua vifungu vya kukuongoza kwenye Kila Jambo wewe Kama wewe na Kama ni upande wa waganga kwenye sehemu yoyote usimwamini mtu labda Kama unafanya kwa utafiti wako ukapata mtu sahihi maana Kuna mengi huyo anayekupeleka anaweza kukuharibia pia baada ya kujua mambo yako ya sirini, kitu kinachowasaidia wengine nikupata mafunzo kwa wale waliokulia kwa mabibi na babu zao wakawa wanajua hayo mambo huwa wanawaelekeza mbinu za kufanya kujisaidia kwenye maisha ambazo hazina madhara. Ila kwenye kazi kanuni za juhudi, maarifa, na maadili zikizingatiwa.
 
Hata nikisimulia matukio ya kichawi niliyo wahi shuhudia bado watu watabisha kwanini? kwa sababu hawamini uchawi..
Nikwasababu matukio ni personal experience na personal experience ni logical fallacy

Kuna roommate alikua anakemea usiku akidai wachawi wamekuja kumjaribu baafa ya kuona kitanda kinatiskisika. Na kweli ukiangalia unaona kitanda kinatikisika as if kuna watu invisible wamekishikilia wanakitingisha lakini uhalisia haukua hivyo ilikua ni teteko la ardhi

Just imagine yule msela asingejua kua ni tetemeko halafu baada ya muda kupita angehisi maombi yake ndio yamefukuza wachawi kumbe hamna kitu. Msele angeweza kutumia personal experience kama hiyo kueneza uongo bila ya yeye kujua
 
Mama mmoja nchi ya mbali alikuwa ameolewa na mme mwenye wake wawili.Yule mke akaona mumewe hampendi kama mke mwingine akaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji.

Yule mganda akamuambia sharti dawa ifanye kazi amletee unyoya wa simba dume yale manyoya ya kichwani wanaita Lion manes.Yule mama alitafakari sana akakumbuka kijijini kwao kuna tabia ya simba dume mmoja mzee sana kupenda kuja asubuhi kuota jua kwenye jiwe flani kila siku asubuhi.

Akajiwa na wazo atafanyaje kumtoa unyoya bila kuraruliwa.Siku ya kwanza alichinja kondoo akagawa nyama za kutosha akaweka juu ya lile jiwe.Yule simba Akaja akazila.Aliufanya huo ukawa ndio utaratibu wa kupeleka nyama kwenye lile jiwe hadi yule simba hata siku hakuna jua alikuwa anakwenda kwenye lile jiwe akijua atapata chakula.

Ilifikia mahali yule simba akamuona yule mama akajua ndio anayemletea nyama kila siku akapunguza ukali wake.Siku moja moja yule mama akawa kabla hajampa nyama anamkuna kuna yule simba kwenye mgongo wake simba akawa anajisikia vizuri sana kwani alikuwa anamsaidia kutoa viroboto.

Siku ya siku akampapasa yule simba akamtoa ule unyoya simba akawa ametulia.Yule mama alijawa na furaha isiyo na kifani akaenda kwa mganga akampa.

Yule mganga alifurahi sana akamtengenezea dawa za uongo ila akampa sharti mumewe kuwa apunguze ukali awe mpole kwa mumewe amtengee chakula kwa lugha nzuri huku amemuwekea dawa kwenye chakula ya uongo.Kwa kifupi yule mganga alimuambia kamtendee mumeo kama ulivyomtenda yule simba mzee atakupenda mno.

Yule mama alifuata masharti yote toka siku hiyo mumewe alimpenda mno mno kuliko mwanzo alikuwa hamdharau mumewe kuwa amezeeka anampa chakula kitamu na maneno mzuri

FUNZO:-Unaweza ukawa unaona flani ana tatizo kumbe tatizo ni wewe mwenyewe.Ukiwa kazini ukifanya kazi kwa bidii kujituma sana uwezekano wa mafanikio kupanda ni mkubwa mno.Unapokuwa mvivu kazini na mchelewaji mganga atakuambia uwe unahakikisha ndani ya geti kila siku unakuwa wa kwanza kuiingia kumbe kuchelewa kwako kazini kulikuwa ndio kunafanya usipande cheo ila mganga katumia mbinu ukajirudi.Mafanikio yako kazini ni juhudi zako sio waganga wa kienyeji
 

Attachments

  • lion mane.PNG
    lion mane.PNG
    398.9 KB · Views: 5
Watu wanajifanya kama hawaishi Africa /Tanzania.Uchawi makazini /sehemu za biashara upo Sana .Me nimefanya kazi sehemu jamaa ni business taycon kibongo bongo Ila bado anaroga tu
 
Performance ya mtu pamoja na nidhamu ya kazi ndio inampa mtu nafasi ya kukua kazini. Inaelekea huyo rafiki yako anavyo vyote ila sababu anaamini kwenye hizo mambo basi ataona ndio zinamsaidia kumbe juhudi yake binafsi na mapenzi ya Mungu vinatosha
Hizi ni sound tu.....kama mfumo haujakukubali sahau kuoanda cheo au kuongezwa mshahara...ni bahati sana
 
Dawa ya kazi ni KAZI
Jibu zuri na ufafanuzi wa hiyo dawa, huyo jamaa yako akwambie
 
Habari,

Aise mimi kuna mahali nafanya kazi ila sasa kuna mtu nafanya nae kazi ananiambia we kaa hivyo hivyo usihangaike. Sasa huyo anaenimbia hivyo ni mtu alikuwa kitengo kingine akahamishwa akapelekwa kingine chenye nafuu kidogo

Halafu sasa ananiambia kashapewa barua ya kuongezewa mshahara ila sasa usemi wake kila akiniona ofisini ananiambia mdogo wangu karoge, hangaika

Je, naomba kujua kama kuna ushuhuda wa ukweli kuhusu uchawi wa namna hii upo kweli?
Awamu hii vituko vyote tutaviona
 
Habari,

Aise mimi kuna mahali nafanya kazi ila sasa kuna mtu nafanya nae kazi ananiambia we kaa hivyo hivyo usihangaike. Sasa huyo anaenimbia hivyo ni mtu alikuwa kitengo kingine akahamishwa akapelekwa kingine chenye nafuu kidogo

Halafu sasa ananiambia kashapewa barua ya kuongezewa mshahara ila sasa usemi wake kila akiniona ofisini ananiambia mdogo wangu karoge, hangaika

Je, naomba kujua kama kuna ushuhuda wa ukweli kuhusu uchawi wa namna hii upo kweli?
utapeli tu ndo umekithir saiz
 
Kuna jamaa angu alikua anampenda demu flani......akaenda kwa mganga flani sijui alimjulia wapi na nilimsindikiza mim mwenyew.....siku hyo tumetoka tu kwa mganga .......ilikua usiku......asubuh ghafla jamaa anagongewa mlango na demu........
Akamuomba jamaa watoke nje waongee.......bwana wee....si demu akaanza kujieleza kiasi gani anampenda kishenzi na usiku huo hajalala kumuwaza tu mshkaji......jamaa nae ili kulevel Mambo akamwambia tu demu kwamba nae ni kitambo anampenda demu ila alikua anashindwa tu kumwambia.........

Wakaanza mahusiano...
Hiyo ilikua 2012.....mwaka 2016 walioana na sa hv ni wanandoa na watoto wawili.....

Huwa najiuliza maswali mengi Sanaa kwnye hili nililolishuhudia na majibu sipati
Na wewe hujajiongeza kama mwenzako?
 
Basi maisha yangekua simple sana, watu tusingekubali kupoteza pesa kusomesha watoto wetu wakati kwa mganga mambo supa

Lakini hata hivyo tungeona zile department nyeti zina endeshwa na mabosi waganga ambao wamekubuhu kwa uchawi
Uchawi wa namna hiyo ungekuwepo, wa kwanza kuingia kwenye hizo nafasi na kupata pesa nyingi ni mchawi mwenyewe.
 
Hayo mambo yapo sana na bila hivyo hutoki lazima uwe na upande umesimamia sehemu yoyote Kama ni Mungu Basi kwa kiwango Cha kujua vifungu vya kukuongoza kwenye Kila Jambo wewe Kama wewe na Kama ni upande wa waganga kwenye sehemu yoyote usimwamini mtu labda Kama unafanya kwa utafiti wako ukapata mtu sahihi maana Kuna mengi huyo anayekupeleka anaweza kukuharibia pia baada ya kujua mambo yako ya sirini, kitu kinachowasaidia wengine nikupata mafunzo kwa wale waliokulia kwa mabibi na babu zao wakawa wanajua hayo mambo huwa wanawaelekeza mbinu za kufanya kujisaidia kwenye maisha ambazo hazina madhara. Ila kwenye kazi kanuni za juhudi, maarifa, na maadili zikizingatiwa.
Uchawi kama ilivyo dini unahusu imani. Imani maana yake ni kukubali uwepo wa kitu hata kama hakuna ushahidi wa kuwepo. Ndugu zangu Wakristu, Waislamu, Wahindu, Wapagani, na wengineo wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini hawana uthibitisho wa uwepo wa Mungu. Kuna wale wajiitao Atheist, wao wanasema kuwa kama kweli Mungu yupo, utolewe uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu. Mpaka sasa kuna waumini wengi hawana uhakika na kuwepo kwa Mungu lakini wanaogopa kuwa na shaka hiyo kwa sababu wanatishiwa na moto wa Jahanamu. Cha ajabu kuliko vyote, ni wachawi kuwa na imani ya kuwepo kwa Mungu huku wakiendelea na yale yasemekanayo yanakatazwa na Mungu. Ukweli ni kuwa wachawi wapo, uchawi upo, swali ni je uchawi unafanya maajabu ambayo watu wanadai unafanya? Pamoja na wachawi na uchawi kuwepo lakini nguvu na uwezo unaosemekana wanao ni uongo mtupu. Wewe ukiwa unaamini uchawi, utafanyiwa mazingaombwe na kuamini, lakini hamna lolote. Miaka ya 70/80 nikiwa nafanya kazi sehemu fulani, kulikikuwa na madareva wawili, mmoja Mmakonde na Mwingine anatoka Moa, Tanga. Basi hawa wawili kila siku kutambiana na waliogopwa saana. Siku moja yule Mmakonde alikosana na mfanya kazi toka Mara. Wakapeana maneno, na yule jamaa wa Mara kamwambia Mmakonde kuwa "nasikia unajidai wewe ni mchawi na unaogopewa. Hapa kwangu umefika na ukifikiria tu kuniroga unaanguyka na kufa. Watu wote kazini walishangaa ujasiri huyu jamaa wa Musoma. Watu walidhani atadhurika lakini hadi leo anadunda na nafikiri yuko kwenye 80 na maisha yake ni mazuri. Basi pakle kazini wakavumisha kuwa huyu Bw. ni mchawi wa kupindukia. Mimi niliwahi kuongea naye kuhusu hili, akasema huyu Mmakonde si lolote. Watu wanaomuogopa tu. Hizo dunguli zake ni kwa waoga tu. Akasema yeye anaogopa mtu akimtishia kumkata panga na wala si uchawi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom