Kuna ubaya/faida gani kuwaongoza watu wanaokuzidi mshahara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ubaya/faida gani kuwaongoza watu wanaokuzidi mshahara?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miruko, May 15, 2011.

 1. M

  Miruko Senior Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kujiuliza sikupata majibu, nikaona nilete hapa jamvini. Hivi kuna tatizo gani kwa kiongozi kwenye chama au taasisi fulani kuongoza watu wanaomzidi mshahara?

  Mfano, uwe waziri lakini mshahara wako uko chini ukilinganisha na mishahara aya watu unaowaongoza? Au uwe rais lakini mawaziri, makabu wakuu na wakuu wa mikoa wanakuzidi mshahara?

  Au kama baadhi ya watu wanavyotaka sasa, kuwa Katibu Mkuu wa CDM Dk. Slaa aongoze chama ambacho watendaji wake wengi ni wabunge wenye mshahara zaidi yake?
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  kwa ufupi uwezo.wa.kuchambua issues wa nape ni mdogo sana badala ya kueleza umma. Ccm ina mkati gani wa kupunguza umaskini yeye anpiga porojo.za tofauti.ya mshahari ni.lazima.ccm.imwondoe.huyu haraka sana
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakuna tatizo hata kidogo na wala hoja siyo hiyo. Hoja hapa ni kauli ya Dr. Slaa kuhusu mishahara ya wabunge wakati ule yeye mwenyewe akiwa mbunge. Kinachosemwa na Nape na pengine wale wanaomuunga mkono ni kwamba, Dr. (Phd) alikuwa akipigia kelele wabunge na pengine watumishi wa umma kujilipa mishahara mikubwa wakati nchi hii ina matatizo lukuki yanayohitaji fedha. Kwa kupokea mshahara unaofanana na wabunge, tena wakati yeye si mbunge siyo unafiki? Mijadala inayuhusu jambo hili ilipaswa kujikita katika kujibu swali hili.
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Kwa maana hiyo unataka kuhalalisha kwamba wabunge ndio wanaostahili kulipwa zaidi? Wabunge si tu kwamba ni wawakilishi wa wananchi bali pia watumishi wa umma hivyo mishahara yao inatakiwa iendane na wananchi wa kawaida waliowachagua na si kujiweka katika "ufalme" fulani. Slaa kwa nafasi aliyo nayo ulimpigia kura?
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usiniulize mimi. Mimi nimefafanua yanayozungumzwa na sasa ni juu ya wewe, mimi na wengine kujiuliza kama matamko ya Dr. (Phd) kuhusu mishahara mikubwa na yeye kupokea mshahara mkubwa ni unafiki au la. Mimi sijatoa fikra zangu kuhusu hili, usiniwambe msalabani!
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Vizuri. Kama ni hivyo, nimejiridhisha kwamba matamko ya Dr. Slaa si unafiki bali anastahili kulipwa anavyolipwa. Na hata mwajiri wake akiamua anaweza kumlipa zaidi, kumpunguzia, au hata kumfukuza kazi kutokana na output yake au sababu nyingine yoyote itakayomridhisha mwajiri.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hayo ni maoni yako na conclusion yako siyo andiko takatifu. Wenzio wengi watasema vinginevyo na kwa hakika onus iko kwa Dr (Phd) kuthibitisha kwamba ama alikosea kusema vile alivyosema au alichofanya ni unafiki.
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Chadema ambaye ndiye mwajiri wa Dr. Slaa wameshafafanua na kufafanua juu ya jambo hilo. Hata magazeti ya juzi Alhamis/Ijumaa yaliandika kwa ufasaha juu ya hilo. Kwa kuwa baadhi yetu hatutaki tu kuelewa, hatutakaa tuelewe. After all siyo responsibility ya Dr. Slaa kujibu hoja hiyo ya ki-magamba. Kamuulize mwajiri wake na kwa bahati nzuri halazagi viporo, alishajibu. Otherwise, hii ni hoja isiyo na mashiko.
   
 9. A

  Analytical Senior Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani kwa kazi anayoifanya Dk Slaa nadhani hata nagelipwa mara mbili zaidi ya hapo ni sawa tu. Wabunge ukiancha mshahara wao wanamarupurupu mengine kibao, mikopo ya magari na kadhalika ambayo mtu kama Slaa hiyo fursa hana. Kipindi kile anakataa alikuwa na hizo fursa zote.

  Hata hivyo Slaa analipwa na CHADEMA (pesa za CHADEMA ambayo hata ukiipigia kelele ruzuku yao haiwezi kupungua hapo), tofauti na wabunge wanaolipwa na serikali. Labda utueleze nyie CCM ambao hata hamtaki kutangaza mishara yenu, hiyo Ruzuku mmewafanyia nini wananchi zaidi ya kofia na kanga na kuwasomba na malori kwenda kwenye mikutano?

  CHADEMA ni kama taasisi, na moja ya mikakati ya taasisi yoyote makini ni kuwalipa maCEO wake vizuri ili wafanye kazi yao pasipo njaa njaa na kuanza kujiingiza na mitego ya rushwa, that is what CHADEMA is doing. Ndio maana unamwona Dr Slaa all the times yuko motivated kuendelea kuwafukua mafisadi nchi nzima kokote waliko. Yaani chama chake kinamuwezesha. CHAMA CHA MAGAMBA (CCM) watakoma.
   
Loading...