Kuna tofauti gani kati ya Home Theatre na Sub-woofer?

yaani mkuu spika kama hii ukaweke sebuleni kwako? mbona haijakaa sexy kiasi cha kukaa sebuleni? kuna picha jamaa kaweka hapo juu kaweka maspika kibaao sebuleni kama disco. sasa vioo si vitapata crack?
hiyo iko uchi inatakiwa ikae ndani ya box lake,maana ikiwa hivyo kwanza haitoi sauti iliyopangwa.
 
Watu wametiririka kitaalaam kabisa mpaka sie wazee wa zamani tunaoweka radio juu ya mtungi kupata bass tunashawishika kununua sabufa
 
kuna bandiko nimelisoma hapo juu jinsi ya kuseti hiyo home theatre kwenye sebule yako na kama usipoipangilia vizuri hutapata matokeo mazuri. huenda ikawa ni kweli. mwaka jana nimenunua home theatre yangu sony Dz 950 pale mlimani city, ina spika nne ndefu na moja kafupi pamoja woofer yake. kwa ushamba wangu nikazitega juu kwenye kingo nne za sebule, kila kona ikawa na spika yake. kile kimoja na woofer yake nikakiweka mbele kwenye sehemu ya Tv ila naona kama sikupata ile ladha halisi inayotakiwa. naombeni utaalamu wa kwenda kuzitega maana mimi ni mpenzi mkubwa wa muziki napokuwa home
Sasa mkuu wewe unataka mziki halafu unaenda kununua home thearte.

Home theater na mziki wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom