Kuna tatizo la Miamala kukwama huku pesa zikikatwa na mitandao

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
17,410
2,000
Mtu unaamka unataka kununua umeme au maji kwa kupitia mtandao wa Airtel au VodaCom. Unafanya manunuzi unaambiwa muhamala haujafanikiwa lakini pesa wanakata. Halafu ukiwapigia simu huduma kwa wateja wanasema watarudisha muhamala huo ndani ya masaa 96 ya kazi yaani siku nne.

Kipindi cha nyuma tatizo kama hili likitokea pesa ilikuwa haikatwi kabisa (Nadra sana na likitokea aidha utapata huduma kwa haraka au pesa yako), lakini siku hizi wanakata hata mara mbili bila kuogopa.

Hili tatizo lingekuwa linatokea kwa nadra basi tungesema ni bahati mbaya, lakini linatokea mara nyingi sana na wanakata pesa zetu nyingi na huduma hatupati. Kibaya zaidi huu uzembe hauchukuliwi kabisa hatua na mamlaka husika. Ila bahati mbaya sisi wengine tuna masikio makubwa na tumeanza kupata minong'ono ya kinachoendelea nyuma ya pazia: Sababu zinazopelekea haka kamchezo kufanyika lakini tukaamua kuzipuuza.

Sisi yetu macho.
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,513
2,000
That is fraud and scum. It shouldn't be tolerated at all cost. The sad thing is authorities are turning a blind eye and deaf ears to these atrocities. They should know when dealing with issues concerning money its like dealing with issues pertaining national importance.

I call upon to all who are indulging in this scumbag thuggery to stop at once. Or else deliberate measures, action and force will be used and applied.

As a nation and majority of law abiding citizens we will never succumb to these mischievous acts of bunch of thieves and we are going to be very strict on this and if the situation persists then we have no choice but to land very heavily on the culprits and the impact will be devastating.

Chaliifrancisco Magonjwa Mtambuka LaRosa
 

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
409
1,000
Juzi imenitokea Airtel muamala umekwama na Makato wamekatwa waliporejesha wakarejesha Tu Ile niliyotuma, maanake ni kwamba nilirudia transaction ya pili Kwa Makato mengine. Hivo huo muamala niliugharamia mara mbili.
 

clixus

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
747
500
Mimi Leo hii imenikuta, then ukiwapigia simu Airtel namba hazipokelew

Weekend hii kukaa bila umeme inaboa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom