Kuna tofauti gani kati ya Mganga wa kienyeji na mchawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tofauti gani kati ya Mganga wa kienyeji na mchawi

Discussion in 'JF Doctor' started by nhassall, Oct 5, 2012.

 1. n

  nhassall Senior Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Natamani kupata mjadala wenye kuweza kuleta majibu yaliyoshiba mawazo huru yenye mitazamo tofauti, kwani siku hizi kuna wimbi kubwa la watu kugeukia dawa za kienyeji zaidi kuliko zile zinazotolewa na hospitali za kawaida.
   

  Attached Files:

 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  utofauti upo mchawi anatumia mazingaombwe huyu anatumia dawa za mitishamba sasa hauoni kama utofauti upo?
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mganga anatibu mchafiwi anadhuru lakini inaweza kinyume chake pia....
   
 4. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hakuna tofauti maana mganga wa kienyeji lazima awe mchawi
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu bornagain Mchawi ni Mtu anaye dhuru watu na hajuwi kutibu watu. Mganga wa Kienyeji

  ni mtu anayejuwa Kutibu na kudhuru pia anajuwa lakini yeye kazi yake ni kutibu sio kudhuru watu. Mganga wa

  kienyeji anayedhuru watu atakuwa ni mchawi na hawezi akawa na kipaji cha kutibu watu na kudhuru watu

  pamoja itabidi acahague moja kati ya hayo mawili awe ni mchawi lakini hawezi pia akawa ni mganga kwa sababu Uganga una masharti aidha uwe ni Mganga usidhuru watu au uwe ni Mchawi wa kudhuru watu kwa mambo ya uganga hutaweza kutibu watu.


  Ukiwa wewe ni Mganga kisha unawadhuru watu utakapodhuru watu hutaweza kuwa na nguvu ya kutibu watu yaani huwezi kuwa na nguvu 2 kwa

  wakati mmoja hicho kitu hakiwezekani hata kidogo.Ukimuona Mganga anaye wadhuru watu huyo sio mganga

  huyo ni Mchawi kwa sababu huwezi kupata Vipaji 2 kwa wakati mmoja hicho kitu hakiwezekani hata kidogo.

  Huwezi kuwa na kipaji cha kuwatibu watu kisha uwe na kipaji cha kuwadhuru watu kwa wakati mmoja uwe na Vipaji 2 Kudhuru na kutibu kwa wakati mmoja haitowezekana hata kidogo.
   
 6. Justin Dimee

  Justin Dimee JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 1,148
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  mmh mbona wapo watu wana enda kwa mganga wanawaloga watu wanakuwa machiz na anaye toa huo uchawi ni huyo huyo mganga apo vp cja elewa.
   
 7. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,964
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Waganga wote wa kishenzi walianza kuumiza watu kwa uchawi, waganga wote ni wachawi lakini wachawi wengi siyo waganga.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  subiri waje wenyewe watuelezee
   
 9. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani kuna

  1) machawi - anadhuru watu

  2) mganga wa kienyeji - anatibu lakini wapo kiimani zaidi eg kuongozwa na majini au shetani kupata solution!! Utakuta anakwambia subiri nipandishe mashetani! Alafu uyaambie matatizo

  3) mtaalamu wa miti shamba au mganga wa tiba mbadala - hawana mashetani zaidi ya utaalamu wa mitishamba utakuta elimu wameiendea shule ( chinese traditional medicine) au kujifunza kutoka kwa wazee ( wamasai) hawa una kwenda na tatizo anakupa dawa bila kupandisha mashetani
   
 10. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi ni mwenyeji wa mkoa mpya wa Katavi and am talking through experience nachokuambia ni kwamba mganga wa kienyeji nae ni mchawi tu. Nasema hivo utakuta mgonga wa kienyeji anamwambia mteja wake kuwa ili upone au ili ufanikiwe unatakiwa kuua mtoto wako na anamvuta kwenye kioo mpaka pale ulipo then anakupa sindano anakuambia ukishamdunga tu kwenye kioo cha kiganga palepale mtoto atafariki so hapo hujaona kama mganga nae ni mchawi tu. Au hata mganga mwenyewe kuna wakati dawa zinaisha nguvu kwa hiyo kuziboost inatakiwa aue mmoja wa familia yake. Kule Sumbawanga kuna watu wametajirika kwa kujiita waganga wanamloga tajiri wao wenyewe halafu wanamuendea moja kwa moja huyo tajiri na kumuambia kuwa sie ni waganga wa kienyeji ili kupona ugonjwa wako unatakiwa utupe milion kumi na kweli ikishatolewa hiyo milion kumi mtu wa watu anapona na wao wanachukua chao.So mganga ni mchawi
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu bornagain Mganga ambaye anayekwambia ukitaka mafanikio yako itabidi umuuwe mtoto

  wako, mganga huyo kwangu mimi nina muita Mchawi sio Mganga mimi Babu yangu alikuwa ni mganga maarufu huko

  kwao Uzaramuni hakuna mtu hata mmoja aliyesema kuwa babu yako aliwahi kuwaambia wateja wake Eti ukitaka kufanikiwa mambo yako lazima Umuuwe Mwanao hicho kitu kamwe sitoweza kukubaliana nacho huyo

  atakuwa sio mganga bali ni Mchawi mganga kamwe hawezi kukwambia ukitaka kufanikiwa Umuuwe mwanao eti ufanikiwe Mganga

  akisema hivyo mimi huwa ninamuita Mchawi sio mganga kazi yake ni kuwatibu watu maradhi na matatizo yao

  sio kuuwa watu anaye uwa watu huyo sio Mganga huyo ni Mchawi. Kwenye Miaka ya 1980 mpaka 1986 mimi

  binafsi yangu nilisha wahi kwenda kwa Waganga hapo Dares-Salaam zaidi ya Waganga 20 nilikuwa ninaumwa

  maradhi ya ajabu Homa za mara kwa mara kichwa kisicho pona Moyo kwenda mbio kiuno na mambo mengine

  siyawezi kuyataja hapa ni Siri yangu nilikwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupima vipimo vyote yaani kupiga picha ya

  EX-Ray,kupima mkojo na Damu hawakuona kitu ndio nikamuwa kwenda kwa hao Waganga na nilipoona mambo

  mengi wanayoyafanya Waganga mengine ni ya ukweli na mengine ni ya uongo na nilijifunza mengi mpaka nlipona

  nili Rogwa na kutupia pepo mbaya na nilimaliza Waganga mpaka akaja kijana mmoja kutoka Mwanza kunitibia

  ndipo nilipo pona kwa hiyo nina wafahamu kwa undani baadhi ya Waganga wanatumia mbinu ili waweze

  kupata pesa nyingi kwa wateja wao kwa mfano wewe unaweza kuumwa na kichwa tu sababu hupati usingizi

  vizuri au una mawazo au una matatizo ya kutopata choo ukienda kwa mganga akikupigia Ramli kitu cha kwanza

  atakuambia umerogwa na mtu wako wa karibu ukikubali hapo umeingia kwenye mtego wake kwa leo

  ninakuacha hapo......
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Viper ninakubaliana na wewe kwa asilimia 99 sikubaliani na mkuu.@bornagain kabisa anavyosema.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Asante Sasa wewe badala ya kueleza unawatukana waganga? mkuu sivyo hivyo usilete matusi hapa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama ambavyo umeambiwa mganga ana uwezo wa kutibu na akikiuka masharti hudhuru pia,mganga wa kweli anapotakiwa kudhuru mtu huangalia kosa la yule au dhuluma aliyoifanya anayetakiwa kulogwa.akikuta jambo alilolifanya yule muhusika ni baya sana kwa mustakabali wa kibinaadamu humuelekeza mlogaji kitu cha kufanya ili kuwezesha kisasi au haki ya mlogaji kufanikiwa.hata hivyo waganga waweza gawanywa katika makudi tofauti{1}mganga mchawi,huyu huloga watu na baadae kuwafanya waje kwake kupata tiba na baadae apate kipato.{2}mchawi mganga huyu huloga watu na baadae hujifanya mjuzi sana wa tiba kwa ujira fulani{3}mtaalam wa kawaida wa dawa za asili huyu sio mganga ila huwa ni mjuzi sana wa dawa mbali mbali za kiasili ambazo huwasaidia nazo watu aidha kwa kipato au kwa msaada tu.{4}mganga kamili,huyu hutibu tu na mara nyingi huharibu njia za wachawi ili kuwezesha ukamilifu wa tiba zake,hadhuru mtu kama hana kosa na akidhuru basi ndipo ubatili wa dawa zake huanza hapo,na toka hapo huwa ni mchawi na sio mganga tena.halafu huwa na nguvu sana za kiasili zitakazomlinda na visasi na hasira za wachawi ambao hawapendi kutibuliwa kwa ishu zao.ninayo mengi ya kuandika lakini kwa leo niishie hapa kwanza.
   
 15. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ukimuuliza yeye anaamini dini gani aweza kwambia yeye ni mkristu wakati wenzake wanazunguka na maiti iliyofukuliwa huko wanaizika tena, tatizo letu sisi waafrika wengi tunapokea kila kitu bila kujibidiisha kujua siri ya dunia hii,tupo kama magunia tunasubiri wachuuzi watujaze bidhaa bila kujali zinanuka au ni safi.kama lile jambo lingefanywa na waafrika hasa watanzania wenzetu wa kabila lolote wangevikwa uchawi,uchafu,ujinga na upumbavu wote unaojulikana.lakini kwa vile lina asili ya kizungu safi tu.hihi dunia hii ina siri sana hii.ila wajinga tutaliwa sana sisi.siku njema mheshimiwa mzizi mkavu.

   
 16. MGANGA WA KIENYEJI

  MGANGA WA KIENYEJI JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mganga wa kienyeji na mchawi ni sawa na Malaika na Shetani. Malaika ndie anaeweza kupambana na Shetani kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Vile vile Mganga wa kienyeji anaweza kupambana na Mchawi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

  Mganga yoyote ili awe mzuri zaidi lazima ajue mbinu za kichawi. Ili uweze kutibu ugonjwa , lazima uujue na ujue tiba yake. Hivyo basi, Mganga sio Mchawi, ila anaujua uchawi ili aweze kukabiliana nao.

  Je Polisi na Wanajeshi ni Majambazi kwasababu tu wanajua mbinu za Majambazi na kutumia silaha za moto?.
   
 17. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,064
  Trophy Points: 280
  Tumekosa maneno mazuri hapa maana kuna Mchawi (huyu anasimama yeye kama yeye na mara nyingi yupo kwa ajili ya kudhuru au kuleta mauzauza) alafu kuna waganga wa kienyeji (ambao wamegawanyika ktk aina mbili i.e. wale wanaotumia mitishamba na wale wanaotumia ramli uchawi), kwa waliosoma St nini wanapenda kuweka kwa lugha hii WITCH DOCTOR (mganga mwenye nguvu ya miujiza) na TRADITIONAL HERBALIST (anatumia miti shamba)

  Au kama alivyofafanua Viper hapo juu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jodoki Kalimilo Umezungumza vizuri ila umekosea kusema kuwa ( wale wanaotumia ramli uchawi) neno (Ramli) kuwa ni uchawi na (Ramli na Uchawi) ni vitu viwili tofauti kabisa.Neno Ramli ni neno la kiarabu kwa kiswahili ni mchanga wa

  kutizamia mambo yako ya maisha au tunaweza kusema kupiga bao kwa lugha ya kiswahili sasa unaweza kujuwa

  kutizamia kwa kutumia hiyo (Ramli) Kupiga Bao lakini ukawa hujuwi kufanya uchawi wala mambo ya uganga unaweza kuwa ni Mtabiri wa kupiga ( Ramli) lakini usiweze kutibu watu wala

  kuroga watu .Na neno (Uchawi ) Uchawi kazi yake Mtu huwa anadhuru watu kwa huo uchawi wake mchawi hajuwi mambo ya Ramli wala mchawi

  hajuwi kutizamia kwa aina yoyote ile Mchawi anachojuwa yeye ni kudhuru watu sasa usituchanganye kati ya mpiga

  Ramli na mchawi ni vitu 2 tofauti kabisa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Tuna hamu ya kutapeliwa.
  Wachawi na waganga ni walewale tu. Anakuloga Juma, Juma anampigia simu Hamis, unaenda kutibiwa na Hamis, then wanagawana mshiko
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  mkuu Sumbalawinyo Umenichekesha kweli mfano wako kama huu mfano kati ya Daktari na muuza Dawa Pharmacy

  wanashirikiana huku nilipo unapoumwa ukienda kwa Daktari atakuandikia dawa nyingi tu kupita hayo maradhi yako ili uende kwenye

  duka la kuuza Dawa Pharmacy ukanunuwe dawa kisha na yeye anapata ulaji wake baada ya wiki,kazi kweli kweli ingelikuwa kuna ushirikiano kati ya Mganga

  wa kienyeji na Mchawi basi Wachawi wasingelikuwa wanakamtwa mkuu amka ujuwe tofauti ya Mchawi na mganga wa kienyeji.
   
Loading...