Kuna ubaya nchi ikichapisha pesa kwaajili ya matumizi yake?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,885
Tanzania has long had plans to issue an inaugural sovereign Eurobond and was held back by the lack of a credit rating. It obtained a B1 assessment, the fourth-highest non-investment-grade reading, from Moody’s Investors Service in March 2018.

In September, the central bank rejected claims it printed notes valued at 1.5 trillion shillings ($653 million) for government use.
 
Nafikiri pesa yoyote lazima itokane na uzalishaji, nje ya hapo ni kuua uchumi, hii tuliona kule Uganda wakati wa Amin alipomwamuru waziri wa fedha kuwa azina ichapishe fedha kwa kuwa serikali haikuwa na fedha.

Lkn pale ambapo serikali haiwezi kukopa kwa sababu hii au ile na makusanyo ya kodi pia ni haba waga wanaishiwa ujanja na kujikuta wanachapisha fedha kama ilivyotokea Zimbabwe, Venezuela nk na matokeo yake ni "Hyperinflation" na uchumi kuporomoka kabisa.

Hii hali ndio inayotunyemelea Tanzania kwani kwa sababu ya Economic Mismanagement makusanyo ya kodi ya serikali yameporomoka na serikali haiwezi kukopeshwa na wakopeshaji mbali mbali kwa sababu kadhaa wa kadha.

Rais John Magufuli alivyoukwaa urais alifikiri akihodhi kila sector angeweza kufanya miujiza na kuufanya uchumi upae ili apate sifa lkn hakujuwa kuwa uendeshaji wa uchumi ni "Different Ball Game with its own cardinal principles".

Sasa kujifanya mjuaji na mtemi kutaiua hii nchi na kuupelekea uchumi wetu kuwa " Basket Case" kama Zimbabwe au Venezuela. Yeye alipashwa abaki na mambo ya utawala tu na uchumi angewaachia wenyewe kwani hapo yeye apende asipende ni "Layman" tu kama wengine.
 
DEFINITION of B1/B+
B1/B+ is one of several non-investment grade ratings (also known as "junk") that may be assigned to a company, fixed-income security or floating-rate loan. This rating signifies that the issuer is relatively risky, with a higher than average chance of default.

Investment grade refers to the quality of a company's credit. In order to be considered an investment grade issue, the company must be rated at 'BBB' or higher by Standard and Poor's or Moody's. Anything below this 'BBB' rating is considered non-investment grade. If the company or bond is rated 'BB' or lower it is known as junk grade, in which case the probability that the company will repay its issued debt is deemed to be speculative.

Source: Investopedia
 
Bidhaa zitapanda bei sana
Thamani ya pesa yetu itashuka mno
Itakuwa vigumu sana kulipa madeni ya nje
Itakuwa gharama sana ku-import bidhaa kutoka nje
 
Tanzania has long had plans to issue an inaugural sovereign Eurobond and was held back by the lack of a credit rating. It obtained a B1 assessment, the fourth-highest non-investment-grade reading, from Moody’s Investors Service in March 2018.

In September, the central bank rejected claims it printed notes valued at 1.5 trillion shillings ($653 million) for government use.
Pesa haichapishwi kiholela, waulize Zimbabwe.
 
Umeshawahi kufika kwenye sherehe ya watu hamsini halafu kikapikwa chakula cha watu 1000? Ukichapisha minoti bila kuzingatia ratio za kiuchumi thamani ya Ile pesa kwa wananchi wa ndani na nje itafanana na chakula kilichobaki baada ya watu kushiba. Watakula mpaka Mbwa na watakiacha maana kipo tu.
 
Mleta mada akili huna kabisa.
Robert Mugabe pamoja na ubabe wake wote hajawahi kutengeneza hela zake.
Sasa kwako wewe unajua ni kitu kidogo sana, hapo ndipo mnapomtia jeuri huyo dictator wenu.
Ajaribu aone, ndio utajua kwanini hata Marekani hawatengenezi hela zao?
 
Nilikuwa nachokoza tu mada braza. Marekani wanachapisha fedha kwa fujo sana sema kwasababu dollar inatumika dunia yote basi hawapati inflation bali nchi zingine ndiyo huathirika(wana export inflation).
 
Tanzania has long had plans to issue an inaugural sovereign Eurobond and was held back by the lack of a credit rating. It obtained a B1 assessment, the fourth-highest non-investment-grade reading, from Moody’s Investors Service in March 2018.

In September, the central bank rejected claims it printed notes valued at 1.5 trillion shillings ($653 million) for government use.
Swali juuu ya Swali
Unaweza ukajiongezea aridhi katika hiii Dunia
 
Hakuna ubaya kuprint na kuingiza kwenye mzunguko, ni one of economic tool kustabilize economy . Ila ubaya unakuja unapoprint wakati una hali mbaya ya uchumi. Muulize Mzee Mugabe atakuwa case study
 
Labda wainject fedha kwenye uchumi kama kutia misaada na zawadi mbalimbali kuwapongeza wananchi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom