mzaramo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2006
- 6,371
- 5,174
- Thread starter
- #21
Kama hivyo ndivyo ilivyo basi tambua haya:
- Muungao haukuletwa na Chama cha Mapinduzi au Kijani kibichi as on your words (1964 ASP ndiyo iliridhia huko visiwani kwa kuona manufaa ya Kuunganisha nchi.
- ASP imekuwepo Visiwani kama chama Tawala, Chini ya Serikali huru ya Mapinduzi ya Zaanzibar mpaka 1977 iliporidhia tena kuungana na TANU kwa bara ili kupata Chama kimoja ambacho kwa heshima ya kuendelea kuyaenzi kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi kwa huko Zanzibar chama mpaka hivi sasa kinaitwa "CHAMA CHA MAPINDUZI"
- Muungano haujaiondolea Zanzibar maamuzi ya kiserikali na utawala na wala hakuna popote hilo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Labda tuseme imeondoa mamlaka ya kuwa na Serikali ya Tanganyika na Taifa la Tangayika).
- Yale ambayo yanatajwa kwenye "Artcles of Union" na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuwa ni mambo ya Muungano ni yale ambayo ASP iliyaona yanastahili kuwa hivyo na kuyaweka chini ya mashirikinao ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri (hakukuwa na shinikizo lolote).
- Uzanzibar upo na utaendelea kuwepo Kikatiba kwa maana ya kuwepo kwa Mkoa huru na Serikali huru ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata hivyo, kwa kuwa Uzanzibar kama ulivyo "Uchaga", Unyamwezi, nk sio "Urai" kwa mujibu wa "Mambo ya Muungano, huwezi kutambulika hivyo kimataifa kuwa "WEWE NI MZANZIBARI" bali ni "MTANZANIA MWENYE ASILI YA ZANZIBARI"....
Btw hizo the so called ARTICLES of UNION mmezificha wapi?
nakumbuka kuna jamaa walienda Mahakamani kuzidai halafu JIIIIIII!!!!!