Kuna ubaya wowote kumchagua Kikwete awe Mfalme? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ubaya wowote kumchagua Kikwete awe Mfalme?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 23, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na Lula wa Ndali Mwananzela (Raia Mwema)

  [​IMG] President Kikwete and King Mswati III at a SADC meeting in Swaziland. Photo/FILE

  [​IMG]

  SAUTI zao zinazidi kupaa na mlio wake unazidi kuitikiwa katika kona mbalimbali za taifa letu. Mwangwi wa hoja zao unazidi kunguruma kwa uchokozi kama upepo unaotangulia kimbunga.

  Tunaambiwa mambo mawili ambayo yanaletwa kwetu kama ukweli: Kikwete ndiye mgombea pekee anayefaa kusimamishwa na CCM; kwani hakuna mwingine na pili; ndiye mgombea anayekubalika zaidi; kwani hata alipoingia madarakani ni asilimia 80 ya wapiga kura waliomchagua. Haya tunaambiwa ni ya kweli na kwa kipimo cha haraka haraka tunawapa jibu; "tumekubali".


  Kutokana na hayo mawili, sauti hizo zimeamua kupendekeza hitimisho lifuatalo: Rais Jakaya Mrisho Kikwete awe mtu pekee kuchukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Sauti nyingine zimeanza nazo zinataka kwenda mbele zaidi na hizi zipo kwenye upinzani.


  Hizi zinataka Rais Kikwete awe mgombea pekee wa urais mwaka huu. Wote hawa wanasema hayo kwa sababu hizo mbili: Kwamba Kikwete anakubalika zaidi na kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kuwa mbadala wake iwe ndani ya CCM au nje yake!


  Tuliyaona haya pia wakati Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alipokuwa akikaribia kumaliza kipindi chake cha kwanza cha urais. Walijitokeza watu (tena baadhi yao wazito) na kupendekeza kwamba kusiwe na wakujitokeza CCM kuchuana naye atakapochukua fomu kuwania urais kwa kipindi cha mwisho cha miaka mitano.


  Sasa jambo hili limerejea tena kwa kishindo katika utawala huu wa sasa wa awamu ya nne chini ya Rais Kikwete, na ndiyo maana katika makala hii nina pendekezo. Napendekeza wale watetezi wa dhana ya "ugombea pekee" wasiishie hapo; bali waende mbele zaidi.


  Kama kweli wanapenda na kweli wanataka wawe chini ya uongozi wa rais kwa muda mrefu zaidi bila kujali uchapakazi wake, basi, wasiishie kupigia debe dhana ya "mgombea pekee". Waende mbele na kufikia kwenye hitimisho la kimantiki, kwamba Tanzania tuanzishe mfumo wa utawala wa kifalme!


  Sasa sisemi jambo hili kimzaha; kama mtu anavyoweza kufikiria. Nimepima faida ya kufanya hivyo kwa taifa na kwa siasa za nchi yetu. Nimeona kuwa wananchi wote tukikubaliana na hoja zao hatuna budi kufikia hitimisho hili kuwa Tanzania inafaa kuwa na utawala wa kifalme.


  Unaweza kushangaa kuna faida gani kuwa na utawala wa kifalme?

  Kwanza, tukiwa na mtawala mmoja ambaye ni Mfalme hatutalazimika kufanya chaguzi za rais kila baada ya miaka mitano! Kwa vile tunakubaliana na dhana ya ‘mgombea pekee' na hatutaki mtu mwingine yoyote awe CCM au nje yake ajitokeze kugombea, basi, ni wazi mfumo wa kifalme ndiyo unaotufaa na unaotustahili.

  Kwa hiyo, tutaokoa fedha nyingi sana (mabilioni) ambazo hutumika kwenye uchaguzi. Fedha hizo zingetumika katika kuchukua fomu, kuzunguka kupata wafadhili, kampeni na baadaye uchaguzi. Kiasi hicho kinaweza kutumika kwenye shughuli nyingine za kuwaletea wananchi maendeleo.

  Pili, tukiwa na mfalme; hatakuwa na sababu ya kufanya mambo kwa ajili ya kuwaridhisha watu wake waliomkampenia kwa sababu hakutakuwa na uchaguzi. Hivyo, Mfalme atakuwa anatilia tu mkazo kufanya mambo yenye maslahi ya Taifa.


  Fikiria kwamba marais wetu wote ilibidi mara kwa mara wawaeleze wananchi mambo waliyoyafanya ili wasije kutoswa kwenye uchaguzi. Sasa tukiwa na mfalme wa kudumu, yeye hatokuwa na wasiwasi wa kutuelezea wananchi au kutubembeleza bembeleza. Atakuwa ni mtawala wetu kweli kweli; kwani hatokuwa na hofu ya kupoteza kura au kupingwa sijui na mpinzani gani!

  Nne, mfumo huu utavisaidia vyama vya upinzani vile vile. Mara kwa mara wapinzani wanatumia muda mwingi ili wafikirie jinsi ya kugombea nafasi ya urais wakati tayari wanajua watashindwa hata kabla upigaji kura wenyewe haujafanyika!


  Hili limekuwa likisababisha migogoro ya mara kwa mara ndani ya vyama hivyo, na kila unapokaribia uchaguzi mkuu, basi, kunakuwa na mvutano wa hapa na pale. Kwa kuwa na mfalme wa kudumu, hata viongozi wa upinzani watakuwa hawana sababu ya kugombania nafasi ya uenyekiti ili waje kugombea urais wa nchi.!


  Kwa hiyo, wapinzani watatilia mkazo zaidi viti vya ubunge kuliko urais; kwani tayari mtawala (mfalme) tunaye anayekubalika na wananchi wengi, kupendwa na kuheshimiwa na vizazi vingi vya Watanzania!

  Tano, itakisaidia pia Chama Cha Mapinduzi (CCM); kwani kwa mara ya kwanza tutaondoa masuala ya mizengwe ndani ya Chama. Tukiwa na mfalme wa kudumu, wana CCM hawatakuwa na sababu ya kuharibiana majina, kuchafuana (hata ikibidi kufoji picha) au kuitana majina mabaya.

  Hii itakifanya Chama Cha Mapinduzi kurudi kama wakati wa Mwalimu Nyerere ambapo walijua kabisa mgombea wao ni mmoja tu na uchaguzi wa ubunge ndio ulikuwa una utamu wake.


  Sasa hizo ni faida chache tu. Nina uhakika kama taifa na wasomi wetu wakifikiria sana wanaweza kuona faida nyingine nyingi zaidi kuliko hizo, na watakubaliana na mimi kuwa tukimpata mfalme mzuri anayekubalika na wengi (chaguo la Mungu) kutaliinua taifa letu mbele ya macho ya wafadhili na kutuonesha ni jinsi gani ‘tumekomaa' kidemokrasia.

  Najua kwa haraka pingamizi kubwa kwenye hoja yangu hii linaweza kutolewa; kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na tuna vikomo vya uongozi, na hivyo ni lazima viheshimiwe.

  Watasema kwamba Tanzania inao watu wengi wanaofaa na CCM inao watu wengi wanaofaa na kwamba marais wetu wataheshimu Katiba na kung'atuka baada ya vipindi vyao kukoma.


  Jibu langu kwao ni kwamba kama tayari tuna rais anayekubalika zaidi sasa hivi na kupendwa kiasi cha kutaka watu wengine wasigombee urais, basi, tayari demokrasia imeshapoteza maana yake.


  Kama kuna watu wenye kuipigia debe dhana ya ‘mgombea pekee' kwa sababu aliyepo sasa (Rais Kikwete) anakubalika, na hivyo kuwataka watu wengine (kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia) wasijitokeze kumpinga, basi, mfumo wa kifalme ndiyo unaotustahili; maana demokrasia hatuiwezi!


  Haiwezekani iwe demokrasia kwa Kikwete kutogombea kwa sababu ya ukomo, lakini isiwe demokrasia kwa watu wengine kumpinga!


  Ni kutokana na jibu hilo naamini tunaweza kwenda mbele zaidi na kufikiria kuwa na utawala wa kifalme kama zilivyo baadhi ya nchi duniani.


  Napendekeza badala ya kupoteza fedha kuandaa Uchaguzi wa Rais, uanzishwe mchakato wa kushawishi umma kuukubali mfumo wa kifalme ili baadaye atafutwe mtu anayefaa, atangazwe kuwa ni Mfalme na familia yake iwe Familia ya Kifalme (Royal Family).

  Sasa najua unaweza ukacheka pendekezo langu hilo ukidhania natania.


  Huko mbeleni naweza kupendekeza jinsi gani tunaweza kumpa maisha anayostahili Mfalme (sijui kama tufuate mfano wa yule wa Swaziland, Mswati (III). Tukiwa na Mfalme na sisi tutakuwa tumejiweka kwenye mataifa ambayo yana wafalme na yameendelea au yanapiga hatua mbele ya maendeleo kama UAE au kule Jordan.

  Hivyo, uchaguzi huu wa 2010 uwe wa wabunge na kura ya maoni juu ya kubadilisha mfumo wetu wa kijamhuri ili tuwe taifa linaloongozwa na mfalme! Sijui wenzangu mnaonaje?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, nimeipenda makala ya Lula, tofauti na wewe ni ndogo tuu, unapendekeza Kikwete awe mfalme!. Kwa upande wangu, JK ni mfame tayari, ila ufalme wake ni wa miaka 10. Mfalme mkuu wa utawala wa Tanzania, ni mfalme CCM ambaye anatawala/atatawala milele!.

  Mfalme Mkuu CCM ameukasimu ufalme huo kwa mwanachama wake mmoja mmoja kuushikilia ufalme huo kwenye ngwe za miaka kumi kumi. Uchaguzi wa rais tunaoufanya ni kukamilisha tuu taratibu.

  Hata hivyo, natofautiana na wewe kwenye hoja kuwa Mfalme CCM kaona JK ndio bora kuliko wote. Hapana!. Ukweli ni kuwa Mfalme CCM alishatambua kuwa JK sio bora kuliko wote na naamini hata JK mwenyewe ameshatambua kuwa yeye sio bora kuliko wote, ila lazima yeye aendelee kwa sababu huo ndio utaratibu waliojiwekea/pangia katika jukumu zima za Ufalme wa CCM, kuwa mwanaCCM aliyekabidhiwa dhamana ya kukalia kiti cha ufalme, atakikalia kwa miaka kumi mfulululizo, liwake jua, inyeshe mvua!.

  Nasi wananchi wa Tanzania, kwa kauli moja, huwa ndio tunaupitisha utawala wa kifalme kwa kishindo kikubwa ili uendeleze ufalme wake kila baada ya miaka mitano, na ufalme wake hautakuwa na mwisho!.

  Kidumu Chama cha Mapinduzi!
  Kidumu!.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unajua badala ya kumpigia debe awe mgombea pekee kina Makamba waanze kupiga debe kuwa Kikwete awe mfalme. Nina uhakika wana CCM wengi wataandamana kuunga mkono jambo hili kwani kama hakuna mtu wa kuweza kumrithi Kikwete sasa haiwezekani mtu huyo akawepo baada ya miaka 5..
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Na jinsi wanachama wa CCM walivyo bendera fuata upepo, akianza mmoja tu tumekwisha.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  Usinikumbushe maisha ya zamani.
  Nikiwa mdogo nilisoma kitabu cha mfalme ****..
  Yaani kwa ajili ya yeye kupenda makuu, na mambo ambayo hayapo kabisa duniani,,,
  alitaka ashonewe vazi ambalo dunia nzima angekuwa nalo yeye tu...
  Akashonewa nguo ambayo ni invisibo.
  Nguo hiyo haikumsitiri mfalme na akajikuta anatembea uchi.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hahaha! You said it. Kuna wanaCCM ambao wenyewe wanaunga mkono kila kitu. Wakati wengine watakapokuwa wanaandamana kupinga, CCM wataandamana kuunga mkono. Lakini pia kumbuka kwamba wengine hawasemi wanachomaanisha bali ni njaa ndiyo zinawafanya waseme hivyo. Kuna watu wanasema hayo ili mheshimiwa akirudi madarakani next time awakumbuke tena. Kwa hiyo si kwa maslahi ya nchi, bali ni kwa maslahi ya matumbo yao na ya watoto wao.
   
 7. R

  Renegade JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Usinikumbushe kisa cha Mfalme ****.
   
 8. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Comrade MM. Nadhani baada ya kufariki baba wa Taifa, japo tulifikiri hatutapata mwingine tena wa design yake mwenyezi Mungu ametutunuku na Nyerere wengine 7,000. Ulichoandika huyu mtoto wa Nyerere Mheshimiwa JK akikisoma ataelewa nina maana gani. Mchango wako MM kwenye taifa hili ni mwenyezi Mungu tu atakurudishia thawabu zake. Haya mambo ni ya ndani mno.

  JK mimi ni mshabiki wako namba moja, acha hao wanaokushabikia kwa sababu wanataka vyeo. Ebu tafuta audience na JF, watu kama MM na wengineo wakusaidie kimawazo wakati huu. Usidharau kipaji, kipaji ni bora kuliko uprofesa.

  JK natamani sana ushinde mwaka huu na utakapomaliza miaka yako 10 Tanzania ikukumbuke kwa ushujaa wako, yaani uwe umeleta tofauti nchini. JK please mimi kama mshabiki wako nambari moja nakuomba utafute sana audience na JF, jamaa wamejaaliwa na muumba wa ulimwengu.
   
 9. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Linganisha chaguzi za hawa watu wawili, JK kwenye CCM mwaka 2005 na Mbowe kwenye CHADEMA mwaka 2009. Kama ni ufalme ungempa nani?
   
 10. L

  Lukwangule Senior Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa haya ni matusi kwa watu wenye akili. sishabikii.matusi kwa sababu zifuatazo:
  .Huenda ndani ya rangi ya kijani kuna washenzi kama walivyo washenzi katika mambo mengine na hii haifanyi kanuni kufunika ukweli.
  .kama inavyoweza kuwa katika rangi ya bluu pia.
  .Tatizo ni fikra kwani walioanzisha na kutengeneza chama chao bado katiba ni njema na nzuri. na inaweza kufaa kabisa lakini huu mcharuko uliopo sasa usifanye kila kitu kibaya bado CCm yaani kijani wanafaa kuwaongoza watanzania wengine. Kuna ufalsafa mbovu kabisa wa kufikiria uzuri wa kaburi ndani mfupa na mnuko na sidhani kama CCM ni kaburi, ninachoweza kusema kama CCM ni kaburi basi vyama vyote vya siasa ni kaburi vinamapungufu makubwa ya kuwa na uzuri wa nje basi! Watu ndio wanaosema tunataka kutawala na tutatawala hivi! Wanawa Israel (historia), walitaka kutawaliwa na mfalme na nabii akasema haifai mungu tu ndiwe awe mtawala wenu,wakasema sisi hatutaki kuwa tofauti na wengine duniani, tunataka mfalme, jamani mfalme atawatoza kodi, wakasema sawa tu, akawaambia atawachukulia watoto wenu kuwa wake zake na masuria, wakasema sawa tu, haya wakamtawaza sauli... naam ni stori tu. nataka kusema hivi wapo wanaotaka kutawala wanaweza hata kwua madikteta na si lazima watoke CCM wanaweza kutoka CUF chadema TLP na haya kanyanga twende kuna vyama 18 vya kisiasa.Watu waliopo CCM si washenzi ni wasstaarabu lakini bado watakuwepo wapuuzi ambao wanafanya kengele zao kuwa na mlio wa shaba yenye upatu mwenye akili na aelewe mwenye roho ya kwanini anaweza kusawazisha goli
   
 11. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi inanikumbusha "The Pied Piper of Hamelin". Tuko kama vipanya na vitoto tunafuata tu kila wimbo tunaopigiwa.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahaha.. huku watu wanamshangilia wakiimba "amependeza".. isipokuwa katoto kamoja kalikokuwa kapiga kelele "mfalme yuko uchi!"
   
 13. L

  Lukwangule Senior Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningelikuwa namchagua mfalme ningempa Jei kei... kitabu cha maisha yake kipo wazi ...Cha Mbowe mahali fulani hivi kinanipa taabu... shua kinanipa taabu kwelikweli na hapo ndipo ninapowaona waswahili wanamaana na misemo yao waswahili husema... heri zimwi likujualo huwa halikuli ukaishaaaaaaaa. Mhh hii nayo! huu sasa mcharuko mwingine... inahu....? ahh si nimesemaaaa
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kikwete.. au umesahau kuwa alikuwa ni mrithi wa Ufalme wa Tanzania tangu 1995 (wengine wamedai kuwa tangu utoto!) Nakumbuka wakati ule wa kampeni hata watu wakatukumbusha jinsi gani JK naye anatoka familia ya machifu wa kabila dogo la Wakwere.. kwa hiyo damu ya kifalme iko ndani yake.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tanzania mbona wafalme tunao tokea zamani. Tofauti ni kwamba siyo ile traditional monarchy ambayo moja kwa moja mnajua who is next inline to become king. Sisi kwetu we democratically elect our kings.

  Look at it this way mkuu. Tanzania kuna chama kimoja ambacho hata kabla ya uchaguzi moja kwa moja tunajua kitashinda. Familia ambazo zimeongoza basically ni zile zile i.e. the Mwapachus, Karumes, Mwinyis etc. Hizi strong hold families the CCM ni kama extended ukoo ambazo zina shindana tu wenyewe kwa wenyewe nani awe "mfalme". Every once in a while tuna pata political outsiders now ambao wanaingia na wao kuanza kuceate dynasties zao i.e. the Kikwetes etc.

  Personally I don't think it's a bad thing to create a dynasty. Nani kati yetu asiye taka watoto na wajukuu zake wafaidi matundu ya kazi zao? Wafanyabiashara hurisisha watoto wao business empires zao, wanasiasa huruthisha watoto wao nchi. And if you look at it, it's very easy mtoto kufuata nyao za baba kama baba alikua kwenye position nzuri.

  Kama wananchi hawataki wafalme au family dynasties basi kazi kwao. Narejea sentesi yangu ya juu niliyo sema we have democratically elected kings.
   
 16. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kikwete anaweza kuwa mfalme wa bagamoyo, hawezi kuwa mfalme wa tz, sisi wengine hatuwezi kukubali, labda sisi tuwa mfelme wake.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa nini achaguliwe awe mfalme?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  soma sababu zimeainishwa hapo juu.
   
 19. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mimi nina uhakika chaguo la Mungu limejazwa nguvu za roho na hivyo hawezi kuogopa mtu wala kundi lolote, after all ni mkuu wa kaya at the moment.

  Si aje tu hapa JF, watu tufanye naye charting!!!
  Hivi ule utaratibu wa kujibu maswali live umeeisha!!!
   
 20. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Labda awe mfalme wa bagamoyo nyumbani kwao!
   
Loading...