Kuna tofauti gani kati ya kaptura, bukta na pensi?

Naona watu wanarukaruka ngoja muhenga niwape somo
Bukta ni brand name kama Nike. Zamani sana kaptura za michezo zilikuwa brand hio ndio maana hilo jina linatumika kwa kaptura nyingi za michezo. Ni kama vituo vya mafuta kuitwa sheli aka shell kwasababu ndio ilikuwa kampuni maarufu ya kuuza mafuta.
Pensi ni Pants Kiingereza. Pants inaweza kuwa short pants, 3/4 pants au long. Ni kama suruali.
Kaptura ni jina la jumla la suruali kipande. Kiingereza ni shorts.
Mimi binafsi nimekulewa mkuu!
Kama kuna mtu hajakuelewa bila shaka atakuwa na matatizo yake binafsi.
 
Kaptura ni neno la kikurya ambalo kiswahili chake ni Kaptula,Bukta ni kama anayovaa Christiano Ronaldo akiwa uwanjani, Pensi wanavaa masharobaro...
 
Bukta nguo fupi ya kiume ,aghalabu yatumiwa kwenye michezo na kujisitiri maungo ya ndani.
Kaptula suruali mkato ya kitambaa laini iliyokatwa magotin na kupindwa kwa mkono .
Pensi kitambaa kigumu ama kisicholaini aghalabu jeans ama kadet iliyoshonwa kitaalam kuiishia magotin .
Upo baharia.?
 
Back
Top Bottom