Kuna tatizo kwenye vyama vyetu vya wafanyakazi

Mzee Kipara

Member
Jan 3, 2011
83
43
Hivi vyama vya wafanyakazi Tanzania navishangaa sana, tunakatwa mshahara kuvilipia ili vitutetee lakini havifanyi hivyo. Najaribu kutafakari maamuzi ya serikali ambayo yalipaswa kuwasha moto kwenye vyama vya wafanyakazi lakini viko kimya
  • Kusitishwa kwa ajira kwa watu waliokuwa wameshapewa barua za ajira (na mpaka leo hawaelewi hatima yao ni nini)
  • Kusitisha upandaji madaraja kwa wafanyakazi serikalini
  • Kusimamisha malipo ya malimbikizo ya nyuma kwa wafanyakazi
  • Kusimamishwa kwa ajira serikalini
Hivi kama vyama vya wafanyakazi haviwezi kututetea katika hayo, vinasubiri mpaka kifanyike nini ndo vitutetee??????
 
Siyo vyama vya wafanyakazi, hata wabunge na vyama vya upinzanini hawalipigii kelele za kutsha hili swala, mimi ningeunga mkona maandamano ya kushinikiza serikali iruhusu ajira kuliko maandamano ya ukuta.
 
Back
Top Bottom