Kuna tofauti kubwa kati ya wanaohama CCM na Wanamia UPINZANI

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,697
Hii nilianza kuifuatilia siku Shi.bud anahamia chadema.
Aliongea mambo mengi misemo mingi na kila Aina ya kejeli za kisiasa lkn hakusema Siri yoyote au baya lolote lenye kuivua CCM nguo mbele ya wananchi.
Trend ni hiyohiyo kwa LWS, S.umaye, Ny.alandu, ...n.k
Hutasikia Huwa tunaiba hivi kura (kama ni ukweli), mwenyekiti aliiba hiki, au tuliwahi kufanya vituko hivi, au ukitaka kuwamaliza CCM Fanya A,B na C.

Ila wenzangu na Mimi wapinzani wakihama chochote anachokijua utakisikia (sisi wananzengo huku Huwa hatujui kama ni ukweli au la).
Utasikia mwenyekiti anafuja pesa, sharti uolewe ndio upate viti maalumu, ooh kule Huwa hatpendani wote, na kila lolote la aibu , la kukera, na kuudhi.

Kuna haja ya kuungwanika ktk mambo ya kisiasa. Hata kama mkeo ni kikojozi mkiachana ukikojozi wake sio sehemu ya ubora wako.


Nawaza kisiasa kidogo..
 
Jingine ni kwamba wanaotoka ccm wanaamua kwa hiari yao baada ya kuona mambo yanayumba kwenye chama hicho, lakini wanaotoka upinzani wanajikomba ili wapate vyeo, na wanaona wasipofanya hivyo wataonekana kuwa mamluki. Halafu wanao kwenda ccm wengi wanashawishiwa kupewa vyeo e.g d kafulila p. Katambi j. Shonza k. Mkumbo a. Mugwira n.k.
 
Ukihama ccm umehama chama dola, ukiongea ya ndani lazima yakukute ya Lissu. Lakini ukihama upinzani kwenda ccm kuropoka ndio kunakupa cheo na namna ya kumpanga mwenyekiti wa ccm akupe namba kwenye timu yake ni siasa za majitaka.
 
Tatizo ni Objective. Kuhama toka CCM kunaleta na uamuzi na utashi wa anayehama.
Kuhama CHADEMA ni mkakati wa CCM kuiua CHADEMA, ndio maana sababu za wanaohama chama ni "Mabaya" ya Mbowe dhidi ya "Mazuri" ya Magufuli.

Nakuhakikishia mwaka 2020 kura za maoni ndani ya CCM zitawatema hawa wasaliti na wanunuliwa wote.

Muda utaongea!
 
NASEMA HIVI NA NIMEKUWA NIKISEMA, AKIREJEA TUNDU LISSU KUTOKA KUTIBIWA CHADEMA ITAKUWA NA NGUVU AMBAZO HAIJAWAHI KUWA NAZO,NA AKIRUDI SAFARI HII LITUMIKE GURUNETI MAANA RISASI ZITAKUWA ZIMEPOTEZA UMAANA.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom