Kuna tofauti gani kati ya binaadamu na mtu (watu)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tofauti gani kati ya binaadamu na mtu (watu)?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by hargeisa, Nov 15, 2011.

 1. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Greetthinkers!!!!!!!!!!
  katika pitapita zangu nilikuta mjadala huu wa binadamu na watu ni tofauti;
  kuwa binadamu ni wote wenye ngozi nyeupe na watu ni wote wenye ngozi nyeusi
  kuwa watu walikuwepo kabla ya binaadamu rejea mtu wakwanza alipatikana Tanzania Oldvai george
  hapa naimani mjadala ulee !!!!! utapata ufumbuzi kwa kiwango fulaani!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hii ndo naipata leo lakini nipo tayari kujifunza
   
 3. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  watoto waadamu mmoja baada kumuua mwenzake aliienda nchi ya miitu na kuuoa alioa nanai hi inaaana kuwa kulikuwa na viumbe wengini kama yye
   
 4. A

  Albimany JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Binaadamu ni viumbe vyote vilioko ulimwenguni ambavyo vinasifa za kiutu.(sifa alizonano mtu)

  Mtu Au watu ni binaadamu amae au ambao wako katika eneo maalum katika dunia.

  1)Mfano: binaadamu akitaka lake hazuiliki au haambiliki. (hapa hakuna mpaka binaadamu yupi ni wote)

  2)mfano: watu wa Tanzania ni wakarimu mno.(hapa imewabagua binaadamu sio wote ni wakarimu bali ni wa eneo maalum,Tanzania tu).

  Ahsante
  By Albimany.
   
 5. chengachenga

  chengachenga Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bin adam - an arabic word means "son of adam" Mtu - is a typical swahili word to mean the same. hii ni nomino.
  binaadamu/ ubinaadamu, mtu/ utu pia hutumika kama sifa nzuri. hana utu/ubinaadamu. kumaanisha sifa halisi ya kiumbe mtu/ mwanaadamu ambayo ni ukarimu, upole, huruma na nyingi nyenginezo zinazomtofautisha kiumbe huyo na viumbe wengine kama majini, wanyama nk.
  best wishez
   
 6. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,451
  Likes Received: 4,734
  Trophy Points: 280
  Nikijazia swali, Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu-Afrucan Charter on Human and People's Rights
   
 7. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bin Adam ni kiarabu kumaanisha yeyote atokanaye na Adam.
  Mtu ni kibantu kumaanisha yeyote atokanaye na kundi hili la wabantu. Hivyo, kama tutazama kwa umakini zaidi, siyo kila binadamu ni mtu au mtu ni binadamu. Watu wanaweza kuwa waafrika wa kundi la wabantu na binadamu wanaweza kuwa waarabu. Kawaida maneno haya hutumika interchangeably. Hivyo, kwa msingi huu, huleta maana sawa. Hii ni sawa na neno ustaarabu. Ustaarabu ni kuchukua mila na desturi za kiarabu. Lawafaa waarabu lakini si waswahili. Nadhani siku zijazo tutakuwa na utaafrika.
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wote wawili mmeanza vizuri ila mmekuja kuharibu baadae...
  Ni kweli neno Bin Adam, linatokana na neno la Kiarab Ibnu Adam (kiume) kwa Kihibrania ni Ben Adam, kama mwanamke basi ni bint Adam, ikimaanisha mtoto wa Adam.

  Hii ikimaanisha kuwa sisi sote ni watoto wa Adam...!

  Neno Mtu, linatoka kwenye lugha za Kibantu "Ntu", likimaanisha kiumbe mwenye kujitambua na mwenye uwezo wa kuongea (human being). Ninaposema lugha za Kibantu nina maanisha ni zile lugha zote zinazo zungumzwa kuanzia ukanda wa Afrika toka kusini mpaka kule Kameruni. (Bantu languages) Lugha hizi zimejengwa na zaidi ya makabila 600.

  Waarabu walipokuja Afrika Mashariki na ya kati, walikuwa wakitumia ili neno Bin Adam kuonyesha ustaarabu kuwa wote tumetokana kwa asili ya baba mmoja (Adam). Wangeweza kutumia neno An-Nāsi likimaanisha pia watu (Mankind). Lakini hata hivyo kwa muingiliano wa Lugha za wenyewe (Kibantu) na Lugha za wageni, wakiwemo hao Waarabu, neno Ntu, alikuwachwa nyuma, liliendelea kutumia, na kila lilipotumia lilijikuta linabadirika kimatamshi na kuja kuandikwa Mtu, badala ya Ntu.

  Kama lilivyokuja baadae kubadilika neno Bin Adam, ambalo linabeba maneno mawili, "Bin" na "Adam", na kuunganishwa na kuwa Binadam.

  Hitimisho ni kwamba, neno Watu na neno Binadam, yote yana maana moja tu... Tofauti itakuja tu pale mtu atapotaka kuleta maana zake binafsi.
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Adam alikuwa mtu, yeye hakuwa binadamu. Hapo mwanzo mungu aliumba watu, ambao ni Adam na Hawa. Hawa sio binadamu. Ni watu, watu hawa wakazaa watoto sasa ambao ni binadamu mpaka sasa. Tunajiita watu kwa sababu tu. Tunatokana na mtu ambaye na Adam.
   
 10. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Maneno yote mawili yana maana moja. Binadamu ni neno Rasmi, Na Mtu ni neno ambalo sio rasmi. Kama Stomach na Belly kwenye kingereza.
   
 11. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Mzee, kwa jumla umeeleza vema ila tu nadharia yako ya mabadiliko ya n-tu kuwa m-tu ni yako binafsi kidogo...

  lakini haidhuru kwa swali lililoulizwa.
   
 12. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wa2 ni weeeengi kwel ila binaadamu wachache haswa.
   
 13. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Mtu ni b'dam mkamilifu yaani mwenye akili timam na uwezo wa kutambua mazuri na mabaya mbele ya jamii.
  B'adam ni yule ambae hana hayo alokua nayo mtu. So mtt ni b'adam lkn bado hajawa mtu kamili na mwendawazimu atoshindwa kujitambua nae pia hawezi kuwekwa kwenye kundi la watu.
   
 14. A

  Akasankara JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2016
  Joined: Feb 28, 2015
  Messages: 1,687
  Likes Received: 1,706
  Trophy Points: 280
  umeanza vizuri lakini umehitimisha vibaya. Yaani wewe umeonesha utofauti, halafu unasema "Tofauti itakuja tu pale mtu atapotaka kuleta maana zake binafsi", huku ukisema "Ntu", likimaanisha kiumbe mwenye kujitambua na mwenye uwezo wa kuongea, halafu eti neno Bin Adam huonyesha ustaarabu kuwa wote tumetokana kwa asili ya baba mmoja (Adam).

  Afadhali ungesema kuwa neno "watu" asili yake ni wabantu na neno "binadamu" asili yake ni waarabu ungeeleweka zaidi kuwa hiyo ndo tofauti katika asili lakini maana ni moja. Hata hivyo umejitahidi kwa ufafanuzi mzuri
   
Loading...