Kuna 'teja' kwa kila familia Zanzibar-BBC utafiti. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna 'teja' kwa kila familia Zanzibar-BBC utafiti.

Discussion in 'JF Doctor' started by mwalimu Jr., Jul 6, 2009.

 1. m

  mwalimu Jr. Member

  #1
  Jul 6, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  KWA MUJIBU wa Idhaa ya Kiingereza ya BBC kuna mbwia unga mmoja karibu kwa kila familia kisiwani Zanzibar.

  Mara tu siasa ya Ujamaa ilipokufa na Tanzania kufungua milango yake wazi kwa kila aina ya biashara-haramu na halali kuingia nchini-utu, adabu, uungwana na maadili yote kwa ujumla yalitokea dirishani na madawa ya kulevya, umalaya, ulevi, mabaa na pombe, usenge na uhayawani wa kila aina ukaingia kupitia mlangoni.


  Aidha tabia ya viongozi wa CCM ya kuwabagua na kuwaacha watu na hususan vijana wenye akili ambao hawataki kulamba miguu yao kwenye mataa kwa kutowapa fursa za kazi, usanii wala michezo kumechangia kwa kiasi kikubwa 'frustaration' zinazosababisha vijana wengi kuishia kwenye tabia ya kubwia madawa, kuwa wakorofi na wahalifu jambo ambalo kabla ya hapo lilikuwa nadra visiwani humo.

  Jambo jingine ni upinzani kuibiwa ushindi katika chaguzi mbili-tatu zilizopita na Bara kuhakikisha imewarejesha nokoa wao wa visiwani madarakani kwa udi na uvumba ili lisitokee lile ambalo litafanya upinzani bara kuona ala kumbe CCM inang'oleka. Hivi sasa kisiwa hicho kimekaliwa na polisi na askari wengi kutoka bara ambao wakati mwingine hudaiwa kuipigia CCM kura wakati wa uchaguzi.

  Pamoja na CUF kuwa inashinda mara zote katika asilimia 99 ya viti visiwani Pemba, CCM ya Unguja imekataa kata kata kuingia kwenye ubia au mseto au serikali mchanganyiko ili kutumia akili na vipaji vya Wazaznzibari wote kuleta maendeleo ya kweli na uhakika.

  Visiwa vya Unguja na Pemba vina kila sababu ya kuwa Dubai au UAE ya Afrika Mashariki iwapo kutakuwa na haki za binadamu, kuheshimiwa demokrasia na watu wot kupewa fursa za kuchangia katika maendeleo ya visiwa hivyo bila ya ubaguzi wa aina yoyote hili. Hili halijawezekana hadi hivi leo na matokeo yake ni kuwaathiri vijana ambao hukata tamaa na kujiingiza kwenye madhambi mbalimbali ikiwemo hayo ya kujiduna sindano za heroin, ambalo nalo huzua jipya kutokana na watu wengi kuchangia sindano moja ukimwi umeanza kuvamia hususan kisiwa cha Unguja toka kaskazini hadi kusini.

  Familia zilizonusurika ni zile ambazo zimewapeleka watoto wao kusoma na kufanya kazi nje na hivyo kuvinyang'anya visiwa hivyo watu wenye uwezo kiakili na kifikira. Viongozi wengi wa serikali kama walivyo watumishi wengi visiwani humo kwa hivi sasa ni watu wenye sifa zenye mashaka kielimu na kiutaalamu.

  Wachunguzi wa mambo wanaamini laana ya kuwa na mateja kwa kila familia huko Unguja baadhi yao wakiwa wanatokea familia za viongozi na matajiri wakubwa visiwani huko haiwezi kuondoka hadi pale kutakapokuwepo na haki, usawa na uwajibikaji kisiasa visiwani humo.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  sisi familia yetu iko unguja na hakuna mbwia unga

  typical BBC

  washakosa cha kuripoti

  hivi na wao tukisema kuwa BBC swahili kumejaa walevi na wazinzi watakubali?
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  unajiona mzima?
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mbona hawaripoti kuwa kila familia Uingereza ina mabaradhuli na wasagaji?
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  leo nimecheka sana mkuu, u made my day..hahahahahahaha.....lofl
   
 6. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  GT kama kweli upo Unguja hii tathimini ya BBC unaikataa unaonekana wewe ni mbishi wa asili au la upo mbali na jamii ya WASHIRAZI. But for me naikubali kwa 90% kuwa ni ukweli shukuru Mungu familia yako haijaadhirika na hilo janga but Most of young man huko unguja wanatumia sana madawa ya kulevya hii yote wanaifanya kutafuta mbadala wa pombe.Unguja niijuavyo mimi kijana avutae bangi/*******/****** anaonekana msafi kimaadili kuliko anaye kunywa pombe.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 6, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Umekosea kusoma mwandishi amesema 'karibu kila familia' na sio kila familia!
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jul 6, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo unakubali kuwa wapo endapo uingereza watakuwepo? Hueleweki!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 6, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi Zenj hakuna hata baa? Kama zipo kwa nini wanatafuta mbadala wa bia?
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hawana story, karibuni watakuja na habari za ki Al Qaida na Osama bn Laden.
  Usistaajabu wakija wakisema Zanziabar kuna WMDs.
  Wanacho wanachokitafuta, subirini tu karibuni tu.
   
 11. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unastahili kuhamaki ndugu yangu. Lakini kweli wanatuonea. Yaani hata zile familia kule Chanja-njawiri?
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Unajuwa hawa mabazungu wakati mwengine wapuuzi sana, ona basi walivyowaharibu Waganda kule, wamewapelekea ubaradhuli hawatambuani saivi, Nsaba Buturo(waziri wa Maadili, Uganda) kichwa kinamzunguka anahangaika kupeleka mswada bungeni kukomesha tabia hii, nimepata kisa kimoja leo katika VOA Michezo, nchini Uganda, kuna kocha mmoja wa timu ya vijana ameshitakiwa kwa kutaka kumlawiti kijana mmoja kambini, huoni balaa hilo. Mabazungu haya yana haribu mila, silka na tamaduni zetu nzuri za Kiafrika kwa kutuletea mabalaa yao haya ya ushoga, umalaya, usagaji,utumiaji madawa ya kulevya, ujambazi, uhuni n.k kwa visingizio vya haki za binaadamu na uhuru wa mtu kufanya atakalo japo upuuzi. Halafu wanageuka wanafanya stori(documentaries) kama hizi wapate kuuza habari nchi zao. damnit!
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Baa tena? Fanya utembelee huko! Zenj hakuna taputapu, ndio maana tende ipo juu baada konyagi...
  Zamani zile Mahonda iliokoa wengi na Sundown zao....
   
 14. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Simpe statistic ,familia zipo ngapi? Na mateja wapo wangapi? Its very simple.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sehemu iliyoathirika sana na madawa ya kulevya ni Mji Mkongwe na baadhi ya maeneo ya Ng'ambo.
  Iwapo wazenj wote wanaishi maeneo hayo basi kazi ipo
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kusema ukweli jamaa na vijana wengi wameathirika ,huu ni ukweli usiopingika,katika ziara yangu ,nilisikitika sana pale mji mkongwe ,nikikaa JAWS CORNER kunywa kahawa basi swahibu yangu alikuwa akinitajia tu ,yule na yule wote ni waathirika wa unga ,kuna mmoja alipita na magaloni ya maji kama sita hata sijui ameyakamata vipi,kuulizia anakwenda kuchota maji wapi ? Nikamegewa kuwa ,jamaa hana biashara ya maji wala mafuta ,zile ni tasnifa zake tu,na ukiona anahakangaika huku na kule na mageloni basi ujue kuwa tayari amesha nusa. Na centre za kuuzia na nyumba zote ni maarufu sana wala hazihitaji polisi kufanya uchunguzi wa kina ,lakini haya yanaachiwa ili kuiharibu jamii ya Kizanzibari ndilo wanalolitamania machogo cha ajabu zaidi hata Raisi wa Nchi ni Muislamu na hili analijua ,lakini sishangai kwa nini amenyamaza kimya,huenda ikawa nae yanamfurahisha ,wataliana wamejaa tele na karibu wote ni watumiaji wa madawa ya kulevya na serikali inalijua hilo.Nlipofanya ziara Pemba nilikutana na Usalama wa Taifa yeye akifanya kazi katika hoteli au kwa jina wenyewe wanajiita Swahili Divers ,mkubwa wa hapo bazungu ni katili sana na ana majibwa kama ng'ombe na ameishatafunisha wazalendo kibao,usalama huyo akaniambia kuwa huyo jamaa ni mkatili na ni mfanya biashara kubwa wa madawa ya kulevya na kuna safari za boti kutoka hapo na kuelekea Kenya ,unajua Kenya na Pemba ni mwendo kama wa nusu saa au saa moja kwa boti iendayo kasi sasa katika njia hii madawa ya kulevya huwa yanasafirishwa ,ikiwa yatapungua upande mmoja bazungu huyu huwa analetewa au anapeleka ,usalama akazidi kudidimiza kuwa amesharipoti makao makuu ,unajua hawa usalama wa Taifa wanakuwa na simu za aina na anapopiga tu kuna vituo vyao huwa vinapokea ,simu anayopiga inaweza kupokelewa Unguja au Daresalaam na hapo ndipo anapotoa tarifa kamili ya kinachoendelea baada ya kutaja code yake,mwisho akaniambia amebwaga manyanga na haripoti tena maana inaonyesha huenda ikawa ni biashara na wakubwa wamo. Sasa tunaposema sema kuwa serikali inayajua mambo yanayofanywa Zanzibar basi ieleweke yanajulikana vilivyo sio na wao bali hata raia wanafahamu kuwa serikali inayajua na inayaachia kwa sababu wanazozijua wao ,ila wasije wakatwambia ni kutokana na usalama wa Nchi kama yalivyo machimbo ya migodi huko Tanganyika.
   
 17. M

  Mbunge Senior Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inauma jamani. Nchi ambayo watu wangelikuwa na furaha na raha na pengine kastarehe na kaanasa hiki na kile sasa ni nchi ya karaha na vipofu ngio viongozi. Angalia kinachoendelea pale Saateni na uongo au ukweli wa jinsi viongozi wetu wanavyochota fedha za ZSSF na mashirika mengine hayo na kuzifuja au kuziwekeza kama zao ili wao na matoto yao waje kunufaika baadaye! Mungu yupo na atatulipia hili kungali mchana kweupe!!!
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..inawezekani ni interpretation tu ya data za idadi ya mateja wa unga vs idadi ya kaya ZNZ.

  ..inawezekana kuna familia hazina mateja kabisa, halafu nyingine zina mateja 2 au 3, nyingine teja mmoja etc etc.

  ..unapoambiwa kwamba asilimia 25% ya mji fulani wana virusi vya ukimwi, haina maana kwamba lazima, lazima, kila penye mkusanyiko wa watu 100 ktk mji huo, 25 watakuwa na vvu. idadi hiyo inaweza kupanda au hata kupungua ktk mkusanyiko huo.


  ..tatizo hili inaonekana lipo ZNZ. sasa ni vyema likashughulikiwa hata kama si kubwa kama lilivyoripotiwa BBC.
   
 19. z

  zanzibar 62 Member

  #19
  Jul 8, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bbc swahili imejaa laana sasa.

  kuna watu humo wanaotetea hata mashoga na kusema eti wana sehem mbili za siri na hizo wamepewa na mungu.

  mwanamama mmoja wa tz mtangazaji wa bbc akiwatetea mashoga.

  na hao mashoga wakitizamwa wana alama kama kawaida ila hujitunga sindano na kufanya maziwa au wengine kubandika maziwa kwa njia ya operesheni.

  ali saleh kutoka zanzibar bbc. akijua fika historia ya zanzibar akiupigia debe ukafiri na kushirikiana na kuwapamba wakafiri na kupotosha ukweli wa zanzibar pamoja na kafiri anayemuoji. hii yote ni kuchunga ugali wake ili asikose kula kupitia bbc.

  bbc ni uzushi na kueneza habari nyingi za uongo na kupendelea upotofu hii yote ni kufaziliwa na na makafiri na kupotosha ukweli.

  zanzibar unga unauzwa wala hakuna kodi yoyote wanayolipa wauza unga. na ajira hakuna kwa wazanzibar ila wageni bila ya utaratibu wowote.

  hakuna utaratibu wowote hakujulikani mzanzibar. mganda, mkenya, mrundi, mrandwa wala wawest afrika pamoja na huu muungano.

  nchi haina sheria

  na huyu jamaa yangu anadai kwao hakuna mla unga lakini ukiruka milango jamaa zake wengine wala unga.
   
 20. z

  zanzibar 62 Member

  #20
  Jul 8, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani hujasikia dada yetu kutoka tz kwenye bbc litumwa atangase eti wana jinsia mbili wamepewa na mungu.

  sisi tunaisikiliza na uzushi wao.

  hao mashoga na wasukumamavi ndio maboss wao.

  hawatangazi watawatetea eti wana jinsia mbili wameumba nazo na mungu hii ndio bbc inavyotufundisha
   
Loading...