Kuna Ubaya Gani Kwa Kikwete Kuitwa Kanali Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna Ubaya Gani Kwa Kikwete Kuitwa Kanali Kikwete?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Feb 2, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Maafisa wa jeshi huwa wanatunza sana vyeo vyao vya kijeshi kuliko title nyingine yoyote; kwa mfano, General David Patreas ana BS. MPA na Ph.D. na aliwahi kuwa professor kabla ya kurudi kwenye active duty, lakini anajulikana kama General Patreas wala siyo Dr. Patreas, General Dr. Patreas, Professor Patreas, General Dr,. Prof Patreas au upuuzi wowote wa namna hivo. Maraisi wengi waliopata madaraka wakitokea jeshini waliendelea kutumia vyeo vyao vya kijeshi, kwa mfano Flt Lt Jerry Lawlings, Col Qadaffi, General Roosevelt, General Amin, General Babangida n.k. Najua Tanzania kuna maafisa wa jeshi wengi walioamia kwenye siasa lakini nao wakatunza vyeyo vyao vya kijeshi:; kwa mfano, Kapteni Mkuchika, Kapteni Chiligati, Kanali Tarimo, Kanali Mjengwa General Said kalembo, na wengineo wengi tu.

  Linalonishangaza ni kwa nini Kikwete haitwi Kanali Kikwete? wakati alikuwa Kanali wa jeshi; je anadharau hiyo title ya kanali? Tangu atunukiwe udakitari wa heshima, amekuwa anajitambulisha kwa huo udakitari wa heshima kuliko hadhi yake kamili ya uafisa wa jeshi, kuna tatizo gani na ukanali?

  Just curious.
   
 2. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  inakua imekaa ki dictecta zaidi labda ndio maana anakwepa
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ma-kanali huwa hawaanguki-anguki ovyo
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kichuguu:

  U-Kanali wake ulivyopatikana ni sawa sawa na U-Dokta wake ulivyopatikana! Kwahiyo yeye amependelea U-Dokta. Ukiangalia tangia akiwa Nachingwea, Tabora, Zanzibar, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Balozi Mambo ya Nje e.t.c hajawahi kuitwa kwa "Title" ya "Col."
   
 5. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  mi naona ni mazoea tu ambayo labda ni yeye au watu wamekuwa wakimrefer kama dr na sio colonel.kwa wenzetu hizi degree za heshima huwa hawapendelei sana kuzitumia kujitambulisha lakini huku ni tofauti.na hili la ukanali ,sina kumbukumbu ya kikwete kuwa full colonel najua aliishia kwenye luteni kanali
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Acha aitwe vyovyote anavyotaka lakini tumemchoka. Sidhani kama kuongeza kanali kwenye jina lake kutabadilisha chochote zaidi ya kumfanya aonekane dikteta zaidi
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hawezi kujiita yeye mwenyewe. Hakuwahi kukikana cheo hicho. Makamba naye ni Luteni!
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280

  Sahihisho kwenye Red isomeke Rawlings.

  Kuhusu Jakaya, ukanali wake ni kama huo huo udaktari wa kupewa. Alikaa TMA Monduli kwa mkono wa siasa zaidi kuliko taaluma ya jeshi.
   
 9. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  muite tu hata wewe ataitika...
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kumbuka enzi za mwalimu alikuwa anawapika vijana kuwa wanasiasa kupitia jeshini na wakitoka huko enzi za chama kimoja walitakiwa kutofungamana na jeshi kwa namna yoyote tena wala kutumia hadhi za kijeshi. Baadaye kidogo masharti haya yalilegezwa hasa wakati mfumo wa vyama vingi ambapo baadhi ya wananchi walikuwa hawalazimiki kupitia jeshini ili kuwa wanasiasa.
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bado kidogo atatunukiwa Uprofesor!
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Suala la Kikwete kutangazwa sana kwa hadhi ya Dr wa kulaumiwa sio kikwete bali ni waandishi wa habari. Hakuna mahali popote tunapoweza kuambiwa kuwa kikwete aliitisha press conference kwamba kapata PHD ya heshima hivyo aanze kuitwa kwa hadi hiyo.

  Kuna jamaa mmoja yuko Ikulu anasema hata katika sahihi zake hata siku moja hajawahi kujitambulisha kama Dr katika nyaraka mbalimbali. Waandishi wa habari wasituzingue tu mbona hata Mkapa, Mwinyi na wengine walipata PHD za heshima? Tuwaulize waandishi wa habari watakuwa na majibu.
   
 13. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kikwete hakustaafu Jeshi bali aliacha na kuingia kwenye siasa...sijui tararibu za kijeshi zinazungumzaje hili na wakati aliacha alifikia rank ya Luteni Kanali sio Kanali!
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Who knows????????????? unaweza kuwa ni kete ya kisiasa kutaka kuonyesha kwamba Rais anapenda kuitwa Dr kumbe pia ni kutaka kumchafua kupitia heshima hiyo.

  Jamani tuwe macho sio kwamba kila jambo linatangazwa kwa nia njema!!!!!!!!!!!!!!!

  hata katika mikutano ya kimataifa wala makongamano sijawahi kusikia kikwete akitambulishwa kama Dr kulikoni na vyombo vya habari? kulikoni Dr inatumika tu kwenye vyombo vya habari.
   
 15. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  aaaah! hii forum..... Mkuu umenichekesha sana. :coffee:
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hivi hamjagundua kwamba, hata ile Idara ya mawasiliano ya Ikulu chini ya Salva Rweyemamu haijawahi kusema na waandishi wa habari kwa kumtambulisha au kuanza jina la rais na Dr Kikwete au Kanali Kikwete? Lakini wao waandishi wakitoka pale wanakwenda kuandika Dr kikwete!!!!!!!!!!!!
   
 17. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe kuwa aitwe vyovyote vile lakini kama leadership ability ni bila bila forget about titles.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hata katika elimu mtu hutambuliwa kwa nafasi ya heshima ya juu, kwa mfano Professor huwezi kumwita Dk, hata kama huko nyuma alikuwa anaitwa Dk. katika ngazi ya Rais sio lazima kumtambua kama kanali au Dk wakati nafasi yake ya heshima ya juu zaidi na yenye mamlaka ya juu ni ya Urais. Kwa wale wataomwita kwa nafasi nyingine ni kwa sababu wamependa wao. Mtu mmoja kumwita Rais, Dk, Kanali, sheikh au Padre kama angekuwa Dr Slaa sio vyema ni usumbufu kwa wasomaji. Utadhani unaandika CV
   
 19. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #19
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ili iweje akijiita kanali ataacha ufisadi au?kwanza mtu mwenyewe mlaini tuu hawezi kuwa mwanajeshi na yeye mwenyewe anaona aibu kutumia hiyo title
   
Loading...