Kuna ubaya wowote kutoboa masikio?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,017
2,384
Wakati nikiwa mdogo wazazi wangu walinitoboa kla sikio kishimo kimoja. Mimi nimependa kuongeza, nimeenda kuongeza kla sikio vishimo viwili jumla vimekuwa vitatu kla sikio. Sasa leo mama ameniona nimevaa hereni ameanza kusema kwann nimetoboa? Kwann sikumwambia km natoboa? Ati unatabia za ajabu unaiga tu. Ati nisikuone unavaa hereni kwa hayo mashimo mengine km kuvaa vaa kwa shimo moja tu kla sikio 🙄 namuuliza kwann anasema "ndio nimesema sitaki kukuona unavaa mihereni mingi" nimebaki nashangaa 😨

😨 Kwan kuna tatizo mtu kuvaa hereni nyingi? Hivi kwann wa mama wa kiafrica wanapenda sana kukuza mambo? Ati kwann sikumwambia? km vile sikio lake. Mwili wangu lakn anataka nimpe habari kla ninachofanya kwa mwili wangu.
 
Mara nyingi tabia ya mtu inaanza kutafsiriwa kwa muonekano wa nje....inategemea na anayekutizama anakutafsiri vipi

Binafsi kutoboa mara tatu natamani lakini naogopa maumivu
 
Kwa wazazi wetu na tulivyolelewa huo unaonekana uhuni wa hali ya juu...na hata mimi nikikutana na mtu wa staili hiyo namuona wa ajabu sana
 
Urembo mwingine ni ujinga tu,sasa kuvaa mihereni mingi ndio unapendeza au? wanawake walio natural wanavutia sana kuliko nyie mnaohangaika kujitoboatoboa
 
Hakuna atakaye kupenda,kukujali,kukuthamini. zaidi ya MAMA yako.

Msikilize MAMA yako.
 
Vikuku,
Tattoos ,
Hereni mengi masikion,
Kipini puani,
Kipini kwenye ulimi,lips na jichon,
Kipini kitovuni,
Mashanga mengi kiunoni,
Mapete mengi vidoleni(hii inategemea)

Mi nakuchukulia we ni kahaba mzoefu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi tabia ya mtu inaanza kutafsiriwa kwa muonekano wa nje....inategemea na anayekutizama anakutafsiri vipi

Binafsi kutoboa mara tatu natamani lakini naogopa maumivu
1675775608394.png
 

Attachments

  • 1675775608715.png
    1675775608715.png
    90 KB · Views: 25
Sio maskio tu, Mwanamke ni Urembo!

ila asizidishe kipimo cha Urembo! Toboa mara 1 upendeze muhimu ujue kupangilia hizo Hereni huko sikioni.

Binafsi napenda mwanamke Atoboe hata Pua, afanye kila analoweza litakalomfanya nimuone Mrembo!

Wanawake ni kama Nguo, kila mtu atachagua nguo aipendayo inayomkaa vizuri..

Binafsi napenda mwanamke Mrembo haswaaa, na anae enda na Fashion!

Tabia haipo katika muonekano japo.
 
Toka mdogo nilitobolewa masikio mara mbili.Nimefika ukubwani nikatamani kuongeza tobo lingine yawe matatu .Kuna muuza urembo huwa anasafisha kucha na kutoboa masikio tumemzoea hapa mtaani mana ni wa miaka mingi nilipomwambia nataka anitoboe akanambia acha hayo mawili yanakutosha usiongeze.
Nikajisemea bora kanambia ukweli na nikauchukua sikutaka tena kuongeza na wala sikumuuliza sababu ya kunishauri niache.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom