Kuna ubaya kujitambulisha kwa kabila la mama?

faru joni

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
478
733
Habarini wana jamvi

Kuna ubaya wowote kuandikisha au kujitambulisha sehemu kwa kabila la mama ukiachana na la baba (namaanisha la baba ukalitupilia mbali)

Karibuni kwa mitazamo!!
 
Duh!, labda kama mother aliolewa na wewe ukiwa (yaani sio mtoto halali wa baba)

Siku zote kabira la baba ndio mpango mzima... kabira ya mama sio kabira yako.
 
Naona watoto weengi waliozaliwa baadaye na mama kumpata baba mwingine ndiyo uamua kulowea kwa mama, maana babako alikufa au hakuwa na mahusiano mazuri na mamako ndipo mama akakutaifisha na kukupeleka ujombani.

Siyo sahihi kujitambulisha kwa kabila la mamako, dunia haikupewa usawa huo.
 
Sisi tunatumia kabila la mama.. baba yangu hakuwahi kufahamu kabila lake, mama yake alifariki muda mfupi baada ya kujifungua na mtoto alichukuliwa na masista. Baba alitusimulia masista walimkuta bibi njiani akiwa ameumwa na nyoka. Wakamkimbiza hospital hakukua na taarifa zaidi.
 
Siyo kawaida acha kudanganya watu, hii hutumika kwa special case tu ndipo mtoto utumia hata ubini wa mama. Narudia ni kwa special case tu, huwezi kuwa upande wa mama hivi hivi tu wakati mama yako mwenyewe anatumia jina la mume wake.
Sasa mi ndo najiita mmakua
Mi sioni kama ina mata sana
 
Habarini wana jamvi
Kuna ubaya wowote kuandikisha au kujitambulisha sehemu kwa kabila la mama ukiachana na la baba (namaanisha la baba ukalitupilia mbali)
Karibuni kwa mitazamo!!
Mkuu kama utaratibu au mila za ukoo wenu zinataka ujitambulishe kwa kabila la mama itabidi iwe hivyo ila kama haziruhusu jitambulishe kama inavyotakiwa hata kama unachukia kabila la baba, Kuna hatari kubwa sana katika kukiuka misingi ya kimila
 
Duh!, labda kama mother aliolewa na wewe ukiwa (yaani sio mtoto halali wa baba)

Siku zote kabira la baba ndio mpango mzima... kabira ya mama sio kabira yako.
Unajuaje kama hiyo mimba imiyokuzaa Wewe ni ya Huyo"Baba" anayekutunza?
Lakini Mama uliishi tumboni mwake.
Kuitwa ubin wa Mama ni Sawa kabisa.
Kama huamini kapime DNA na huyo Baba.
 
Rafiki yangu baba alikuwa Mhaya mama Mchaga, sikuzote alisema yeye Mchaga. Hata. Hata surname ya kihaya aliiona si alitumia jina la baba yake la kanisani.
 
Naona watoto weengi waliozaliwa baadaye na mama kumpata baba mwingine ndiyo uamua kulowea kwa mama, maana babako alikufa au hakuwa na mahusiano mazuri na mamako ndipo mama akakutaifisha na kukupeleka ujombani.

Siyo sahihi kujitambulisha kwa kabila la mamako, dunia haikupewa usawa huo.
Kwani sio sahihi , wazazi wote si wamechangia damu ? Nani anatoa usawa ?
 
Kunatatzo lolote kutumia kabila mama?? Watu wengi watanga hutumia makabila ya mama zetu sababu wengi hawajui kabila zababa zao
 
Back
Top Bottom