Kuna tofauti gani kati ya kaptura, bukta na pensi?

Kibuje

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
292
286
Hivi vitu kiukweli mimi binafsi vinanichanganya, kama ambavyo hesabu logarithm zilivyokuwa zikinichanganya sekondari.
Kwa wale wajuzi wa mambo hebu tuwekane sawa hapa, kuna tofauti gani kati ya bukta, pensi na kaptura?
 
Bukta ni nguo ya michezo fupi inayoishia magotini na kaptula ni nguo ya kuvaa fupi. Pensi ni aka ya kaptula
 
Nashauri mleta mada atafute wazazi wake au watu wazima wanaoshi jirani yake watamsaidia kutofautisha hapa jukwaani wengi wetu tunawaza mengine haya maswali ya watoto ni shida.!
 
Thread crossed, for further references concert Ze Mburula, Le kibamia
 
1.Kaputura (kaptura) ni kwa ajili ya watoto wa kiume wanaosoma shule za msingi.

2.Bukuta (bukta)ni kwa ajili ya watu wote wakubwa kwa wadogo sema mara nyingi hutumika kwenye lahaja za kimichezo.

3.Pensi pia huvaliwa na watu wote,na chimbuko lake ni nguo vupi ya jinsi lakini hii imeenda mpaka sikuhizi kuna pensi za nguo laini au vitambaa.

Note:- Majina yote yana maana sawa yaani yanataja kitu kile kile
 
Bukta ni nguo ya michezo fupi inayoishia magotini na kaptula ni nguo ya kuvaa fupi. Pensi ni aka ya kaptula
Zote zinaweza kufika juu au chini ya magoti na pia zote ni nguo. Tunachotaka kujua ni tofauti yake mkuu!
 
Nashauri mleta mada atafute wazazi wake au watu wazima wanaoshi jirani yake watamsaidia kutofautisha hapa jukwaani wengi wetu tunawaza mengine haya maswali ya watoto ni shida.!
Ukishindwa kujibu kaa kimya mkuu. Sio lazima kila mtu ajue wewe ni mjinga kiasi gani.
 
1.Kaputura (kaptura) ni kwa ajili ya watoto wa kiume wanaosoma shule za msingi.

2.Bukuta (bukta)ni kwa ajili ya watu wote wakubwa kwa wadogo sema mara nyingi hutumika kwenye lahaja za kimichezo.

3.Pensi pia huvaliwa na watu wote,na chimbuko lake ni nguo vupi ya jinsi lakini hii imeenda mpaka sikuhizi kuna pensi za nguo laini au vitambaa.

Note:- Majina yote yana maana sawa yaani yanataja kitu kile kile
Afadhali ya wewe mkuu, umejaribu kujibu!
Kama kaputura (kaptura) inavaliwa na watoto, ina maana watu wazima hawavai kaptura?!
Unaweza kuvaa pensi michezoni?
 
Kaptura
20190904_130808.jpeg
 
mara nyingi Pensi inakuwa kaptula ya kitambaa cha jeans,kigumu,,kaptula inaweza kuwa ya kitambaa cha cotton lakini si cha jeans,halafu bukta ni kaptula ila ya kitambaa laini,mfano polyster,kwa uelewa wangu
 
Ndio maana huwezi kwenda matembezini na bukta
 
Kaptula funavaa mabaharia

Pens wanavaa wanavaa wanaume wa dar

Bukta wanavaa wanaspot
 
Bukta - Nguo fupi za Michezo
Kaptula - Nguo fupi inayoishia magotini ambayo ikiwa ndefu itaitwa suruali ikiwa fupi kwenye magoti ni kaptula
Pensi - Nguo yeyote fupi ya kuvaa ambayo haifall kwenye category ya bukta wala kaptula.
 
Ukishindwa kujibu kaa kimya mkuu. Sio lazima kila mtu ajue wewe ni mjinga kiasi gani.
Mjinga wewe usiejua maana ya majina hayo,yaani hadi unaota mav*zi na unapata mume bado hujui vitu vidogo kama hivyo?
Unampaje huduma mumeo na wanao kama vitu vidogo vinakushinda kuelewa!?
Jiangalie tena huko chini jinsia yako!!
 
Naomba nikupandishe cheo, kutoka kuwa mjinga mpaka sasa wewe ni MPUMBAVU rasmi.

Hongera sana mkuu! 🤣
 
Hivi vitu kiukweli mimi binafsi vinanichanganya, kama ambavyo hesabu logarithm zilivyokuwa zikinichanganya sekondari.
Kwa wale wajuzi wa mambo hebu tuwekane sawa hapa, kuna tofauti gani kati ya bukta, pensi na kaptura?
Naona watu wanarukaruka ngoja muhenga niwape somo
Bukta ni brand name kama Nike. Zamani sana kaptura za michezo zilikuwa brand hio ndio maana hilo jina linatumika kwa kaptura nyingi za michezo. Ni kama vituo vya mafuta kuitwa sheli aka shell kwasababu ndio ilikuwa kampuni maarufu ya kuuza mafuta.
Pensi ni Pants Kiingereza. Pants inaweza kuwa short pants, 3/4 pants au long. Ni kama suruali.
Kaptura ni jina la jumla la suruali kipande. Kiingereza ni shorts.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom