Kuna Tofauti Baina ya "Uwongo" na "Kutokuwa Kweli": Tuwe Makini na Matumizi yake Kwenye Mijadala

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,570
19,442
Kusema Uwongo ni tendo kutoa taarifa zisizokuwa kweli kwa makusudi kabisa ili kuficha ukweli. Mtu anayesema uwongo ni mwongo, na akitoa ushahidi wa namna hiyo mahakamani anaweza kuhukumiwa kwa kuidanganya mahakama.

Kutoa taarifa zisizokuwa kweli kwa ama kudhani kuwa ni za kweli kabisa kulingana na unavyozielewa au kwa kutozijua sawasawa siyo uwongo. Mtu anayetoa taarifa za namna hiyo hutambulika kuwa ametoa taarifa ambazo si za kweli lakini si mwongo. Ikiwa mahakamani itagundulika kuwa mtu ametoa ushahidi ambao si wa kweli lakini ni kwa sababu alikuwa ana taarifa mbaya, basi mahakama huukataa ushahidi wake kwamba hana taarifa kamili.

Nimegundua kuwa kwenye mijadala ya kisiasa hapa JF kuna watu kadhaa ambao ni wepesi sana wa kuwaita wenzao waongo kwa taarifa zozote wasizokubaliana. Ukifuatilia sana, mara kadhaa imeonekana wale walio wepesi wa kuita wenzao kuwa ni waongo, huwa mara nyingi pia ni watu wenye uelewa mfupi sana wa jambo lenyewe linalojadiliwa. Huwa wana michango ya kitoto kitoto sana.

Kama huna uhakika kuwa mwenzako hadanganyi kwa makusudi ya kuficha ukweli, basi mwambie tu kuwa "hii siyo kweli" na mwambie kwa nini siyo kweli, usikimbilie kusema kuwa "huu ni uwongo" bila kueleza kwa nini unaamini mtu huyo anaficha ukweli kwa makusudi.

Ni vigumu sana kwenye mijadala hii kujua kama kweli mwenzio anasema uwongo; hivyo ni vizuri tujenge tabia ya kukubali kuwa yeyote anayesema jambo ambao tunadhani kuwa si kweli, basi mtu huyo halijui jambo hilo sawasawa lakini siyo kwamba ni mwongo.
 
Mmmmm!!!, kinyume cha ukweli ni uongo, ni hapo tu ndipo mtu anaweza kudadavua uongo na ukweli.
 
Back
Top Bottom