Kuna tofauti gani kati ya maneno haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tofauti gani kati ya maneno haya?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MwanaFalsafa1, Sep 26, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Napenda kuuliza kuna tofauti gani kati ya neno "marehemu" na "hayati"? Najua yote yana tumika kumtaja mtu aliye fariki ila juzi nikamsikia mtu ana sema aki taka angependwa kuitwa hayati na si marehemu. Siku weza kumuuliza pale pale ndiyo maana nimeamua kuja humu kuuliza.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wataalamu wa kiswahili (if I am not wrong) wanasema ni tofauti ya matumizi. ikiwa kwa mfano Nyerere unataka kutamtaja katika maongezi ya kawaida unaweza kusema marehemu, lakini ikiwa unakumbuka jambo alilotenda au usemi wake unasema hayati kwani usemi wake wawezza kuendelea kuexist.
  too bad many presidents will never be hayati bali marehemu
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Yote maneno yenye asili ya Kiarabu marehemu (Al-Marhum) kwa watu wa kawaida na Hayati (Al-Hayat) kwa watu wenye nafasi au jina katika jamii
   
 4. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Sina uhakika, ila wanasema marehemu ni asiye na kisomo, na hayati ni msomi na mwenye mchango ktk jamii.
   
 5. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asante! hata mimi nilikuwa nikifahamu vivi hivi, ukiangalia kamusi ya kiswahili-English majina yote yana kuwa referred to as deceased or the late. kama alivyosema safari, hayati huwa inatumika kwa viongozi au watu wenye remarkable conbtribution kwenye jamii na marehemu ni kwa kila mtu. lakini nadhani pia si makosa mfano kusema marehemu mwal. Nyerere. Kwa ufupi ni kuwa kila Hayati ni Marehemu lakini sio kila Marehemu ni Hayati!
   
 6. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Marehemu
  Tofauti ni nafasi aliyokuwa nayo huyo mtu kabla ya kifo chake. Katika hali ya kawaida kunawatu ambao tunawaita waheshimiwa. Yaani kila unapotaka kumtaja lazima uanze na Mh. Fulani, na pia wapo ambao hulazimiki kuanza na neno Mheshimiwa .... pindi unapotaka kumuita kwa jina, Hivyo basi tofauti hizi ndizo ambazo hupelekea kuwepo kwa matumizi haya ya Marehemu na Hayati katika nyakati tofautitofauti. Mtu ambaye katika uhai wake halitumiki neno Mheshimiwa basi akifa huitwa Marehemu,

  Hayati
  Kadhalika mtu ambaye hutumika neno Mheshimiwa ili kumuita, pindi akifa tunalazimika kutumia neno Hayati ili kuonesha kwamba bado tunaheshimu nafasi aliyokuwa nayo wakati wa uhai wake.

  Tofauti katika matumizi
  Kuna wakati inalazimika kuwepo kwa tofauti katika matumizi ya maneno haya. Mfano; unapotaka kumzungumzia mtu aliyekwisha kufa nje ya cheo au nafasi aliyokuwa nayo katika jamii basi litatumika neno Marehemu na si Hayati. Kwa mfano: tukimzungumzia Edward Moringe Sokoine nje ya nafasi aliyokuwa nayo wakati wa uhai wake tutasema Marehemu Moringe Sokoine ali........... Lakini tutakapokuwa tunamzungumzia katika nafasi ya uheshimiwa wake tutasema Hayati Moringe Sokoine ali.........


  Ikumbuke haya yote si sheria ila ni utaratibu tu katika lugha, ambao umechukua nafasi kutokana na mazoea yaliyopo katika matumizisahihi ndani ya jamii zetu.
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Pia Hayat linaweza likawa jina la Mtu!.. nina rafiki ya mpakistani anaitwa HAYAT
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Asanteni nyote kwa majibu yenu. Sasa naelewa. Ila kwa kuendeleza tu mjadala.
   
 9. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Karibu tena kaka kwa kumalizia kuna kipande cha rylics nyimbo flan INTA HAYATI na hivi ndivyo walivyo tafsiri

  Inta Hayati,
  (You are my life)
  Inta Habibi.
  (You are my love)
  Min awil nazra
  (from the very first sight)
  Wsourti nassibi.
  (You became my destiny)
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Neno Marehemu, linatokana na neno la kiarabu Al-Marhum, maana yake ni Mwenye Kurehemewa (Linatumika kwa Binadam aliye fariki au Kufa)

  Neno hayati pia ni neno la kiarabu na maana yake ni Uhai, au Mwenye Uhai
   
 11. K

  Kanwa Member

  #11
  Jul 19, 2013
  Joined: Feb 15, 2013
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeelimika nami,
   
 12. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2013
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Hivi m2 anaweza kuitwa 'hayati' siku 3 baada ya kufa au kabla hajazikwa? Hivi unaweza kusema ndugu wa hayati waje kutoa heshima za mwisho kwa hayati, hata kama alikuwa kiongozi au m2 mwenye nafasi katika jamii? Mimi navyojua, marehemu ni m2 aliyekufa na hajazikwa bado. M2 akifa hata kama itapita miaka 10 bila kuzikwa hawezi kuitwa hayati. Marehemu ni m2 aliyekufa na hajazikwa bado, na baada ya kuzikwa na kupita muda fulani ndio anaanza kuitwa hayati.
   
 13. y-n

  y-n JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2013
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 1,735
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  jf,raha kweli-kweli.
  nasikia kuna mwingine anaitwa Hayat JK,yupo magogoni pale.!
   
Loading...