Kuna tofauti kubwa kati ya MWANANCHI na MWENYENCHI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tofauti kubwa kati ya MWANANCHI na MWENYENCHI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 10, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kauli hii ime tolewa na mmoja wa marafiki zangu. Ilitolewa kiutani lakni nika jikuta nime guswa na hayo maneno. Kwamba Tanzania( na pengine sehemu zinginezo) kuna MWANANCHI na MWENYENCHI. Nika sema ili kuijenga na kuwa hoja ya kujadiliwa ni lazima haya maneno mawili yatolewe maelezo. Maneno haya yata kuwa na maana tofauti kwa kutegemea na mtu binafsi na neno gani ana jifushisha nalo zaidi.

  Mwananchi:
  Mwananchi kwangu mimi ni yule mtu wa kawaida. Mtu ambae hana sauti wala maamuzi katika maswala mbali mbali yanayo husisha maisha yake mwenyewe. Ni yule ambae maamuzi yote hutolewa kwa niaba yake, saa nyingine bila hata kuulizwa ana taka nini. Mwananchi ana mali lakini hata hiyo mali humilikiwa kwa niaba yake na kumiliki kwake kuna tokana na mapenzi ya "wenyenchi". Mwananchi ni yule anaye fanya kazi kwa niaba ya mfumo badala ya mfumo kufanya kazi kwa niaba yake. Mwananchi ni wewe ambao upo hapa una lalamikia mfumo uliyopo kwa sababu mfumo uliyopo hauku nufaishi kwa lolote au kwa lolote.

  Mwenyenchi:
  Mwenyenchi ana muhitaji mwananchi lakni akisha timiziwa mahitaji yake humuona mwananchi si lolote si lolote. Huyu anaweza kuwa mwanasiasa anaye kuomba kura lakini ukimchagua hatimizi ahadi zake. Anaweza kuwa mfanyabiashara ambae ana kunyenyekea ununue bidhaa yake lakni akisha pata hela haoni thamani yako. Pia anaweza kuwa bosi wako ambae ana sifiwa kwa uchapaji kaze wake ili hali kazi zote hufanywa na wewe, na hata siku moja hakupi asante. Mwenyenchi siku zote ana linda "status quo" kwa sababu mfumo uliopo unafanya kazi kwa ajili yake na kwa niaba yake.

  Kama nilivyo elezea mkuu kwangu mimi sifa kuu ya nwananchi hapa ni yule ambae ana lalamikia mfumo uliopo kwa sababu haufanyi kazi kwa niaba yake. Kwa kufuata maelezo hayo naamini kabisa kama wengi wetu humu ni wakweli katika hoja zetu basi wengi wetu ni wananchi, wananchi ambao hawa furahii mfumo uliopo........

  Swali langu haswa ni kwamba je wengi wetu tuna lalamikia mfumo uliopo kwa sababu ni wananchi wazalendo? Au ni kwa sababu mfumo uliopo ume tunyima sisi binafsi kuwa na hadhi ya "wenyenchi"? Je wengi wetu tunge kuwa katika nafasi za tunao walalamikia siku zote humu tungefanya tofauti au tunge kuwa kama wao kwa maana mfumo uliopo upo kwa ajili yetu?

  Nimesema yote haya kwa sababu nimegundua pia sifa kubwa moja wapo ya MWANANCHI pia ni yule anaye taka kuwa MWENYENCHI. Natumai uzalendo unao hubiriwa humu ndani ni wa kweli na siyo unafiki wa watu ambao wameona mfumo uliopo umewanyima kuwa wenyenchi.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mwanafalsafa,

  Hayo makundi uliyoyataja yapo kila mahali, kwamba kuna class struggle ktk individual level mpaka kwene level za juu kama makundi ktk jamii. Umeongelea suala la mfumo, lakini tatizo sio tu mfumo, bali ni binadamu na mindset yao ya ubinafsi. Umegusia hapo mwishoni kwamba 'mwananchi' ana-strive na yeye siku moja awe 'mwenyenchi', which is quiet true. Sasa ktk scenario kama hii usitegemee kwamba status quo ya kuendeleza madaraja (classes) itaondoka.

  Kwangu mimi naona kama ni mzunguko usio na mwisho, kwamba kila mtu ni mbinafsi na anajitahidi kwa kila nafasi kuwa mbinafsi zaidi na kujilimbikizia faida binafsi ili awe mbele ya wengine, lakini at the same time analilia kwamba mfumo uliopo unamkndamiza, lakini punde nafasi ikipatikana ya kupanda kwene pecking order anasahau kila kitu na ku-acquire status ya 'uenenchi'. Kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba watu wote hatuezi kuwa 'wenyenchi', hivo basi jitihada zetu zinaji-contradict kwa sababu haziangalii reality.

  Hoja yangu hapa ni ubinafsi ndio chanzo cha yote, na kama ubinafsi utaendelezwa madhila zaidi yatachumwa siku kadr zinavoenda.
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndugu Abdulhalim,

  Your analysis is very correct. Angalia tu safu ya viongozi tulio nao sasa. Wengi(si wote) wa viongozi tulio nao leo wana tokea kwenye familia zilizo kuwa za hali ya kawaida. Wengine mpaka leo wana jiita "watoto wa wakulima" na wengine hata hizo nafasi walizo nazo ni kutokana na elmu ya bure waliyo pewa na serikali ya awamu ya kwanza. Lakini leo hii angalia vipaumbele vyao vilipo? badala ya kusaidia watoto wa masikini kama wazazi wao walivyo saidiwa leo hii wana zibia ridhiki watoto wa wenzao na kuzibia ridhiki za mwananchi wa kawaida.

  Nakubaliana pia na analysis yako ya kwamba tupo kwenye mzunguuko usio na mwisho. kwa hali ya kawaida una tegemea mtu aliye tokea katika maisha duni au hali ya chini kuwa bingwa na mtetezi wa mwananchi wa kawaida. Lakini nae akipata nafasi ana taka kulipizia manyanyaso na yeye huanza kunyanyasa waliopo chini yake. Nadhani tatizo kubwa duniani ni UNAFIKI. Tuna lalamikia anasa na kufuru za walionacho lakini na sisi tuki pewa nafasi tuna taka kuishi na kutunzwa kama wafalme.

  Anyway maishani siku zote( at least kwa hli ilivyo sasa) lazima tuta kuwa na waongozwa na waongozi. Tunacho hitaji ni viongozi ambao walau wata wapa walio na njaa chakula walicho kibakiza na siyo viongozi wa sasa ambao hula, hushiba kisha kumuaga chakula kilicho baki. Tuna hitaji viongozi watakao ona aibu kutembelea magari ya kifahari kwenye magari mabovu na kuishi kwenye nyumba za kifahari huku wakizunguukwa na "uswahilini". Tuna hitaji viongozi watakao ona aibu kuwa juu kwenye ndege wakati chini masikini hutembea kwa miguu peku. Sawa maishani lazima kutakuwa na walio "juu" zaidi wa wengine. Ila ninacho angalia mimi siyo how high are the high people but how low are the low people. Tuki punguza urefu wa "low" basi natumai walau watu wata jiona wana viongozi ambao wanaweza wasielewe wanacho pitia bali wana watambua na kuwa jali.
   
Loading...