Kuna tofauti kubwa kati ya 'Mama Ntilie' wa Mwanza na Dar

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,697
Pamoja na kuwa haya ndio majiji makubwa nchini, kwa Mwanza suala la kumjali mteja ktk sekta ya ulaji ni ziro kama sio chini ya ziro.

Mfano mama ntilie...
Dar...
.wako shapushapu...
.Wanamthamini mteja utadhani wanamjua miaka mingi...
.Wanajua kupromote chakula wanachokiuza hata kama hakina kiwango...
.Muda wa kukaribishwa hadi kula ni mfupi sana...
.wasafi kidogo japo sio sana...
.wana lugha ya ushawishi kuanzia bosi hadi wahudumu wake...

Mwanza
.Wengi wamezubaazubaa...
.unaweza ukatumia kama dakika tano kumuelimisha unachotaka muhudumu...
.Hawajali Muda wa mteja wao...
.Lugha zao sio za kumbembeleza na kumshawishi mteja, wengi wanaona kama wewe ndio unawasaidia...
.Pamoja na kuwa karibu na ziwa la maji baridi lkn wengi sio wasafi sana.
.Ni kawaida mteja kuja nao wakawa wanakuangalia huku wakipiga story na kujishauri jinsi ya kuamka kuja kukuhudumia.
 
Kuna factors kama
1. Level ya ushindani
2. Aina ya wateja unaowahudumia
3. Kujielewa na kuielewa biashara unayoifanya
4. Na kadhalika

Juzi nimepigwa na butwaa hapa ninapoishi/sinza/ kuna gari asubuhi nikitoka nakuta imeshapaki nikirudi kwenye saa 2-3 usiku ndio inaondoka kuja kuuliza ni ya mama ntilie nikajaribu during the weekend kuangalia huduma yake kwa kweli ni ya hali ya juu na bei ya chakula haitofautiani na Manzese
Nilichokigundua ni kwamba anajua anachokifanya na anajijua
 
Yaani mimi nakuunga mikono na miguu kabisa kwa mama ntilie wetu wa mwanza naweza kusema ni wajinga hawajui kumshawishi mteja kwamba akienda arudi tena yaani wapo wapo tu kama makontena bandarini yanasubiri kupakiwa wana lugha chafu unaweza kuagiza chakula hata nusu saa wewe umekaa tu kijiweni unasubiri ukienda kumuangalia kwanza ndiyo anatukana tu wasaidizi wake mama lishe wa Mwanza mubadilike
 
Mama Ntilie wa Dar walio wengi ni wasafi sana na niwakarimu sana,kwa mfano ukienda soko la ndizi-mabibo,mama ntilie wa Manzese tiptop ( huwa wanapatkana sana nyakati za usiku),mama ntilie wa urafiki soko la kuku,mama ntilie wa maeneo ya magomeni,posta (wanapatikana ufukweni), mama ntilie wote wa Mwenge na Sinza ni wasafi sana
Lakn mama ntilie wa Mwanza walio wengi ni wachafu na hata kiswahili kwao ni tatzo japo siyo wote!
 
Level of competition Dar ni kubwa saana kila mama ntilie anajaribu kujitofautisha na wenzie ili kuwavutia wateja zaidi

Mwengine mpaka chai anatia tui

Kuna mwingine yeye ana radio yake anatia miziki ya wahenga tuu basi utakuta msururu wa Wahenga

Huyu mwingine ndio kazidisha kazi ya wahudumu 2 yeye ana wahudumu visichana vidogo dogo kama 6 hivi na huwa anavibadilisha kila baada ya muda
 
Wapi hapo mimi ni muhenga Pana nifaa mdau wa nyimbo zile hahahahha
 
Yaani mimi nakuunga mikono na miguu kabisa kwa mama ntilie wetu wa mwanza naweza kusema ni wajinga hawajui kumshawishi mteja kwamba akienda arudi tena yaani wapo wapo tu kama makontena bandarini yanasubiri kupakiwa wana lugha chafu unaweza kuagiza chakula hata nusu saa wewe umekaa tu kijiweni unasubiri ukienda kumuangalia kwanza ndiyo anatukana tu wasaidizi wake mama lishe wa Mwanza mubadilike
kuna haja ya kuelimishwa aisee.
wengi wanamentality za miaka ya tisini ambapo mtu kuja kula kwa mama ntilie anakuwa anamuogopa muhudumu maana ilikuwa sio kawaida. wengi tulikula kwetu.
siku hizi mambo yamebadilika ila wengi bado hawaendani na kasi ya mabadiliko ya sasa. Akitokea mtu akajaza hilo ombwe utasikia majungu "anatumia dawa huyo".
 
Level of competition Dar ni kubwa saana kila mama ntilie anajaribu kujitofautisha na wenzie ili kuwavutia wateja zaidi
Mwengine mpaka chai anatia tui
Kuna mwingine yeye ana radio yake anatia miziki ya wahenga tuu basi utakuta msururu wa Wahenga
Huyu mwingine ndio kazidisha kazi ya wahudumu 2 yeye ana wahudumu visichana vidogo dogo kama 6 hivi na huwa anavibadilisha kila baada ya muda

Kuna mtaa mmoja huwa napitapita pale mama ntilie (wengi wamekodi flemu) buku jero unaweza kula mboga karibu sita standard iko safi kabisa.

Kabla ya mida ya misosi wanapita kwa wadau kuomba order yaani wadada na wamama wachangamfu, chakula bora hadi mtu anashindwa achague nani amuache nani.

Nikasema mmoja wa hawa ukimcopy ukampaste hata nyegezi stand alafu yule wa pale stand (kuna mmoja yupo kwenye jengo advanced kidogo sio mama ntilie kivile) anaweza kuwa millionea.
 
thread zingine bhana kama nyimbo za singeli na baikoko. mi hata siwaelewagi maana kila kitu siku hizi ni mkoa vs mwanza ama kabila vs wasukuma ni ushamba wakati mwingine. kuna msemo unasema hivi akutukanae kwa sauti rohoni anakukubali.
 
baadhi ya mama lishe wa Dar wanaweka hamira kwenye chakula chao,baadhi,mwanza sina uhakika kama wanafanya hivyo

ila kwa usharp,wa Dar they mean business,mwanza bado maisha ya kawaida na maisha hayajakaza

sinza pekee ina fastfood nyingi kuliko mwanza,pale mwanza mjini na hata pembeni ni vigumu kuona fastfood,labda mabanda ya chips
 
Acheni maneno yenu tabia ya mtu mmoja sio tabia ya mkoa mzima. Research yako ilikuwa na sampling kiasi gani? Nenda darajani karibu na msikiti wa mabanzi uone kuna dada anaitwa madina uagize msosi. Mke wako itamchukua miaka 10kufikia
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom