Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,627
- 154,986
Mwanangu kamaliza form six, hakupata chuo mwaka huu, hivyo namfanyia mipango aende masomoni India akasomee degree ya graphic designing.
Nimegundua kuwa ana mapenzi ya dhati kwa binti yetu wa kazi, naye binti wa kazi anampenda kijana wangu kwa dhati.
Je zaidi ya mimba kuna athari gani nyingine?
Sijamwambia mume wangu kuwa nimegundua mahusiano hayo, ila nilikaa na huyo msichana, akasema anampenda mwanangu na wamesha kubaliana kuoana baada ya kijana kutoka masomoni India.
Nimeongea na kijana, anasema anampenda sana binti huyu wa kazi, na yuko tayari kuoa hata kesho, ili akienda India aache mke nyumbani.
Naombeni ushauri wenu.