Kuna ubaya gani House girl akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanao?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,077
2,000
Mwanangu kamaliza form six, hakupata chuo mwaka huu, hivyo namfanyia mipango aende masomoni India akasomee degree ya graphic designing.
Nimegundua kuwa ana mapenzi ya dhati kwa binti yetu wa kazi, naye binti wa kazi anampenda kijana wangu kwa dhati.
Je zaidi ya mimba kuna athari gani nyingine?
Sijamwambia mume wangu kuwa nimegundua mahusiano hayo, ila nilikaa na huyo msichana, akasema anampenda mwanangu na wamesha kubaliana kuoana baada ya kijana kutoka masomoni India.
Nimeongea na kijana, anasema anampenda sana binti huyu wa kazi, na yuko tayari kuoa hata kesho, ili akienda India aache mke nyumbani.
Naombeni ushauri wenu.
 
Fixed Point

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
11,309
1,225
mimi pia sioni kama kuna ubaya
ila sikushauri waoane kabla mwanao hajaenda shule.......
hao watoto bado ni wadogo, na kwa huyo kijana wako huko anakoenda atakutana na mengi tu, mwache aende akiwa free, akirudi kwa huyo binti basi kweli itakuwa alikuwa chaguo lake.
na pia msije mkampotezea mwelekeo binti wa watu, akaolewa halafu kijana akapata dada mwingine huko wakapagawishana halafu binti wa watu akaachwa solemba.
hayo mambo ya kuahidiana kuoana yapo hata kwa mahusiano ya watoto wa primary, kwa hiyo kuahidiana kuoana haimaanishi wanapendana kihiiiivyoooo na kweli wataoana.
kama ulishaongea na watoto basi ni vizuri husband pia ukamwambia....... siyo vizuri asikie toka kwa mtu mwingine
 
Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,597
2,000
Worry not...let the boy go to India, kuna vingi vya kuexplore kule, am sure atarudi akiwa na mtazamo tofauti!
Ila kuna kitu cha hatari nakihisi hapo, inawezekana mnamfungia sana huyo mtoto wa kiume mpaka anaona ndio kafika hapo na hakuna cha kuexplore huko nje...si tabia nzuri kufungia watoto, hasa wa kiume!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
Nina wasiwasi na aina ya malezi uliyompa mwanao. Anataka kuoa akuachie mke aende masomoni? Ulishamfundisha uwajibikaji kweli? Akienda shule, mkewe anakuwa hgeli wa bure unampa maintainance allowance au vipi?

Kitu kingine ni discipline. Mtu yeyote aliye na discipline, atahakikisha hatamani visivyotamanika. Hgeli ni dada, anapaswa kuwa kama mlezi na muangalizi wa familia. Kwa mwanao kutembea n hgeli haina tofauti na boss kutoka na secretary wake. Mnaweza kuja kudhurika bila kujijua. Najipatia picha nidhamu niliyokuwa ninayo wakati nakua, both kwa houseboy, mlinzi na housegalo. Kumbe ningeweza kuolewa na yule houseboy? Hapana, alikuwa kaka na aliweza kunisaidia hata maujanja ya kitaa.
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
Mwanangu kamaliza form six, hakupata chuo mwaka huu, hivyo namfanyia mipango aende masomoni India akasomee degree ya graphic designing.
Nimegundua kuwa ana mapenzi ya dhati kwa binti yetu wa kazi, naye binti wa kazi anampenda kijana wangu kwa dhati.
Je zaidi ya mimba kuna athari gani nyingine?
Sijamwambia mume wangu kuwa nimegundua mahusiano hayo, ila nilikaa na huyo msichana, akasema anampenda mwanangu na wamesha kubaliana kuoana baada ya kijana kutoka masomoni India.
Nimeongea na kijana, anasema anampenda sana binti huyu wa kazi, na yuko tayari kuoa hata kesho, ili akienda India aache mke nyumbani.
Naombeni ushauri wenu.

nadhan hao wanamalizana hamu tu HAPO
 
Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,651
2,000
Umri alionao ni mdogo(nimefikiria umri wa wastani kwa wanaomaliza kidato cha sita) sana kufikia maamuzi ya kuoa.
Mwanao bado ana maisha marefu sana mbele yake, na sote tunajua KUOA ama KUOLEWA ni mpoja ya hatua katika safari ya maisha ya mwanadamu.
Si uamuzi ambao unapaswa kufanywa kwa pupa, ninahisi jambo moja ndio limemchanganya sana kijana wako nalo ni matunzo aliyokuwa akipewa na House maid kama kupikiwa, kufuliwa nguo n.k n.k na bila shaka kwake hayo mambo yalikuwa ni mageni pengine kasoma shule ya bweni na ni wanaume tu
 
Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
559
0
Mwanangu kamaliza form six, hakupata chuo mwaka huu, hivyo namfanyia mipango aende masomoni India akasomee degree ya graphic designing.
Nimegundua kuwa ana mapenzi ya dhati kwa binti yetu wa kazi, naye binti wa kazi anampenda kijana wangu kwa dhati.
Je zaidi ya mimba kuna athari gani nyingine?
Sijamwambia mume wangu kuwa nimegundua mahusiano hayo, ila nilikaa na huyo msichana, akasema anampenda mwanangu na wamesha kubaliana kuoana baada ya kijana kutoka masomoni India.
Nimeongea na kijana, anasema anampenda sana binti huyu wa kazi, na yuko tayari kuoa hata kesho, ili akienda India aache mke nyumbani.
Naombeni ushauri wenu.
Huyu mwanao pamoja na house girl kila mmoja ana umri gani?????? Ndoa sio rahisi hivyo remember!!!!!!!
 
Tamatheo

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,302
2,000
Mwanangu kamaliza form six, hakupata chuo mwaka huu, hivyo namfanyia mipango aende masomoni India akasomee degree ya graphic designing.
Nimegundua kuwa ana mapenzi ya dhati kwa binti yetu wa kazi, naye binti wa kazi anampenda kijana wangu kwa dhati.
Je zaidi ya mimba kuna athari gani nyingine?
Sijamwambia mume wangu kuwa nimegundua mahusiano hayo, ila nilikaa na huyo msichana, akasema anampenda mwanangu na wamesha kubaliana kuoana baada ya kijana kutoka masomoni India.
Nimeongea na kijana, anasema anampenda sana binti huyu wa kazi, na yuko tayari kuoa hata kesho, ili akienda India aache mke nyumbani.
Naombeni ushauri wenu.

Yaani kweli bila kupepesa macho (neno la vijana) una kijana amemaliza kidato cha sita bado hujui adhari za kujamiiana tofauti na MIMBA, hivi kweli yale malezi ya vijana kabla ya ndoa yapo tena? Kwa heshima na taadhima naomba kuongeza madhara mengine 1. Kijana wako akirudi masomoni kuna uwezekano mkubwa wa kumwacha huyo HG wakati wewe umeshakubali USHENGA, binti atakuona wewe na mwanao ni maadui zake...tafakari 2. Magonjwa ya Zinaa na Ukimwi, kabla hawajaanza mahusiano hawakuomba ridhaa kwako kwani hata wewe hukujua dhara hili 3. Huyo binti amejihisi salama kwani anatoka kwenye HG na kuwa MKWE hivyo uanze kutafuta HG mwingine 3. Ngono katika umri mdogo zinaaribu saikolojia za wahusika kwani mapenzi yanachukua kila kitu katika binadamu hivyo naweza kukudhibitishia kwamba kutokupata matokeo mazuri ya kidato cha sita kwa mwanao kumesababishwa na huyo HG ambaye sasa ni MKWEO wa sirini......USHAURI..kwa mtazamo wangu hawa wanatamaniana na wala sio kupendana na ndio maana mwanao anajigamba anaweza kumwoa hata sasa huku akiwa hajui kesho yake na kwa wewe kuingilia kati katika hali ya kuuliza na sio kukemea na kukaripia kumewaongeze hatua katika tamaa zao, hivyo basi mwambie mzazi mwenzie bila kuhusisha mazungumzo baina yako na wao na pia bila kutetea lolote kisha kwa kuunganisha mawazo mumpe malezi bora huyu kijana wenu, kidato cha sita cha watoto wetu wanaosoma wadogo ni umri wa kumalizia balehe na kuvunja ungo hivyo msifikiri hapo kuna wapenzi siku watawaumbua mtaanza kutoa viapo na laana kwa mwanenu...Sorry nimejisahau kwa ujumbe mrefu ila waweza niPM nikupe matokeo na hasara....USIDANGANYIKE NA WATOTO
 
Mkora

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
370
225
ndio shida ya watoto wa kiume hapo unaweza kukuta nyumba nzima wanamzunguka hg kila mtu kwa wakati wake:glasses-nerdy:

Mkuu hiyo kweli tupo maana nakumbuka enzi ya enzi kila mtu kwa muda wake hadi mshua akatia mkwala kuleta House boy haya na huyo mumle tigo tuone
 
MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,812
2,000
Hakuna tatizo lakini fikiri haya

-Huyo anaenda kusoma anakuachia ulezi maana lazima umweke kama mtoto wa nyumba.
-Utakuwa na kazi ya kulinda maana lazima ajijue kuwa ni mke wa mtu
-Na huko mwanao anenda unahakika gani kama hatabadilisha mtizamo.

Nionavyo mimi huweiz pinga mapenzi yao lakini mambo ya ndoa yaache ya baadae aende kusoma arudi ajitegemee ndio aoe, asije mfunga kwenye ndoa huyo binti kunako atakapobadilika mbel. Na muulize huyo Bidada anaweza subiri muda wote huo?
 
Tamatheo

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,302
2,000
Nina wasiwasi na aina ya malezi uliyompa mwanao. Anataka kuoa akuachie mke aende masomoni? Ulishamfundisha uwajibikaji kweli? Akienda shule, mkewe anakuwa hgeli wa bure unampa maintainance allowance au vipi?

Kitu kingine ni discipline. Mtu yeyote aliye na discipline, atahakikisha hatamani visivyotamanika. Hgeli ni dada, anapaswa kuwa kama mlezi na muangalizi wa familia. Kwa mwanao kutembea n hgeli haina tofauti na boss kutoka na secretary wake. Mnaweza kuja kudhurika bila kujijua. Najipatia picha nidhamu niliyokuwa ninayo wakati nakua, both kwa houseboy, mlinzi na housegalo. Kumbe ningeweza kuolewa na yule houseboy? Hapana, alikuwa kaka na aliweza kunisaidia hata maujanja ya kitaa.

Pamoja na kukosa kitufe la like ila chukua LIKE, hapo ni tamaa na matamanio kama mama tambua mwanao ndio kwaanza ameiiba dunia ya mapenzi, kemea na kuonya sio kuwa MSHENGA
 
Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,946
2,000
Mambo hayo, mimi sitii neno, nawaachia makungwi na manyakanga walonge wao.
Allah msikh
 
Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
0
mama akikosa hekima nyumba itayumba.
Je unaiona nyumba yako ni nyumba imara?
Hebu hili jambo kajadilianeni na mumeo kabla ya kutaka mawazo yetu
 
gobore

JF-Expert Member
Aug 17, 2009
717
195
Hahaaa sipatii picha eti mke wangu ndo anakuja kuniambia Baba nanihii mwanao anataka amuoe HG ndo aende kusoma! Ntawakimbiza wewe pamoja na huyo mtoto na HG/MKE wenu.......

-Hao ni watoto bado oa hiyo ni fling tu na huwa hatuoi kwasababu ya flings, muache akakutane na wasichana wengine uone kama hatabadili msimamo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom