Kuna tofauti gani kati ya "Secretary General" na "General Secretary"? Kwanini Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) haitwi "General Secretary"?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,395
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kuna tofauti gani kati ya "Secretary General" na "General Secretary"? Kwanini katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN) haitwi "General Secretary"?

Tafadhali tazama screenshots hapo chini;

The Secretary General
images (57)asddd.jpg

The General Secretary
images (57)asdddzxcdsssss.jpg

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,747
2,000
Ninaomba ufafanuzi wa wataalam please.
Maneno yote kwa tafsiri ya Kiswahili ni Katibu Mkuu, ambaye ni Afisa Mkuu au kiongozi wa chama cha siasa au shirika.

Kwa lugha ya Kiingereza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaongezewa neno "The", ambalo hutumika kama kiunganishi cha nomino (noun) yenye upekee (specific). Umoja wa Mataifa ni Taasisi ya kipekee duniani, kwani kuna Taasisi na vyama vingi vya siasa vyenye Katibu Mkuu.

Kwa kiingereza kwa mfano hawasemi "earth" (dunia), bali "the earth" kwa maana kuwa dunia ni kitu pekee katika sayari
 
The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
6,891

Kwahiyo?
 
Naona Mods wame edit hiyo heading. Swali langu original ni hili hapa;

Kuna tofauti gani kati ya "Secretary General" na "General Secretary"? Kwanini katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN) haitwi "General Secretary"?
 
Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,981
2,000
Hili jambo nakumbuka lilishajadiliwa kipindi cha nyuma. Tafadhali tafuta uzi wenye heading;
1. General secretary
2. Secretary general
3. Chief secretary

Wasalaam!
 
Sulphur Hexafluoride

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,700
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kuna tofauti gani kati ya "Secretary General" na "General Secretary"? Kwanini katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN) haitwi "General Secretary"?

Tafadhali tazama screenshots hapo chini;

The Secretary General
View attachment 1575007

The General Secretary
View attachment 1575008

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ngoja wajuzi wa masuala haya waje.
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,747
2,000
Mkuu, hayo mambo ya "The" mimi wala sijayauliza. Mods ndio wame-edit heading na kuweka hiyo "The"
Sawa mkuu...
Pamoja kwamba "mods" wamebadili ulichokuwa umekusudia kuuliza, bado kimsingi Katibu Mkuu (General Secretary au Secretary General) ni neno linalomaanisha kitu kimoja, yaani Mkurugenzi Mtendaji ambalo hupendwa kutumiwa na mashirika ya kimataifa, yasiyo ya faida, na ya kisiasa. Mengine hutumia "Executive Secretary". Hapa nchini tunatumia km Serikalini Katibu Mkuu Kiongozi (Chief Secretary) ambaye ni kiongozi wa Makatibu Wakuu (Permanent Secretaries).

Shughuli za Katibu Mkuu zinajumuisha shughuli za "Secretary" au Katibu katika kiswahili, ambaye ni mtu anayefanya kazi za kumsaidia mkuu wa shughuli yoyote ya kiofisi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom