Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 10,656
- 21,081
"Kitwanga umemuacha mke wako, umeenda kwa mwanamke mweupe," alisikika mzee baba akimwambia aliyewahi kuwa waziri kwa kukaa pembeni ya mama mmoja mwenye rangi ang'avu. Kwa jamii iliyostaarabika utani wa namna hii unavuka mipaka. Kitwanga alidhalilishwa na yule mama alivunjiwa heshima.
Aghalabu utani wa mzee baba unavuka mipaka hasa akihusisha wanawake.Hii tabia inabidi ikome.
Aidha kuhoji kwa mzee baba hasa akiwa anahoji watendaji mbele ya wananchi ni kwaajili ya kudhalilisha na si kueleweshana. Mtakumbuka wakati anamuhoji mkandarasi kule Dodoma; Mkurugenzi wa Nachingwea; Afisa Polisi kule Butimba nakadhalika. Wote hao ni watu wazima wenye familia zao na mamlaka katika maeneno yao ya kazi, kwa kuwadhalilisha mbele ya kadamnasi anawavunja molari na kuwatisha watendaji wengine. Tabia hii inabidi ikemewe kwa nguvu zote. Nani atamfunga paka kengele?