Kuna tofauti gani ya kupata urais na kuwa rais ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tofauti gani ya kupata urais na kuwa rais ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Jul 23, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  hivi vitu hutofautiana?
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Swali gumu sana hilo, mtu asipokuwa makini anaweza kupata "zero"

  Ngoja nijaribu kwa kutoa mifano..........

  Mwalimu alikuwa Rais....Mzee Ruksa alipata U-Rais

  Mr Clean alikuwa Rais.....Mk**e alipata U-Rais

  Hassan Dalali alikuwa Mwenyekiti....Ismail Aden Rage alipata U-enyekiti.....!!!!!!!!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  mkuu naona umenipa kazi nyingine tena.but nimekupata
   
 4. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umezunguuka sana mkuu..
   
 5. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kwa mtazamo wangu kupata urais ni kitendo cha mtu kuingia madarakani (madaraka yenye jina la urais) baada ya kuwa ametamani na kutafuta nafasi hiyo kwa muda fulani kabla. Kwa Tanzania ni namna kama iliyomwingiza JK madarakani. Hapa mtu anayetamani kuwa rais anakaa na watu wake wa karibu na kupanga mikakati ya namna gani ataweza kupata nafasi hiyo. Mwisho wanatafuta fedha na kufanikiwa kutengeneza njia inayompeleka jamaa madarakani. Sifa mojawapo ya viongozi wa aina hii ni kushindwa kutoa maamuzi kwa kuwaogopa waliompa/kumwezesha kupata urais huo. Huyu hata ukimwuliza ghafla tangu ameingia madarakani amefanya nini anachoamini rais mwingine asingeweza, atakwambia ametoa uhuru kwa vyombo vya habari na kummwagia tindikali aliyetumia uhuru huo kufichua maovu ya wanasiasa.

  Kuwa rais
  ni kitendo cha mtu kuingia madarakani (urais) baadaya kuwa amefanya shughuli tofauti kwa mafanikio makubwa au madogo pasipo yeye mwenyewe kutamani wala kukusudia saaana kupata nafasi hiyo. Mfano inatokea mtu, kwa imani za watu kwake akajikuta anawajibika kuchukua nafasi hiyo kwa matakwa ya watu wengine na kuwa na mamlaka kamili juu ya maamuzi anayopaswa kuyatoa pasipo kuwaogopa watu fulani fulani. Dr. Slaa angeingia madarakani baada ya uchaguzi wa 2010 angekuwa rais. Dr. Shein wa Zanzibar pia anaweza kuwa mfano wa ambaye amekuwa rais maana hakujitafutia nafasi hiyo mwenyewe bali watu walioamini atafaa ndiyo walipendekeza na kumuwezesha japokuwa inawezekana wakawa wamefanya hivyo kwa maslahi yao tofauti na umma. Kama anao uhuru wa kuamua anachoamini kinawafaa watu wake kwa pamoja pasipo kuhofu watu waliomweka hapo anafit moja kwa moja katika hili.
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Analysis nzuri!
   
 7. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Rais anaweza kuwa wa Coca Cola, Toyota, Chuo au taasisi yoyote, nchi n.k. Tena nasikia siku hizi hata kuku nao eti wanataka wawe na Rais wao. Wanasema eti wamechoka kuchinjwa chinjwa ovyo na binadamu. Hawakatai kuchinjwa, ila wanataka kuwe na utaratibu maalum wa kupotezewa maisha yao. Takwimu zinonesha kuwa kuku zaidi ya bilioni 10 hupoteza maisha kila mwaka, idadi inaweza kuongezeka miaka ya karibuni
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  unaongeza idadi ya post zako
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ndio tofauti ya kuwa raisi na kupata uraisi haswa!
   
 10. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Sitta alikuwa Spika, Makinda aliupata uspika.....umemaliza.
   
 11. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha haaaa....!!!!!Hakika Mkuu!
   
Loading...